Malaria Sugu
JF-Expert Member
- Jul 7, 2009
- 2,653
- 270
Sina imani naye hata kidogo tokea gazeti lake la Rai kwenye kampeni ya 2005 limchafue Salim na kumpamba JK na wengi walioshiriki walibarikiwa kupewa vyeo!! sio bure na siku hizi gazeti lake hili Raia limebadilika siyo lile la mwanzoni yetu macho!!!
Ila jenerali ni mzalendo wa kweli, embu jaribuni kuzisoma kwa utulivu na umakini sana makala zake,jamaa huwa anachambua mada kwa ufasaha sana, kwa kweli ni zenye umuhimu sana kama viongozi wetu wataamua kuzifuatialia nakuzifanyia kazi
Mkapa ile kampeni timu yake ya 1995 wale wengi wa karibu aliwatema live na hapo ndo bifuu kuubwaaa mkapa alilopata toka kwa hao akina jenerali na wenzie.Kuchambua mada kwa ufasaha sana ni kipaji na si uzalendo. Usinielewe vibaya sina maana kwamba Jenerali si mzalendo kwa sababu hatujawahi kusikia sababu yoyote ya kufanya tumshuku kwamba si mzalendo zaidi ya kuvuliwa uraia wake. Ndio maana tungependa kujua sababu iliyosababisha avuliwe uraia - je ni kweli alikuwa si raia au walikosana na swahiba wake? Je Mkapa hakugundua hilo wakati anamtumia kwenye Kamati yake ya watu wa karibu naye ya Kampeni za kugombea Urais mwaka 1995?
Mie ni msomaji mzuri wa makala zake na za wengine kwenye magazeti mbalimbali. Ninachoweza kusema kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba anaandika ili aonekane kwamba yuko juu ya waandishi wengine zaidi ya kuandika kuonyesha 'uzalendo wa kweli'.
nadhani kachukua msimamo wa kati,anauma na kupiliza.Makala zake ni nzuri sana ila ni kwa watu wa daraja fulani ama sivyo utafungia maandazi gazeti,Hutoi kitu!!!
Mimi nadhani kuna mambo mawiri; maisha na ukweli sasa kama ukweli unakuharibia maisha unajaribu kuukimbiya. Lakini kama unawapamba mafisadi mimi naona ni bora kukaa kimya kama unahofu maisha yako, kuliko kuwatukuza.