Jengo la NSSF Moshi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jengo la NSSF Moshi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mamzalendo, Sep 28, 2012.

 1. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Habari wakuu leo nina tafakari kidogo nimeambiwa jengo linalojengwa opposite na manispaa ya moshi ni la nssf na linaenda ghorofa kumi na ni commercial complex,nimeliona lakini najiuliza litalipa na kama litalipa kwa kiasi gani?kama majengo tu ya kawaida ni vigumu kufanya renovation je litalipa kiasi cha kumudu periodic maintenance au its just a waste of money,embu kama kuna mwenye any economic survey au business plan ya jinsi itakavyolipa maana i dont see any business worthy that investment,but i stand to be corrected and educated,
   
 2. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  Jengo lile linajengwa na kandarasi wawili kwa joint venture JV ... Group Six ya China na ADVENT Construction .... dah ... sijui kama investment will worth with time ... will the rate of return be considerable?
   
 3. m

  massai JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Lazima litadoda lile,moshi ngo's zipo chache mno,biashara yenyewe slow sana,jengo lenyewe kama mlimani city sijui...labda wafanye apartment na bado halitajaa.
   
 4. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hata mimi nimewaza kwa kweli,nadhani linahitaji kuangaliwa tena,kabla ya kuendelea kuwekeza,a man without vision is a nightmare,we need to rethink n convince ourselves for the coming years,
   
 5. d

  dkn Senior Member

  #5
  Sep 28, 2012
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 132
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  business environment yetu na culture yetu kidogo itakuwa ngumu kwa majengo kama haya kuwa complex business centres. Ninachoona mimi jengo kama hilo Moshi hata kwa ofisi za kawaida bado kwani Moshi haina mashirika, viwanda, migodi etc wa kuweza kupata entrepreneurs kufungua ofisi zao hapo. Angalia mfano wa biashara ndogo ndogo, wamachinga kwenda kuwaweka kwenye complex kama hizo italipa, watu wetu wanataka kufanya biashara nje kuonekana na pia customers wana mentality kitu kikiuzwa sehemu kama hiyo ni bei ghali bora kwenda sokoni nje ni bei poa. Nafikiria hatujafikia level kama hiyo, bidhaa zetu, quality na advertisement bado. Complex kama hizo kwanza serikali isaidie kuelemisha watu business development, planning, advertising na kuweka centres za bidhaa kwa categories mfano kwa mji wa Moshi kama unatafuta vifaa vya ujenzi kama rangi utaipata kwenye hiyo complex floor moja na wafanyabiashara wote wako hapo
   
 6. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2012
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  May be another ufisadi!
  Lets wait and see
   
 7. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Ujenzi wa majengo kwa security funds zetu ni chakula ya wazee!!! Likimalizika wahusika wote ni lazima wawe na ghorofa kila mmoja somewhere!!! Ha ha ha michango at ufisadi!!
   
 8. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #8
  Sep 28, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Dkn upo sahihi kabisa kuna haja ya kubadili mitizamo,na je itachukua muda gani kabla halijakongoroka,tukiweza kufumua yale maviwanda yote yaliyokufa kwenye barabara ya kutoka memorial kwenda tpc,we can expect at least something,kahawa house yenyewe sijui kama imejaa,masupermarket sijui kama yanafanya vizuri may be nakumat,
   
 9. d

  dkn Senior Member

  #9
  Sep 28, 2012
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 132
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  hizi investments wanazofanya NSSF kwa hela za wanachama na kutoa mikopo mashirika ambayo inaonekana kabisa chances za kurudisha hela ni ngumu huu ni ufisadi. tutaona mengi waliokopa NSSF watatumia hela then watafilisika hela zimepotea, jiulize mbona wasikope benki kama ADB kwa daraja la kigamboni? kuna projects nyingi zinatakiwa zifanyike kwenye kukusanya kodi lakini wanakimbilia hela za wanachama kwasababu hazina zengwe. NSSF ingefanya kazi bila kuingiliwa na serikali kwenye miradi kama hiyo nafikiri ni shinikizo la serikali lakini hailipi kabisa kuwa na complex kama hizo mara 100 wangefikiria hata hotels au shule, vyuo return yake inaeleweka.
   
 10. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  jamani kama kweli basi hizi laana hazitamalizika katika nchi yetu,yaani ni mabilioni ina maana watu ni vipofu hawaoni halitalipa?au wananchi tukatae?tunahitaji wazalendo katika kila fani tungepata kikundi cha wana uchumi wakatathimini tungekuwa na point za kulipinga otherwise ni ufujaji ya hela za wananchi,
   
 11. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #11
  Sep 28, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kweli angalao hostels lakini hata hvyo vyuo vingapi moshi vitalijaza,dah watanzania tunahitaji kufikiri na kufikiri,na si kila kitu ndio kuna neno hapana pia lazima litumike,sasa tufanyaje dkn?
   
 12. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #12
  Sep 28, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mamzalendo, who cares in Tanzania nowdays? Kila mtu akipata nafasi anakwapua tu maana hata katika mikataba ya madini, gesi, umeme, vitalu vya wanyama kote ni wizi tu. Aliyekuwa na uchungu na nchi hii kwa sasa ni marehemu na kila tarehe 14 October tunakumbuka mengi yake. Mungu akulaze mahali pema peponi baba yangu uliyenipa elimu na afya hadi leo ninajitegemea big!!! Sijui ingekuwa leo kama ningekanyaga shule!!
   
 13. d

  dkn Senior Member

  #13
  Sep 28, 2012
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 132
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mamzalendo na Zogwale nakubaliana na nyie na uchungu wa nchi yetu, tatizo kubwa ni mfumo. Labda mnikosoe kama nimekosea, miaka ya 90, 80 na 2000 ilikuwa ni rahisi kupitisha hoja kwani wabunge walikuwa wa chama kimoja. Sasa hivi mimi na wanaJF tunaongea haya kwa sababu ya technologia ya mawasiliano imetupa uwezo wa kuchangia mengi. Mfano hela za NSSF ni za wanachama, nani anawakilisha wanachama kwenye maamuzi ya miradi kama hiyo? hakuna hata mmoja ni sijui directors wanaoteuliwa na Rais (tena wengi wa kwa kujuana na wanaua kabisa mashirika ya umma aliyoacha mwalimu). Sasa hivi tuna chances kubwa za kutumia bunge kwa kuwa kuna wapinzani na sisi pia humu kwenye forums na forums nyingine tunasikika ingawa hatupo huko. Projects kama hizo ziletwe bungeni, jamani tunataka kufanya mradi huu kwa pesa za NSSF italeta faida hii na hii na wastaafu wetu watakuwa kwenye maisha mazuri kutokana na faida. Project inawekwa mezani inapitiwa na kurekebishwa na kuwa approved, sidhani kama wabunge wote watakuwa mambumbumbu kukubali kila kitu bila ku scrutinize. Tatizo kubwa viongozi wana maslahi yao, hata kama kuna upungufu watakubali tu ifanikiwe hata kuhonga na ikipita kwa Rais yeye ni kuletewa hotuba kusoma na shallow benefits ya mradi kama wa NSSF na simlaumu kwani yeye siyo technical person anategemea aliowachagua kesho tunalalamika Rais alifanya hivi leo lile jengo halina watu au watu wamekataa kufanya biashara hapo basi utasikia jengo limebinafsishwa na mtu analipa pesa ndogo, na watu private wakipata hiyo opportunity wanafanya vitu vya ajabu na kutajirika faster kwani wako creative na innovative nini cha kufanya hapo na wanaangalia faida siyo sisi kupata sifa na kuiba kwenye miradi kama hiyo. Unaweza kuamini serikali inatoa tender labda ya vifaa kama sh. milioni 100 na bidhaa hiyo hiyo inauzwa milioni 40, mfanyabiashara anaondoka ma million 60 faida, gap ni kubwa lakini katikati kuna watu wanakula..nchi imeoza hakuna uzalendo natamani sana capitalism angalau majirani zetu Kenya wanasiasa wana hela zao hata wasipofanya siasa na kuiba ni ngumu kwani kila kitu kiko wazi.
   
 14. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #14
  Sep 29, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  yote haya ni kukosa vision maana tungejiuliza tu kila m2 akiwa hajali hatima ni nini?sasa inabidi pawepo mkakati wa kurudisha akili za watu,jana tulikuwa tunatafakari yaani kuna ujinga ukiufikiria unaona si ujinga labda ni laana,mtu ambaye ni mchoyo hata kwa nafsi yake si mtu wa kawaida
   
 15. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #15
  Sep 29, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Dkn ni kweli uliyosema,sa ingine hizi fedha tunazotamani ni ujinga,we need a name that will live even after someone is dead,embu tazama m2 anajenga hovyo hovyo daraja au jengo bila kufikiri ipo siku mwanae atatumia na je likitokea la kutokea?anaingza dawa feki kumbe mwanae aliyeko boarding ndo anatumia,au mchele?yaani ni lazima tuamke tuone beyond hizi pua zetu,unajua watoto wetu ipo siku watatutukana au hata kushawishi tufukiwe hai tukiendelea na hizi tamaa za kijinga,sawa jengo litaisha halafu hamna matumizi kweli m2 anaweza kujisifu alikuwa sehemu ya hyo project?
   
 16. HUSSEIN MUSHI

  HUSSEIN MUSHI Member

  #16
  May 16, 2014
  Joined: Feb 16, 2013
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa vile Moshi inaenda kuwa City linaweza kulipa......
   
 17. WENYELE

  WENYELE JF-Expert Member

  #17
  May 16, 2014
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,172
  Likes Received: 757
  Trophy Points: 280
  Fikra ndogo na zenye ghubu na husuda na maendeleo chanya ndo zitaamini kuwa hili jengo litapata hasara!
  Majengo km haya ndo yanaifanya NSSF kua shirika pekee ka umma lenye uwezo wa kuihudumia serikali via mikopo.NSSF imejenga mijengo mirefu Arusha toka mwaka jana mambo ni mazuri tu,kumbukeni Moshi iko sehemu nzuri sana kibiashara kati ya Kenya na mt Kilimanjaro,majengo km haya ndo yanahitajika....Anyway nisije mkasema nawatetea,mi hapa Moshi nimekuja mwaka jana tu.....
   
 18. m

  majeshi 1981 JF-Expert Member

  #18
  May 16, 2014
  Joined: Dec 7, 2013
  Messages: 1,766
  Likes Received: 207
  Trophy Points: 160

  afadhaali mji wetu uwe wa kisasa zaidi
   
 19. o

  ommymbwambo Senior Member

  #19
  May 16, 2014
  Joined: Mar 25, 2014
  Messages: 193
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tena nawasifu nssf cz waliona mbali sana kujenga hili jengo.labda ulitaka wajenge Simiyu?
   
 20. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #20
  May 16, 2014
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,796
  Likes Received: 20,751
  Trophy Points: 280
  kwani mji wa moshi utabaki hivyo hivyo milele?? majengo ni longterm investment baada ya muda litalipa tu
   
Loading...