Jela Miaka 30 kwa wizi wa Sh 10,000 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jela Miaka 30 kwa wizi wa Sh 10,000

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Maverick, Jul 10, 2008.

 1. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2008
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Maoni: Watalamu washeria tusaidieni kama adhabu ni stahili kwa kukosa lililotendwa au ndio ya mnyonge na maskini?

  MFUNGWA Yahaya Shariff aliyekuwa akitumikia kifungo cha miaka 15 jela kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha juzi, aliongezewa adhabu hiyo na kufikia miaka 30 jela baada ya kukata rufaa akipinga adhabu ya awali.

  Yahaya aliongezewa adhabu hiyo baada ya kupinga kifungo cha miaka 15 katika Mahakama ya Rufaa kwa kile alichokieleza kutotendewa haki na Mahakama Kuu Kanda ya Tanga na ile ya wilaya, iliyomhukumu kifungo hicho.

  Mahakama hiyo ikiongozwa na majaji watatu, walifikia wa kumuongezea adhabu mrufani kwa maelezo kuwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha alilotiwa nalo hatiani, adhabu yake ni miaka 30 badala ya 15 anayoitumikia sasa.

  Katika uamuzi wa kesi hiyo, majaji hao walieleza kuwa adhabu ya kifungo cha miaka 15 alichopewa na Mahakama Kuu, haikuwa halali kwa kuwa kosa hilo linaangukia katika kifungu cha adhabu ya chini ya kifungo cha miaka 30.

  Mrufani huyo akiwa na mwenzake, Hamad Hassani, walitiwa hatiani mwaka jana na Mahakama ya Wilaya ya Korogwe kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha na kuhukumiwa kifungo cha miaka 15 jela.

  Hata hivyo, baada ya kutiwa hatiani, Sharrif na mwenzake walikata rufaa katika Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, kupinga adhabu hiyo ambapo Hamad alishinda na kuachiwa huru, lakini Yahaya alitakiwa kuendelea na kifungo chake, jambo ambalo alilipinga na kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa.

  Awali ilidaiwa katika mahakama hiyo ya Wilaya ya Korogwe kuwa, mrufani na mwenzake Hamad walimpora, Florence Kalaghe sh 10,000, baada ya kumtishia kwa silaha.

  Tanzania Daima
   
 2. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2008
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Maverick,
  Hii taarifa ina maneno "unyang’anyi" na "walimpora". Wewe kwenye title yako umeamua kutumia neno wizi.


  Wewe unaonaje ndugu?  .
   
 3. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #3
  Jul 10, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mimi si mwanasheria kitaaluma lakini najua wizi unao involve silaha, adhabu aliyopewa ni size yake. Masikini alidhani ata serve kwa kupunguziwa 15 kumbe kadungwa zaidi 15. Wacha aendelee kunyea pipa huko magereza. Asubiri na mafisadi wakina C***** na L***** na R***** wanakuja kumjoin very soon.
   
 4. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ningekuwa ni mimi ndiye Mh Hakimu ningempa na viboko 12. 6 anapoanza kutumikia na 6 atakapomaliza ili akamuonyeshe mke wake. Serious I am not joking
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Duh pole sana mfungwa....kumbe alifanya unyang'anyi kwa kutumia siraha.
  Usiangalie thamani ya kitu alicho nyang'anya hata angenyang'anya 500 angepigwa mvua hizo hizo 30.Lakini angeiba kwa kuhamisha adhabu ya mvua 30 haikuwa sahihi angepewa ya kufyeka nyasi au kusafisha vyoo au adhabu nyingine ndogo ndogo kwani mtu kaiba 10,000/= ukimfunga miezi 6 serikali ndo inaingia hasara kumlisha kwa hiyo anapewa adhabu ndogo ndogo.
  Huyu hii adhabu alistahili kwa vile alifanya unyang'anyi kwa kutumia siraha.
   
 6. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Absolutely!
  Hili ni kosa lenye kiwango cha chini cha adhabu ya miaka 30 jela( starting) na kwenda juu!!
  Wizi ( theft) na robbery ( unyang'anyi) ni makosa mawili tofauti....na wa kutumia silaha tena ndo kabisaaaaa..balaa kubwa maana lazima uanze na mvua 30 kwa kwenda mbele!
   
 7. NaimaOmari

  NaimaOmari JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 807
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  hukumu ingekuwa hivi na majaji wote wa tanzania basi nchi yetu ingekuwa swaaaafi ... naona huyu hajatoa rushwa ... majambazi wakubwa wakubwa wanaua na wanakula na mahakimu na wanawalk free ... ameingia mtegoni kama zombe wacha anyee debe
   
Loading...