Jenerali Ulimwengu Katika Kumueleza Maalim Seif

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,915
30,259
JENERALI ULIMWENGU KATIKA KUMWELEZA MAALIM SEIF

Konganano la Maalim Seif lilihudhuriwa na watu wengi ambao wanamchango mkubwa katika maendeleo ya fikra Tanzania.

Kuanzia wasomi maarufu kama Emiritus Prof. Issa Shivji hadi viongozi wa dini waliosimamia haki bila hofu kama Sheikh Ponda Issa Ponda.

Walikuwapo watangazaji wa Radio na TV maarufu kama Hamza Kassongo na Charles Hilary.

Na kulikuwa na viongozi wa juu wa Tanzania kama Rais Amani Karume, Joseph Warioba na Joseph Butiku.

Kwa siku mbili ukumbi wa Kongamano la Uzinduzi wa Maalim Seif Foundation ulielemewa na mazito yaliyopita Zanzibar na yote hayo Maalim Seif akiwa katikati yake.

Kuna wakati wasikilizaji walifurahi wakapiga makofi kwa furaha na wakati mwingine ukumbi mzima ulijiinamia kwa kuona aibu na kuingia simanzi kuwa tumefikaje katika hali hiyo ya kufedheheka kama taifa.

Hapo wanajiuliza ingekuwaje kama Maalim asingetumia busara.

Tungejikuta na vifo vya watoto na wanawake maiti zimelaliana nje ya Hoteli ya Bwawani.
Jenerali.

Nilikuwa na Jenerali meza moja tukila chakula cha mchana.

Nikamwambia kuwa nimejaribu sana kuiga staili yake ya uandishi hasa lugha yake ya Kiingereza bila mafanikio na nimekata tamaa kwa ajili umri wangu umesonga mbele tabu kujifunza.

"Mohamed wewe ni wa kuniambia mimi maneno hayo?"

Kwa hakika niliyasema maneno yale kumuambia Jenerali kwa dhati ya nafsi yangu.
Jenerali akacheka akaniambia, "Basi bakia hivyo hivyo."

Huenda Jenerali hajui lakini yeye amekuwa na mchango mkubwa sana kwangu katika safari yangu ya uandishi.

Jenerali hakupata hata siku moja kuacha kuchapa makala zangu katika magazeti yake yote aliyoanzisha na kumiliki.

Kwa wanaonifahamu hasa katika miaka yangu ya mwanzo ya uandishi watakumbuka makala zile.

Makala ambazo wahariri wengine wasingethubitu kuzigusa.
Jenerali hakuwa na shida na kalamu yangu.

Jenerali alipokaribishwa kuzungumza akarekebisha kauli iliyomtambulisha kama mwanasiasa.

Jenerali akasema kuwa mwanasiasa ni yule anaefanya siasa kuwa ajira.

Jenerali akasema kuwa yeye anashughulika na siasa lakini si kama ajira bali anafanya na kazi nyingine.

Jenerali akaanza kueleza hali ya siasa ilivyokuwa Tanzania si muda mrefu uliopita.
Jenerali hakubabaisha wala kubabaika.

Kisha akaingia katika uchaguzi.

Hakufika mbali ssana sauti ya Mzee Warioba tukaisikia sote ikiingia kati kwa upole na unyenyekevu mkubwa ikisema kuwa si lazima Jenerali aseme yote.

Nina hakika ni kuwa aliyetafadhalisha alikuwa Mzee Warioba laiti kama kauli ile ingetoka kwa mwingine...

Huyu ndiye Jenerali.
Kuna kitu cha miaka hii ya karibuni kinaitwa "Streisand Effect."

Barbra Streisand alikuwa mwanamama mcheza senema na pia muimbaji na mimi nikipenda muziki wake katika miaka ya 1980.

Barbra alikwenda mahakamani ili mahakama iwazuie watu fulani kuweka nyumba yake hadhir kwa kila mtu ajue ilipo.

Barbra Streisand kafanya vile baada ya hawa jamaa kukaidi.

Kesi ilipokwenda mahakamani ikawa ndiyo kiama cha Streisand kwani jambo lenyewe sasa likawa bayana kila mtu analisoma kwenye magazeti na kuangalia kwenye TV; na kujua hiyo nyumba ilipo ilhali yeye alitaka nyumba yake iwe na stara.

Hii ndiyo Streisand Effect.
Mahakama hazina faragha.

Alilotaka Streisand liwe faragha mahakama likalimwaga uwanjani.
Nimesoma kuwa Jenerali kapewa onyo kali na Spika wa Bunge akimtuhumu kushambulia Bunge.

ya onyo hilo ghafla jambo limegeuka kuwa burudani ya aina yake.

Kichekesho.

Nadhani katika hivi vichekesho kuna jambo la kujifunza hasa ukigeuza shingo nyuma kuangalia yaliyomfika Barbra Streisand.

Barbra Streisand kataka kadha kapata kadha wa kadha.

Screenshot_20211112-223713_Facebook.jpg
 
View attachment 2008346
Seen
 
Mweusi...
Nimelisema jambo lenyewe mbona?
Basi nadhani Mimi nilikuelewa kuwa Jenerali iwe kwa uandishi wake au kauli yake huwa hakwepeshi au amung'unyi maneno anatoa kile anachokisikia moyoni mwake, ndio maana hata wewe Mzee Mohamed ulikua uanatamani uandishi wake pia kama nimekuelewa na wewe makala zako zilizokua zinapitia kwenye mikono ya Jenerali alizipitisha bila woga ukizingatia waandishi/wahariri wengi wanaogopa makala zitakazowaletea shida na serikali au zenye ukweli Sana. Pia tunaona katika kumuelezea hayati Maalim Seif anazungumzia siasa za Tanzania bila kubabaika kuhusu ujasiliamali wa kisiasa. Jenerali "akasema kuwa mwanasiasa ni yule asiyefanya siasa kuwa ajira." Na alipoanza kuzungumzia kuhusu uchaguzi Mzee Warioba akamkatisha, hapo tunaona Mzee Warioba alijua kitakachotokea Jenerali angemwaga kila kitu ndio maana kwenye kumalizia umegusia "Streisand Effect." Ambapo kile alichojaribu kukizuia Mzee Warioba ndicho kinachojadiliwa. Tuko pamoja Mzee Mohamed Saidi kwa makala zako tunapata historia na chakula cha akili
 
Streisand's effect hahahaa Shkamoo Mzee....huu uandishi wako Naupenda sana japo nauchukia maana pale simulizi inaponoga ndio unakuta imeisha ghafla. Hongera sana Mzee

View attachment 2008389

KAMA ANAYO PICHA NA ATAKUPA UISAMBAZE ITAKUWA ILE ALIYOPIGA AMEVAA NGUO ZA KIJANI AKIJINASIBU KAMA COMMANDER WA VIJANA WA CCM!!! WAKATI HUO ANAZENGEA UBUNGE WA KONGWA!!!
 
Basi nadhani Mimi nilikuelewa kuwa Jenerali iwe kwa uandishi wake au kauli yake huwa hakwepeshi au amung'unyi maneno anatoa kile anachokisikia moyoni mwake, ndio maana hata wewe Mzee Mohamed ulikua uanatamani uandishi wake pia kama nimekuelewa na wewe makala zako zilizokua zinapitia kwenye mikono ya Jenerali alizipitisha bila woga ukizingatia waandishi/wahariri wengi wanaogopa makala zitakazowaletea shida na serikali au zenye ukweli Sana. Pia tunaona katika kumuelezea hayati Maalim Seif anazungumzia siasa za Tanzania bila kubabaika kuhusu ujasiliamali wa kisiasa. Jenerali "akasema kuwa mwanasiasa ni yule asiyefanya siasa kuwa ajira." Na alipoanza kuzungumzia kuhusu uchaguzi Mzee Warioba akamkatisha, hapo tunaona Mzee Warioba alijua kitakachotokea Jenerali angemwaga kila kitu ndio maana kwenye kumalizia umegusia "Streisand Effect." Ambapo kile alichojaribu kukizuia Mzee Warioba ndicho kinachojadiliwa. Tuko pamoja Mzee Mohamed Saidi kwa makala zako tunapata historia na chakula cha akili
Mweusi...
Nimemkusudia Spika kwa kumuonya Jenerali.

Matokeo yake sasa lile alilokuwa amefanya Jenerali peke yake kwa kummuonya kawakaribisha wapenzi wa Jenerali kwenye mtanange.

Mashambulizi yameongezeka.
Hii ndiyo Streissand Effect.
 
Nimekupata sana
 
Back
Top Bottom