Jenerali Mabeyo(JWTZ): Kuna Viashiria vinavyotishia Usalama wa Nchi. Hatua zinachukuliwa kudhibiti hali hiyo

Mbona ulimboka alitolewa kucha kipind cha jk,mwembechai,mto ruvu watu waliokotwa ktk viroba tawala zilizopita,ni uhalifu kama uhalifu mwingine,sema awamu hii ngosha kashika pabaya, ukiwa poacher anakudaka,ukibeba sembe anakudaka,ukipindisha check unae,ukirob mahali unae,wewe na familia yako mlozoea hayo mambo lazima uumie tu,sisi wajinga tusiosona huku kusini na tunakomjazia kura tunamwona wa maana,nyie wapigaji jasho lazima liwatoke,na bado.
Hata kumbukumbu huna Ruvu Magu huyu huyu. Ccm ni wale wale. Fisadi zaidi yake ni nani anajizolea mihela bila kujali bunge lilipanga nini vikao vyote ni hasara tupu yeye ndio yeye. Anamshitaki Tido matumizi mabaya ya madaraka yeye hizo za bombadia kaizinisha nani?
 
Hata kumbukumbu huna Ruvu Magu huyu huyu. Ccm ni wale wale. Fisadi zaidi yake ni nani anajizolea mihela bila kujali bunge lilipanga nini vikao vyote ni hasara tupu yeye ndio yeye. Anamshitaki Tido matumizi mabaya ya madaraka yeye hizo za bombadia kaizinisha nani?
We ulikalia moto wacha ukuunguze,mtasimulia tu kwa utawala huu,hizo kelele ni kama maumiv ya ma-vi tu wakati wa ku-nya,unalia peke yako ukimaliza unachamba unatoka,h uyo magu ana backup kubwa kuliko wewe mwenye id zaidi ya kumi unaemfungulia uzi wa kumtusi kila dakika,na ni yeye aliyekuachia huu uhuru wa kumtusi na kumkejeli,hivi mwadhani kuwa raisi ni rahisi kama kuwa CEO wa kampuni?
 
Kumbe inawezekana akaalikwa kwenye hafla na kutoa hotuba ya Namna hii? Watangulizi wake sikuwahi kuwasikia wakisema sema ndo maana kwangu nimeona jambo geni.

Hongera kwa kuona viashiria vya uvunjifu Wa Amani na kuanza kuchukua hatua. Kikubwa ni ushirikiano na hali ya uzalendo Kwa kila mtu ni muhimu sana.
 
Inafaa akumbuke sisi ndiyo waajili tunaweza mletea noss yeyote inabidi amtii to hata akiwa lipumba sawa.yeye asmpambe sizonje.yeye aongolee alivuo imarisha vikosi kwa ajili ya kutulinda.tukiamua sizonje hafai ila Dovutwa sawa
 
nashangaa sana hii serikali ya ccm. hii amani mnayoizungumzia ni ipi? juzi hapa mtu anapigwa mapanga na kufa wengine wanapotea tu hawajulikani mnasema kuna amani? tusidanganyane kwa sasa amani hakuna

Nakumbuka ile kauli ya "Mzee Mapesa" wakati huo akiwa mpinzani aliwahi kusema "Tanzania hakuna amani, kilichopo ni uvumilivu." Hapo kwenye "uvumilivu" nafikiri angeweza pia sema kilichopo ni "uoga." Na sasa hivi ndio tuna tishwa kwelikweli ili tuendelee kuogopa kudai haki zetu, kubwa kati ya hizo haki ni kuishi kwa amani (ya kweli) ndani ya nchi yetu wenyewe....
 
Nakumbuka ile kauli ya "Mzee Mapesa" wakati huo akiwa mpinzani aliwahi kusema "Tanzania hakuna amani, kilichopo ni uvumilivu." Hapo kwenye "uvumilivu" nafikiri angeweza pia sema kilichopo ni "uoga." Na sasa hivi ndio tuna tishwa kwelikweli ili tuendelee kuogopa kudai haki zetu, kubwa kati ya hizo haki ni kuishi kwa amani (ya kweli) ndani ya nchi yetu wenyewe....
ukimuuliza sasa hivi atayakanusha vibaya mno
 
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (JWTZ), Jenerali Venance Mabeyo amewataka Watanzania kujiepusha na vitendo vinavyoweza kutishia usalama wa nchi na kuharibu tunu ya amani iliyopo.

Ameeleza kuwa hivi sasa vipo viashiria vinavyotishia usalama wa nchi, na kwamba hatua zinachukuliwa ili kudhibiti hali hiyo.

Jenerali Mabeyo amewaomba Watanzania kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli dhidi ya wizi, ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi za umma, kwa kuwataja hadharani watu wanaojihusisha na vitendo hivyo.

Ametoa kauli hiyo jana wakati akifunga Maadhimisho ya Tamasha la Mashujaa wa Vita ya Majimaji katika Viwanja vya Makumbusho ya Mashujaa wa Vita ya Majimaji mjini Songea.

Mabeyo amesema vita dhidi ya wizi na ufisadi, iliyoanzishwa na Rais Magufuli, si ya mtu mmoja, bali kila Mtanzania anapaswa kushiriki, kwani mali zinazoibwa na baadhi ya Watanzania, zinapaswa kuwanufaisha watu wote.

Mabeyo alisema badala ya kushughulika na uvunjifu wa amani, ipo haja ya Watanzania kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano, ambayo imedhamiria kuwatumikia wananchi kwa kuboresha huduma za kijamii ili kutoa fursa kwa wananchi kutumia muda wao kufanya kazi za kujiletea maendeleo.

Ametaja baadhi ya mambo yanayotishia usalama wa nchi kuwa ni matumizi mabaya ya utandawazi ambayo mbali na ya kuharibu utamaduni wa nchi, baadhi ya watu wanaitumia vibaya kwa kuhamasisha wananchi kufanya na kushiriki katika matukio ambayo yanaashiria uvunjifu wa amani na utulivu uliopo nchini kwa muda mrefu.

Jenerali Mabeyo alitaka shule za msingi, sekondari na vyuo nchini, kufundisha wanafunzi umuhimu wa kulinda, kutunza amani na wananchi kuishi kwa kupendana, badala ya kutumia muda wao kutafuta sababu za kutengana, jambo ambalo halina tija kwa taifa.

Wakati huo huo, Jenerali Mabeyo aliitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuboresha Makumbusho ya Mashujaa wa Vita ya Majimaji ili yatumike kwa ajili ya utalii na kuliingizia taifa fedha nyingi.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Chiristina Mndeme alisema Serikali ya Mkoa wa Ruvuma, itaongeza nguvu katika kulinda mipaka yake ili wananchi wa mkoa huo waweze kuendelea na kazi za uzalishaji mali.


HIVI HUYU MKUU WA MAJESHI HAJAWAHI KUSIKIA KUNA WATU WASIOJULIKANA ? PIA HAJAWAHI ONA DEMOCRACY IKICHEZEWA KWA MAKUSUDI LEO IMEFIKIA HATA CHAGUZI NDOGO WATU KUULIWA NA KUTIWA VILEMA ? JESHI LA POLISI LIMESAHAU MAJUKUMU YAO LIMEKUA TAWI LA CCM ? AKILI HANA BASI HATA PICHA HAONI ?
 
Nilikuwa namheshimu sana huyu kaka kwa hekima zake ila sasa kama ameingia kwenye siasa za maji taka za kuua na kutupa watu kwenye bahari, kupiga risasi watu na kuwazuia kwenda hospitalini, kupoteza watu na bado anaisifia serikali badala ya kukaa kimya hapo naanza kuwa na wasi wasi. Mwanajeshi hana chama wala itikadi. Enzi za kulazimishwa kuwa TANU/CCM tukiwa JKT zilishapita.
 
Back
Top Bottom