Jenista Mhagama: Dkt Mollel ni msaada mkubwa kwangu, anaitendea haki Sekta ya Afya

Jenista Mhagama: Dkt Mollel ni msaada mkubwa kwangu, anaitendea haki Sekta ya Afya

DodomaTZ

Senior Member
Joined
May 20, 2022
Posts
161
Reaction score
200


Waziri wa Afya, Jenista Mhagama amempongeza Naibu Waziri wake, Dkt. Godwin Mollel na kueleza kuwa anaitendea haki nafasi yake hiyo na amekuwa msaada mkubwa kwake.

Amesema hayo Aprili 8, 2025 ambapo amekabidhi zawadi kwa mikoa, wilaya, vijiji na shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu katika utunzaji wa mazingira pamoja na Hospitali za Kanda, Hospitali za wilaya, mikoa, vituo vya afya na zahanati katika utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi.

Tuzo hizo amezitoa wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Afya Kitaifa yaliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Katika utoaji wa Tuzo hizo Mhagama ameambatana na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tamisemi- Afya Mhe. Dkt. Festo Dugange, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe, Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe pamoja Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule.
 
Back
Top Bottom