Jela miaka 40 kusafirisha dawa za kulevya

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Mtwara imewahukumu watu wawili kati ya watatu kifungo cha miaka 40 jela na kulipa faini ya Sh. 1,517,853,318 baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya.

jela (1).jpg


Hukumu iliyotolewa na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam aliyeteuliwa kusikiliza kesi hiyo, Jaji Issaya Halfani, baada ya kuridhishwa pasio shaka na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri.

Waliohukumiwa ni Ahmadi Nyamvi na Athumani Mohamedi wakazi wa Wilaya ya Kindondoni mkoani Dar es Salaam, huku ikimwachia huru mshtakiwa wa tatu, Monicar Mathias Murumba, baada ya kutoonekana na hatia.

Baada ya kutiwa hatiani, wakili aliyekuwa anawatetea, Hadson Ndusiao, aliiomba mahakama kuwapa wateja wake adhabu nafuu kwa alichodai ni wakosaji wa mara ya kwanza, pia wamekaa mahabusu kwa muda mrefu, hivyo wanajutia makosa waliyoyafanya na watakuwa raia wema warudipo uraiani.

Jaji Halfani akitoa hukumu katika kesi hiyo namba 04/2012, alisema kosa la kwanza la kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin aliwahukumu kila mmoja kifungo cha miaka 20 jela pamoja na kulipa faini ya Sh. 1,490,780,580.

Kosa la pili la kusafirisha dawa ya kulevya aina ya cocane aliwahukumu kutumikia kifungo kama hicho jela na kulipa faini ya Sh. 13,535,869 kila mmoja na kufanya ya faini ya Sh. 1,517,853,318.

Jaji Halfani alisema adhabu zote zinakwenda kwa pamoja, hivyo watalazimika kutumikia kifungo cha miaka 20 jela kila mmoja, huku ikimwachia huru mshtakiwa wa tatu Monica Mathias Mulumba.

Awali ilidaiwa na Mwanasheria wa Serikali, Godfey Mramba, kuwa washtakiwa walikamatwa Januari 11, 2012 katika Kijiji cha Mchinga, Wilaya na Mkoa wa Lindi, wakiwa wanasafirisha dawa hizo zikiwa kwenye madumu na thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 9.

NIPASHE
 
Duh! Hukumu inatolewa zaidi ya miaka 9 baada ya kukamatwa! Kesi ilikwama wapi? Kwa wajuzi wa sheria, ina maana hiyo miaka 20 kila mmoja, inajumuisha na miaka waliokaa mahabusu? Kwa maana ya kwamba kila mmoja amebakiza miaka 11 kutoka sasa ya kutumikia kifungo? Au miaka inaanza upya?
 
Aisee Miaka 9 mingi Sana halaf kifungo anaenza kuanza Moja tena Sio fair kabsa
 
yote HAYA siyo sawa kukaa muda wote huo, SIO HAKI. Humo kunanukia Rushwa, uzembe, ubambikaji kesi, kutojali mahangaiko ya wengine. Ona Huyo aliyethibitishwa Hana hatia, baada ya miaka 9
Halafu Mla Mali za umma na muhujumu inchi yupo uraiani.

Inchi ngumu sn hii.
 
Duh! Hukumu inatolewa zaidi ya miaka 9 baada ya kukamatwa! Kesi ilikwama wapi? Kwa wajuzi wa sheria, ina maana hiyo miaka 20 kila mmoja, inajumuisha na miaka waliokaa mahabusu? Kwa maana ya kwamba kila mmoja amebakiza miaka 11 kutoka sasa ya kutumikia kifungo? Au miaka inaanza upya?
Kwa Tanzania inaanzia upya kabisa.

Tena nahisi kuna harufu ya rushwa kwenye suala Hilo.

Haiwezekani wanaokamatwa na grams 250 wafungwe maisha.

Na waliomamatwa na kilo zaidi ya 100 wapigwe miaka hiyo.

RIP MAGUFULI...

Africa hakuna haki...
 
Kwa Tanzania inaanzia upya kabisa.

Tena nahisi kuna harufu ya rushwa kwenye suala Hilo.

Haiwezekani wanaokamatwa na grams 250 wafungwe maisha.

Na waliomamatwa na kilo zaidi ya 100 wapigwe miaka hiyo.

RIP MAGUFULI...

Africa hakuna haki...
Sasa kumfunga mtu unadhani kunasaidia? Dawa ni wanyongwe tu
 
Bilioni tisa siyo kitu kidogo wakuu,
hata mimi najitosa kwakweli kuisafirisha.
Yani billion 9 mwenyewe unaiona nyingiiiiiii. Kweli tumetofautiana na kanun ya maisha wote hatuwez kuwa sawa.
 
Mahabusu miaka tisa!! Mingi sana au ndio ile utasikia upelelezi haujakamilika
 
Yani billion 9 mwenyewe unaiona nyingiiiiiii. Kweli tumetofautiana na kanun ya maisha wote hatuwez kuwa sawa.
Acha zako basi, hujui bililion tisa ni bajeti ya nchi?

Uanze kuhesabu billion 1,
Bill 2,
Bill 3,
Bill 4,
Bill 5,
Bill 6,
Bill 7,
Bill 8,
Mpaka billion 9.

Acha kabisa mkuu.
Hapo ukisema uzipange milioni mia mia mpaka zifike bilioni tisa si mpaka utazeeka.
 
Nipeni mchongo wa haya mambo jamani. Anyone interested. Am ready kufanya shughuli kati ya tz na Kenya.
Mimi kwa hapa ndani ya Tanzania naweza nikafanya vizuri sana!
sema tu ndiyo hivyo kupata sehemu ya kuanzia ni ngumu!
 
Wengine maisha wenye mzigo mdogo, wenye mzigo mkubwa miaka 40 kazi kweli kweli.
 
Mwaka 2012 nilikutana na dogo flani nilimuacha shule kitambo tulikumbukana sababu nilisoma darasa moja na kakayake, dogo alikua vizuri na alinichana live anauza ‘poda’, “bro kama unaweza nikupe mchongo” nikamuambia nipe namba nitakuchek, akaniambia namba sikupi ila siku nyingine nitakuja tuongee. Sikumuona tena, najua atakua ameshanasa.
 
Back
Top Bottom