Jenerali Ulimwengu anamtumikia nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jenerali Ulimwengu anamtumikia nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Malaria Sugu, Jul 22, 2009.

 1. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #1
  Jul 22, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Je, kweli Jenerali Ulimwengu anawatumikia watanzania kama vile alivyokuwa Habari Corparation, Chanel na sasa yupo gazeti la Raia Mwema, au tuseme sasa anamtumikia mwanasiasa mmoja aliekuwa maarufu?

  Nasena hivyo hasa baada ya miaka ile alikuwa ni mmoja ya waandishi waliokuwa wanafichua maouvu mpaka kufikwa kufukuzwa nchini lkn sasa tunamuona amegeuka kabisa, anawapamba mafisadi
   
 2. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #2
  Jul 22, 2009
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Kivipi?
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mzee wa Hoja kaishiwa hoja hapa! Ni mafisadi gani anaowapamba? Tunachojua ni kwamba ile Habari Corp ialiyokuwa akiimiliki sasa ndiyo imekuwa inawapamba mafisadi.
   
 4. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mie ningependa kujua Jenerali walikosana nini na swahiba wake Benjamin William Mkapa hadi kufikia kupokwa uraia? Labda lilishajadiliwa humu, ntafurahi mtu akinielekeza wapi ili niweze kutegua kitendawili hiki!

  Makala za Jenerali kwa kweli hunipa shida kuzielewa zina lengo gani.
   
 5. Prince Alberto

  Prince Alberto Member

  #5
  Jul 22, 2009
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ila jenerali ni mzalendo wa kweli, embu jaribuni kuzisoma kwa utulivu na umakini sana makala zake,jamaa huwa anachambua mada kwa ufasaha sana, kwa kweli ni zenye umuhimu sana kama viongozi wetu wataamua kuzifuatialia nakuzifanyia kazi
   
 6. K

  K4jolly JF-Expert Member

  #6
  Jul 22, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sina imani naye hata kidogo tokea gazeti lake la Rai kwenye kampeni ya 2005 limchafue Salim na kumpamba JK na wengi walioshiriki walibarikiwa kupewa vyeo!! sio bure na siku hizi gazeti lake hili Raia limebadilika siyo lile la mwanzoni yetu macho!!!
   
 7. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #7
  Jul 22, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Nakubaliana nawe kwa sehemu kubwa. Dhambi ya kumbagua Salim kama ilifanywa na Jenerali anastahili kulaumiwa (kulaaniwa kama asemavyo Seleli). Lakini nakumbuka kilichofanywa na Rai wakati ule ni kumbeba JK. Aliyefanya hivyo ni Salva na wote tumeona. Sasa hivi salva na Jenerali hawaivi.

  Dhambi ya kumbagua Salim ingali inaitafuna serikali ya JK. Patachimbika mpaka watubu hiyo dhambi.

  Sasa kuhusu Raia Mwema kubadilika, naomba kutofautiana kidogo. Hili ni gazeti ambalo mpaka sasa limebaki bila harufu ya itikadi wala kutumwa na mwanasiasa yeyote. Aliye na data tofauti na msimamo huu, amwage tuone.
   
 8. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #8
  Jul 22, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuchambua mada kwa ufasaha sana ni kipaji na si uzalendo. Usinielewe vibaya sina maana kwamba Jenerali si mzalendo kwa sababu hatujawahi kusikia sababu yoyote ya kufanya tumshuku kwamba si mzalendo zaidi ya kuvuliwa uraia wake. Ndio maana tungependa kujua sababu iliyosababisha avuliwe uraia - je ni kweli alikuwa si raia au walikosana na swahiba wake? Je Mkapa hakugundua hilo wakati anamtumia kwenye Kamati yake ya watu wa karibu naye ya Kampeni za kugombea Urais mwaka 1995?

  Mie ni msomaji mzuri wa makala zake na za wengine kwenye magazeti mbalimbali. Ninachoweza kusema kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba anaandika ili aonekane kwamba yuko juu ya waandishi wengine zaidi ya kuandika kuonyesha 'uzalendo wa kweli'.
   
 9. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kitila ameuliza swali, "kivipi?" hajajibiwa watu wanaanza kujadili hewa. Wanajadili mambo mengine kabisa na mtoa hoja kapotea. Nadhani hapa si mahala pake na mada iliyowasilishwa hapa na MzeeWaHoja haina mashiko kwa sababu nilitarajia ataweka angalao "Rai ya Jenerali" ya wiki hii ama ya wiki iliyopita akaichambua, ama akaja na story ama makala ya gazeti la Raia Mwema, inayolinda mafisadi angeeleweka.

  Mimi nadhani kachanganya kati ya Rai na Raia Mwema na kama hivyo ndivyo, sioni sababu ya kuendelea na hii thread tukapoteza muda
   
 10. Shabobabo

  Shabobabo JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2009
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mimi nadhani kuna mambo mawiri; maisha na ukweli sasa kama ukweli unakuharibia maisha unajaribu kuukimbiya. Lakini kama unawapamba mafisadi mimi naona ni bora kukaa kimya kama unahofu maisha yako, kuliko kuwatukuza.
   
 11. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #11
  Jul 22, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
 12. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Haina maana watu kutumia umeme na pesa za Internet kujadili hewa .

  kama mtu anatoa hoja na anashindwa kuweka ushahidi ama hata chembe zenye mahusiano na ka ukweli haina maana kujadiliana ,kwani hakuna cha kujadiliana hapo.
   
 13. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Anawatumikia watanzania -kama alihitaji jibu la swali tuu.
   
 14. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  lete ushahidi wa jenerali kuwapamba mafisadi.
   
 15. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #15
  Jul 22, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkapa ile kampeni timu yake ya 1995 wale wengi wa karibu aliwatema live na hapo ndo bifuu kuubwaaa mkapa alilopata toka kwa hao akina jenerali na wenzie.

  kwa hiyoo jenerali hakutegemea kabisa kutoswa kivile mpaka akaanzisha makala kali za kuukosoaa sana utawala wa BWM...

  JK kuingia mwanzoni akaanza kumpamba, nanukuu ''Kwa mara ya kwanza tumepata kiongozi anayekemea rushwa kwa uwazi kabisaa''. (maneno ya jenerali hayo kwa Jk)

  Gafla akagundua jamaa walaa sio kama anavyofikiriii....hapo alitambua nguvu za akina RA dhidi ya mkuluu na mtandao kwa ujumla ambao Jenerali hawakumwihitajiii...

  yeye, salva, shoo wakaparaganyika na RA kiulainiii akainunua HCL na kuiweka chini yake huku salva akielekea ikulu, shoo mtaani lakini akipata chapuo za kazi toka kwa RA kupitia salva...

  Jenerali kwa sasa anasoma ramani upya atokee vp ila yupoo makinii asikanyage miiba mapemaaa..kile kibano cha uraia hatasahauu..
  HABARI NDO HIYOOOOOOO..
   
 16. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #16
  Jul 22, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
 17. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #17
  Jul 23, 2009
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  nadhani kachukua msimamo wa kati,anauma na kupiliza.Makala zake ni nzuri sana ila ni kwa watu wa daraja fulani ama sivyo utafungia maandazi gazeti,Hutoi kitu!!!
   
 18. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #18
  Jul 23, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Nimeipenda sentensi yako. Hebu ifafanue vizuri niipende zaidi!:)
   
 19. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #19
  Jul 23, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  mafisadi ni kina nani??
   
 20. K

  Kalimanzira Senior Member

  #20
  Jul 23, 2009
  Joined: Aug 15, 2007
  Messages: 100
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Binafsi sidhani kama unahakika na hili unaloongea. Jenerali ni miongoni mwa wanataaluma wachache sana katika nchi yetu mwenye uwezo mpana sana wa kujadili mada, kwa ufasaha na uelewa wa kiwango cha juu. Rejea makala zake nyingi tu! Lakini pia kazi hii ya "ukombozi wa fikra" za watu inahitaji mwitikio. Jenerali amekuwa mwiba mkubwa sana wa watawala katika kuamsha uelewa na udadisi wa wananchi katika mambo mengi sana. Na kwa kiasi kikubwa ndio ilikuwa chanzo cha kuambiwa "si raia". Hivyo ni vema wakati wa kumjadili mtu kama ulimengu walau uwe na vielezo vya kiyakinifu.
   
Loading...