Maverick
JF-Expert Member
- May 29, 2008
- 308
- 11
Maoni: Watalamu washeria tusaidieni kama adhabu ni stahili kwa kukosa lililotendwa au ndio ya mnyonge na maskini?
MFUNGWA Yahaya Shariff aliyekuwa akitumikia kifungo cha miaka 15 jela kwa kosa la unyanganyi wa kutumia silaha juzi, aliongezewa adhabu hiyo na kufikia miaka 30 jela baada ya kukata rufaa akipinga adhabu ya awali.
Yahaya aliongezewa adhabu hiyo baada ya kupinga kifungo cha miaka 15 katika Mahakama ya Rufaa kwa kile alichokieleza kutotendewa haki na Mahakama Kuu Kanda ya Tanga na ile ya wilaya, iliyomhukumu kifungo hicho.
Mahakama hiyo ikiongozwa na majaji watatu, walifikia wa kumuongezea adhabu mrufani kwa maelezo kuwa kosa la unyanganyi wa kutumia silaha alilotiwa nalo hatiani, adhabu yake ni miaka 30 badala ya 15 anayoitumikia sasa.
Katika uamuzi wa kesi hiyo, majaji hao walieleza kuwa adhabu ya kifungo cha miaka 15 alichopewa na Mahakama Kuu, haikuwa halali kwa kuwa kosa hilo linaangukia katika kifungu cha adhabu ya chini ya kifungo cha miaka 30.
Mrufani huyo akiwa na mwenzake, Hamad Hassani, walitiwa hatiani mwaka jana na Mahakama ya Wilaya ya Korogwe kwa kosa la unyanganyi wa kutumia silaha na kuhukumiwa kifungo cha miaka 15 jela.
Hata hivyo, baada ya kutiwa hatiani, Sharrif na mwenzake walikata rufaa katika Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, kupinga adhabu hiyo ambapo Hamad alishinda na kuachiwa huru, lakini Yahaya alitakiwa kuendelea na kifungo chake, jambo ambalo alilipinga na kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa.
Awali ilidaiwa katika mahakama hiyo ya Wilaya ya Korogwe kuwa, mrufani na mwenzake Hamad walimpora, Florence Kalaghe sh 10,000, baada ya kumtishia kwa silaha.
Tanzania Daima