Jengo walilopanga CHADEMA kama Ofisi, Mtaa wa Ufipa Kinondoni ni la Nani na kodi yake ni kiasi gani?

Chuo ni mhimu sana, si watu wote wamepita vyuo vya kawaida, viongozi wanahitajika ni wengi kwa ngazi mbalimbali, kila mtu kujibunia style ya uongozi si approach nzuri, ni kama inhouse traing ya kampuni japo kila mtu ni proffesional. Chadema then tekelezeni as soon as possible.
 
Wajenge hicho chuo halafu waone kama ndio kitawapatia ushindi 2015! Maana ingekuwa ni elimu ya uongozi tu sijui wangapi wanajua jinsi CCM ilivyosomesha watu wake kuanzia Bulgaria, Yugoslavia (ya zamani) na kupitia Chuo chake cha Chama Kivukoni. Guess how they turned out.. Jeshi lilisoleweza kujipanga kuanzia kwenye makao makuu yake linaweza vipi kushindana na jeshi ambalo limejipanga vizuri?

Tatizo bado watu hawajaamua kukaa tayari kumuelewa adui yao - CCM na jinsi gani CCM imejipanga na itajipanga kushinda tena 2015. Wakati nyinyi mnajenga Chuo cha Maadiili wenzenu wanajijenga upya kuanzia makao makuu.. just watch. Kama mnataka kutoa elimu ya maadili, andaeni warsha, semina n.k kwa viongozi wenu hata kozi za wiki moja au mwezi mmoja ambazo chama kingeweza kutoa ruzuku na kiasi kingine kinalipwa na wahudhuriaji wenyewe.

Believe me Chuo cha Maadili ya viongozi is a waste of scarce resources. It is strategically misconceived.
 
Mie nilishaanza siku nyingi kuwa:

NAOMBA MAKAO MAKUU YA CHADEMA YAJENGWE TABORA.

Sisemi Sikonge maana huko ni mbali sana hasa mvua ikinyesha.

Tabora kunafikika kwa barabara, Ndege na Train.

Makao makuu ya Chadema yataweza kuupa mkoa huu masikini changamoto ya maendeleo.

Zaidi, angalia sahihi yangu. Nimekuwa naandika Post kibao ili watu wasome sahihi yangu......

Nina imani kuna watu wataunga mkono. Ahhh, Tabora maeneo ya kujenga siyo shinda sana.

Nafahamu itakuwa kasheshe kupata kibali kwani CCM imeshika hatamu.

Penye nia pana njia. CHADEMA KARIBUNI UNYANYEMBE HQ (TABORA).
 
Mzee Mwanakijiji, mbona umemaliza yote!!!

Mzee Sabodo, wawekezaji waadilifu na wananchi wengine wahisani (Mzee Ndesamburo ukiwemo), CHADEMA kijenge Makao Makuu (Nguvu ya Umma Plaza) kwenye Jimbo la Mhe Mnyika Ubungo karibu na eneo la Malamba Mawili (kukwepa foleni, mrundikano katikati ya jiji, kukingia neema za Satelite City zinazozungumzwa kila siku huko) ili kuonyesha ubunifu katika hilo pia kulinda lango kuu la Jiji la Dar es Salaam.

Huko mashirika yatakayohitaji miofisi hayana idadi, wafanyabiashara watakaohitaji eneo nadhifu la kutolea huduma kwa wateja wanaotokea mikoani usiseme, wananchi waishio pembezoni mwa mjii wanaochukia foleni za sasa hivi lakini hururaha huduma katika maeneo mazuri no ndio hivyo. Cha zaidi, mwenye wazo lake ni mwanakijiji atawaeleza zaidi alichokiota kuhusu 'Command Centre' ya kueleweka. Mimi kama Mwana-JF mwenzake, wazo nimeliunga mkono.

Cha msingi tafuteni kiwanja kipana sana kisha mtangaze kutafuta wabia watakaojenga ghorofa yenye idadi sawa na wabunge wote (wa kuchaguliwa na kuteuliwa) wa CHADEMA wa sasa kuliobarikiwa na Mungu safari hii baada ya uchakachuzi. Utaratibu ukiwekwa vizuri basi hata sisi wanachama tu tukauziwa hisa (zinazolindwa kisheria) basi jengo la kisasa tutaliporomosha tu.

Huku ndio kukubalika huko na umma wa Tanzania na kuleta maana kamili ya WANANCHI PLAZA / NGUVU YA UMMA PLAZA. Chapu basi!!
 
Uwezo Tunao.. ulichosema kinaakisi kabisa jina lako! Nimependa hadi mapendekezo ya mahali. Tunaotaka Chadema kifanye vizuri 2015 tupinge hili la Chuo cha Maadili na tuweke presha kwenye ujenzi wa Makao Makuu mapya. Yaani nakumbuka kama kwa soni siku wanamtangaza Dr. Slaa kuwa mgombea wa Urais - walifanyia uani! Angalia picha.
 
Hiyo ndiyo inavyoonyesha ni jinsi gani hivi vyama vya upinzani TZ havina mwelekeo mzuri. Kama hawawazi kujenga makao makuu yao, je wataweza kujenga nchi?
 
Na hakuna vyuo Tanzania ambavyo vingeweza kutoa elimu hiyo katika Tanzania au East Africa? Kipi ni kitega uchumi bora kati ya chuo na shule ya sekondari ya kisasa? Katika ushindani huu wa vyuo chuo cha maadili cha Chadema kitaweza kuhimili mikiki mikiki ya kushindana kitaaluma na vyuo vingine hapo au itatoa kozi kwa wana Chadema tu? Jamani hata Chuo cha Chama Kivukoni kilibadilishwa! Ninaamini kozi za maadili n.k haziitaji chuo Unless kama ni sehemu ya elimu nyingine rasmi (kama kozi ya shahada n.k). Vinginevyo, kozi hizo au mafunzo hayo yanaweza kutolewa hapo makao makuu ya chama (kutakuwa na conference halls i hope) n.k

Sijui umepata wapi wazo la kuwa na makao makuu makubwa kama yale ya Dodoma. Utaona kuwa sikutumia neno "makubwa" wala sikulinganisha na ya "CCM". NImesema makao makuu ya kisasa! yanaweza kuwa madogo kwa kukidhi mahitaji na hayahitaji kuwa kama ya CCM Dodoma. Yanahitaji kuwa ya kisasa - ina maana gani?

well.. I just said the same thing better - Chadema wajenge makao makuu mapya, ya kisasa. Wewe umeweka kachumbari na limau. Thanks.

Unakubaliana na mimi kuliko unavyopingana nami.

Safi kabisa. U see.. Chadema inahitaji kujenga makao makuu mapya ya kisasa. Thanks.

Nilikurupuka Mzee
sikukuelewa vizuri, nadhani tunaimba shairi moja lakini beats ndo zipo tofauti
ingawa bado naamini chuo ni muhimu sana kwani knowledge is power.
 
Nilikurupuka Mzee
sikukuelewa vizuri, nadhani tunaimba shairi moja lakini beats ndo zipo tofauti
ingawa bado naamini chuo ni muhimu sana kwani knowledge is power.

absolutely.. lakini hawa walioko madarakani sasa unajua wamepitia vyuo vingapi; na wana knowledge kiasi gani, for starters Chenge ni Harvard alumnus!
 
Watu wanasikitisha saana... Yaani hawaamini maadili waweza kufundishwa chuo???!! Lakini nijuavyo mimi chama kama chama kina misingi yake ambayo watu wengi hawaijui...sasa ni wakati muafaka kuwafundisha watu maana ya ILANI, mikataba na Katiba na mambo kama hayo watu wajue vizuri ili wakafundishe wenzao mtaaani... Lakini chuo hichi si cha kila mtu ni viongozi tuu wa CHADEMA wa ngazi mbalimbali... Hata CCM wanacho kama hiki kinasaidia kukuza kujiamini na ujasiri wa mtuuu

Kuhusu makao makuu ya ''kisasa''.. Mimi napinga kwa kuwa kuishi nyumba au kufanya kazi ya kawaida sio kufa huko... Hata Tajiri namba moja duniani anaishi kwenye nyumba ya dola 35,000 tuu aliyonunua mwaka 1958 kule marekani lakini bado maisha yanaenda.... Watanzania Tatizo letu ni kupenda kuwa wajisiriamali ndo maana tunakuwa mafisadi... Kuna haja ya kujua maana ya jengo la "biashara" na ofisi ya chama cha siasa..
CCM wameiba majengo yoote mijini huko mikoani ili wawekeze mahela lakini Biashara na Siasa si vitu sawa hata tone japo waweza kuwa mfanyabbiashara pia mwanasiasa...

MwanaKijiji nimekuelewa sana unataka watu wakae kwenye AC na nyumba ya Tiles yenye vigae juu na pia ukuta mweupe usio na Chooping lakini kumbuka vyoote hivi vina gharama zake hebu waza kila mtu akija kutoka makao makuu kutaka angalau akaweke tiles kwenye ofisi ya CHADEMA....
Hapa ni vita ya hoja sio vita ... Tafadhali mali na utajiri ni vitu vya dunia hii kamwe havitafika ufalme wa mbinguni kwa Mungu baba... Mungu Allah mwenyeenzi na rehma...
 
Ni kweli kabisa mkuu Mwanakijiji.
Kwa kweli Chadema inahitaji ofisi ya makao makuu yenye hadhi kabla 2015. Nakumbuka wakati wa mchakato wa kuelekea uchaguzi mkuu ofisi ile ilikuwa haitoshi kabisa kulingana na wingi wa watu na mlundikano wa vifaa ka kweli utaratibu ulikuwa bado sana. hata namna ya kupata vifaa ilikuwa shida mpaka nikakata tamaa. tuanze sasa kuijenga chadema tayari kwa kushika madaraka makubwa zaidi.
 
...Nadhani issue ya ujenzi wa chuo imechukuliwa juu juu tu. Kuna anayefahamu kitakuwa na ukubwa na uwezo gani? Je, makao makuu ni muhimu sana zaidi ya kuwanoa watendaji ulionao katika medani za uongozi.

...Nyingi ya shughuli zilizotajwa kama excuse ya kujenga makao makuu zinaweza kufanyika katika chuo hicho....yes, hata organization ya uchaguzi/chaguzi.

...Issue kubwa ya handling ya uchaguzi uliopita haikuwa kutokuwa na HQ kubwa na ya kisasa, bali upungufu katika organization ya kampeni zote. Zilikuwa decentralized sana, kidogo ingefaa, sio sana.

...Somo. Umahiri wa kampeni za Obama haukuwa katika ukubwa wa HQ or whatever, bali kwenye organization nzuri na ya kisasa ya kampeni.
 
Wajenge Dar Es Salaam

Kamao Makuu yawe ya kisasa, tena yawe kwenye uwanja au ardhi ya makumi ya eka kujiandaa na miaka mia ijayo na si kama tulivyo sasa, wafikirie kuwa na chuo, tasisi mbalimbali za maendeleo nk in one stop
 
Wajenge hicho chuo halafu waone kama ndio kitawapatia ushindi 2015! Maana ingekuwa ni elimu ya uongozi tu sijui wangapi wanajua jinsi CCM ilivyosomesha watu wake kuanzia Bulgaria, Yugoslavia (ya zamani) na kupitia Chuo chake cha Chama Kivukoni. Guess how they turned out.. Jeshi lilisoleweza kujipanga kuanzia kwenye makao makuu yake linaweza vipi kushindana na jeshi ambalo limejipanga vizuri?

Tatizo bado watu hawajaamua kukaa tayari kumuelewa adui yao - CCM na jinsi gani CCM imejipanga na itajipanga kushinda tena 2015. Wakati nyinyi mnajenga Chuo cha Maadiili wenzenu wanajijenga upya kuanzia makao makuu.. just watch. Kama mnataka kutoa elimu ya maadili, andaeni warsha, semina n.k kwa viongozi wenu hata kozi za wiki moja au mwezi mmoja ambazo chama kingeweza kutoa ruzuku na kiasi kingine kinalipwa na wahudhuriaji wenyewe.

Believe me Chuo cha Maadili ya viongozi is a waste of scarce resources. It is strategically misconceived.

MM The problem inside CDM is leadership deficiency. They need visionary leader who understand CCM politics from head to toe, i doubt even if CDM knows the urgency of change that is within Tanzanian.
 
Na hakuna vyuo Tanzania ambavyo vingeweza kutoa elimu hiyo katika Tanzania au East Africa? Kipi ni kitega uchumi bora kati ya chuo na shule ya sekondari ya kisasa? Katika ushindani huu wa vyuo chuo cha maadili cha Chadema kitaweza kuhimili mikiki mikiki ya kushindana kitaaluma na vyuo vingine hapo au itatoa kozi kwa wana Chadema tu? Jamani hata Chuo cha Chama Kivukoni kilibadilishwa! Ninaamini kozi za maadili n.k haziitaji chuo Unless kama ni sehemu ya elimu nyingine rasmi (kama kozi ya shahada n.k). Vinginevyo, kozi hizo au mafunzo hayo yanaweza kutolewa hapo makao makuu ya chama (kutakuwa na conference halls i hope) n.k

Sijui umepata wapi wazo la kuwa na makao makuu makubwa kama yale ya Dodoma. Utaona kuwa sikutumia neno "makubwa" wala sikulinganisha na ya "CCM". NImesema makao makuu ya kisasa! yanaweza kuwa madogo kwa kukidhi mahitaji na hayahitaji kuwa kama ya CCM Dodoma. Yanahitaji kuwa ya kisasa - ina maana gani?

well.. I just said the same thing better - Chadema wajenge makao makuu mapya, ya kisasa. Wewe umeweka kachumbari na limau. Thanks.

Unakubaliana na mimi kuliko unavyopingana nami.

Safi kabisa. U see.. Chadema inahitaji kujenga makao makuu mapya ya kisasa. Thanks.

Jamani mi nadhani kama sijakosea hizo milioni 150 according to wishes za mfadhili ni kutumika kujenga chuo cha maadili. Tusikiuke wishes zake, CHADEMA itakuwa ime misuse funds kwani ni kinyume la lengo la mfadhili. Hata siku nyingine watajikosesha misaada zaidi. Hili ndo tatizo kubwa la ugomvi wa donors na Waafrika, wana misuse funds. Kama wanataka makao makuu wabuni njia nyingine ya kupata funds kwa jambo hilo.
 
Naunga mkono ujenzi wa ofisi ya makao makuu ya people's power -chadema inaweza hilo kwa sasa kwa kutumia peoples power ni muhimu sana. Niliwambia chadema ni taasisi na watanzania wana matumaini nalo ndio maana hatujadili cuf au tlp tunajua wale ni njaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa tupu hawako kwa maslahi ya umma.
 
Wana JF,
Wiki mbili zilizopita nilipata wageni kutoka Uingereza, wana Asasi yao ya mambo ya siasa ya jamii wakaniomba niwapeleke makao makuu ya Chadema nilichokikuta ni aibu tupu wageni wangu wakabaki wanacheka kwa dhiaka, Ofisi ipo uswahilini kinondoni mtaa wa ufipa (manyanya) Ofisi ya vyumba vitatu, utadhani ni Saccos, Chadema wanapata Ruzuku kwa mwezi milioni 203.6 kwa mwaka milioni 809,545,848. kwa nini wanashindwa kujenga ofisi? wanashindwa na CUF wanapokea Ruzuku milioni 117.4 kwa mwezi wamejenga jengo lao buguruni, Hali hii makao makuu ya Chadema yapo hivi je mikoani kuna hali gani? pesa yote inaenda kwenye maandamano na posho mnatafuna kodi zetu Watanzania. ofisi mbovu inavuja mnashindwa na UPDP, wamepanga jengo zima wamefanya ofisi
 
Wana JF,
Wiki mbili zilizopita nilipata wageni kutoka Uingereza, wana Asasi yao ya mambo ya siasa ya jamii wakaniomba niwapeleke makao makuu ya Chadema nilichokikuta ni aibu tupu wageni wangu wakabaki wanacheka kwa dhiaka, Ofisi ipo uswahilini kinondoni mtaa wa ufipa (manyanya) ya vyumba vitatu, utadhani ni Saccos, Chadema wanapata Ruzuku kwa mwezi milioni 203.6 kwa mwaka milioni 809,545,848. kwa nini wanashindwa kujenga ofisi? wanashindwa na CUF wanapokea Ruzuku milioni 117.4 kwa mwezi wamejenga jengo lao buguruni, Hali hii makao makuu ya Chadema yapo hivi je mikoani kuna hali gani? pesa yote inaenda kwenye maandamano na posho mnatafuna kodi zetu Watanzania. ofisi mbovu inavuja mnashindwa na UPDP, wamepanga jengo zima wamefanya ofisi

Rephrase your writings!
 
Back
Top Bottom