Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Baada ya kusikia habari kuwa CHADEMA wana mpango wa kujenga Chuo cha Maadili ya viongozi kwa heshima ya Bw. Sabodo aliyeahidi kuwachangia shilingi 150 nimejikuta nikitamani kunyofoa nywele zangu kichwani. Kati ya vitu vya kwanza ambavyo ninaamini Chadema wanahitaji kwa haraka zaidi ni makao makuu ya kisasa ya chama kinachojiandaa kutawala.
Ninaposema "makao makuu ya kisasa" nina maana ya jengo na mazingira yanayoendana na hadhi ambayo Chadema imejijengea sasa hivi lakini vile vile mahali ambapo kuna miundombinu ya kisasa vile vile. Lakini zaidi pia kujenga makao makuu ambayo hayatokuwa ofisi tu bali pia sehemu ya kitega uchumi.
Wapo wanaofikiri kula makao makuu sii kitu cha muhimu au si jambo la haraka kabisa. Wanafikiri wataendelea kujiandaa kushinda kwa kutumia vibanda vya nyasi na kutoa matangazo ya mipango yao kutoka uani! Chadema kama kinataka kianze kujipanga kiukweli sasa basi la kwanza ni kuandaa a modern command center. Nitawaachia wengine wafikirie makao makuu ya kisasa yaweje.
Lakini ukiniuliza mimi.. kati ya vitu vya kwanza kabisa vya kujiandaa na vitatupa mwanga kuwa sasa kweli CHadema inataka kushinda utawala wa nchi ni jinsi gani inajiandaa kwa makao yake makuu na kutoka hapo ofisi zake za ngazi za chini. Wakijenga hayo makao makuu basi wanaweza kuwa na sehemu ya mafunzo ambapo mafunzo ya maadili na mengine yataweza kutolewa.
======
Jan 8, 2014
WanaJF,
Ni takribani mwaka mmoja na nusu sasa tangu Mfanyabiashara maarufu nchini ndugu Sabodo kuahidi kuwa atasaidia kwa hali na mali katika ujenzi wa ofisi za makao makuu ya CHADEMA.
Ndugu Sabodo alitoa ahadi hiyo alipokuwa amealikwa na CHADEMA katika hafla fulani ambapo alisema kwamba pamoja na kwamba yeye ni kada wa CCM lakini ana imani kubwa na CHADEMA na kwenda mbali zaidi kuitabilia ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Kutokana na imani yake kwa CHADEMA, Ndugu Sabodo aliahidi kuisaidia CHADEMA kupata ama kujenga ofisi za kisasa makao makuu ya CHADEMA.
Tangu siku ile sijasikia tena Sabodo wala CHADEMA kuzungumzia hatua zilizofikiwa ili kufikia adhima hiyo.
Naomba msemaji wa Chama,au Kurugenzi ya Habari chadema ama Sabodo mwenyewe kama ni member wa jamii Forum kulitolea ufafanuzi na maelezo ya kutosha.
Nawasilisha.