Jenerali Ulimwengu: Kusema kuwa Mungu amesaidia kupungua kwa Wagonjwa wa Corona ni Dhihaka kwa Mungu na ni Porojo

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,857
7,615
Jenerali Ulimwengu nguli wa masuala mbali mbali ya Kijamii akihojiwa na DW, kipindi kilichorushwa leo saa Saba Mchana amesema kuwa Kusema kuwa Mungu amesaidia tume punguza idadi ya Wagonjwa wa COVID-19 ni Dhihaka kwa Mungu na ni Maneno ya Porojo Porojo.

Akijibu swali aliloulizwa na Mtangazaji wa DW kuwa Tunapaswa tumshukuru Mungu kwa kusaidia Kupunguza Maambukizi ya COVID-19, Ulimwengu amesema, nindhihaka kwa Mungu kufanya hivyo kwa kuwa si kweli kwamba Mungu anaipenda Tanzania pekee na kuichukia Rwanda, Kenya, Italy, Marekani n.k. Aliongeza kuwa Mungu hawezi kuichukia Italy ambako Kuna MAKAO makuu ya Kanisa la Roman Catholic na Kuipenda sana Tanzania na kwamba hilo ni Dhihaka kwa Mungu na ni maneno ya Porojo Porojo.

Akihojiwa kuhusu idadi iliyotajwa na Rais ya wagonjwa wa Corona kuwa ni Mia nne na Ushee huku vifo vikiendelea kubaki 16 na kwamba Mtoto wa Rais kukuta na virusi vya CORONA na baadae kupima na kukuta hana virusi hivyo, Ulimwengu amesema Kuna maswali yanahitaji majibu.

Amesema angependa kupata majibu ya vipimo gani vimetumika kupata idadi hiyo, je ni vipimo vile vile vilivyotiliwa shaka na Serikali vilivyopima mapapai na Mbuzi au Kuna vipimo vipya vinavyoaminika vimeingia nchini...

Maoni yangu: Tuendelee kuwa waangalifu kama alivyotuasa Mhe. RAIS.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe kwa kuwa Roma ndio makao makuu ya kanisa la katoriki basi Mungu lazima awasikilize zaidi hao kabla yenu nyie:- Mzee wa Upako
Gwajima.
Kakobe
KKKT
Anglikana
Sabato
A.I.C

Kazi mnayo mpaka aje awasikilize nyie !!

Sent using Jamii Forums mobile app
Napata mashaka maneno hayo yatakuwa si ya General ninayemfahamu.Kwamba Mungu awasikilize Waroma zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe kwa kuwa Roma ndio makao makuu ya kanisa la katoriki basi Mungu lazima awasikilize zaidi hao kabla yenu nyie:- Mzee wa Upako
Gwajima.
Kakobe
KKKT
Anglikana
Sabato
A.I.C

Kazi mnayo mpaka aje awasikilize nyie !!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulimwengu hajui kuwa Tanzania inapendwa Sana na mungu kuliko italy,kwasababu ya Nyerere..🤗🤗
 
Wachangiaji ambao ni baadhi ya wale vijana ambao mchango wao ulikuwa ndani ya ile 10m pamoja na mzee baba mle ndani na maeneo ya kulizunguka kanisa utawajua tu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nahishi kwa wasi wasi sonona sonona🎵🎵,
Nahishi kwa wasi wasi corona corona🎵🎵
 
Back
Top Bottom