nizakale
JF-Expert Member
- Oct 23, 2019
- 4,029
- 2,902
Inasikitisha lakini ndio hivyo tena kwamba jengo la serikali linaezekwa kwa mabati meupe ! Hii ni fedheha kwa jiji La Mwanza ambao ndio wenye mradi huu. Tunajua kwamba majengo ya serikali iwe ni shule, vituo vya afya au hospitali huezekwa kwa mabati ya rangi. Leo hii jengo la stand limeezekwa kwa mabati meupe hadi kuyatazama tu yanaumiza macho. Viongozi wa mkoa kuanzia mkuu wa mkoa, mbunge wa Nyamagana, Mkurugenzi wa Jiji wako kimya kabisa wakati madudu haya yakifanyika. Tunaomba waziri anayehusika na TAMISENI atembelee mradi huu ili aone kinachoendelea hapa.