Jee mshtakiwa no X alikuwa nani katika kesi ya uhaini ya Karume?

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
[h=1][/h]Written by amini // 21/12/2011 // Habari // No comments

Karume_Poster_c19xx-564x272.jpg
Hakuna shaka kuwa mshtakiwa no X katika kesi ya mauwaji ya Karume alikuwa ni Juliasi Nyerere lakini kwa kipindi kile alihifadhiwa kutajwa jina lake ktk Mahakama kuu ya Zanzibar.
Wazee wetu Zanzibar wanasema asilimia % 70 ya kifo cha Father K kilipangwa na Master plan ya Nyerere ili apate kuitawala Zanzibar kiujanja ujanja kwa vile kuna baadhi ya mambo Father K alikuwa msugu na asio kubali kirahisi.
Siri nyingi zilijitokeza baada ya kufa Father K lakini usalama wa taifa walijaribu kuzizima kwa mkono wa chuma wa Nyerere kutimiza malengo yake ya kuifunika Zanzibar kiutawala.
Sababu za kifo cha Father K
Baada ya Nyerere kumuona Karume kuwa baadhi ya mambo sio mwepesi wakukubali alijaribiu kujifanya dumi lakuwili na Master plan na kumtumia Humud na kundi lake kwa kuwapika chuki kumbe alikuwa na ajenda yake mbali ya kuitawala Zanzibar kimpinu.
Father K nakumbuka pale katika uwanja wa Maisara alitutangazia kuwa wananchi wa Zanzibar musiwe na wasi wasi na Muungano, huu Muungano ni wakipindi cha miaka 10 tu ikifika miaka kumi tutauangalia vipi unatufaa au vipi?.
Na kabla ya miaka kumi ikiwa hautufai basi tutauvuja nikama vile koti ikiwa tutahisi linatubana basi tutalivua au ikiwa tunahisi linatuletea joto basi tutalivua tubakie na chati ,
Wengi wanasema hawakumfahamu raisi wetu alikusudia nini siku ile, badhi ya wazee wamekuja kufahamu hivi sasa kuwa Father K alikuwa tayari amesha mfanyia wasi wasi mwenzake Nyerere kuwa hakuwa na nia njema na Muungano.
Kuanzia kipindi kile alichotutangazia katika hadhara Mh Karume ilianza mivutano na vugu vugu za ndani na kulikuwa na hata kufarikiana badhi ya wakati wazee wa karibu na Father K wanasema.
Kuna tetesi zinasema kuna badhi ya kipindi Father K alikuwa akinugunika kuwa Nyerere anajifanya kaka mkubwa mwenye kumpangia mambo akafika hadi kusema sote ni wanaume na mwanamme hapangiwi kazi ya kufanya na mwaname mwenzake.
Migogoro ilikuja pale Nyerere alipotaka kupitisha mambo kwa Tanganyika na yafanye kazi mpaka Zanzibar na mengine nikama vile pesa za kigeni alitaka Nyerere azikamate yeye Tanganyika hali yakuwa Zanzibar ilikuwa inajitosheleza kifedha ukilinganicha na Tanganyika kipindi hicho.
Nyerere hakuwa na zamira njema na Karume katika Muungano, bali alikuwa na agenda yake mbali na fikra za Karume, alijaribu kujifanya Ndumi la kuwili ili lengo lake liwe kuitawala Zanzibar.
Nyerere bada ya mapinduzi ya Zanzibar 1964 kumgowa Sultan alitumia kigezo cha kumchawichi Karume kwa kumteka mawazo kwa kumwambia nitakuwa karibu sana na wewe kiulinzi na kimawazo ili Warabu wasiweze kurudi tena kukupinduwa.
Ndio hapa akatumiminia Jeshi la Wakuria kila pembe ya visiwa vya Unguja na Pemba hii nikuona kuwa Karume kulindwa kumbe ni kuwa Zanzibar katika himaya ya kijeshi na mikononi mwa Juliasi.
Baada ya kupinduliwa Sultan (Warabu) Nyerere aliwapokea warabu Tanganyika makundi kwa makundi na kuwapa hifadhi bila ziki, kama kweli hakuwa na agenda ya siri kwa nini aliwapa hifadhi? .
Lakini agenda ya Nyerere ilikuwa sio Warabu nikuizibiti Zanzibar tukiashana na Sultan(Warabu) kulikuwa na Wazanzibar wasomi na wana Afro –Shiraz na wana mapinduzi kindaki ndaki akina Hanga, Mdugi Ussi,Othman Sharif, Jahaa na wenzake.
Hawa wote walikuwa Wazanzibar safi na wamesoma na ni wafrica wa Zanzibar na wana Afro-Shirazi na wana Mapinduzi no 1 lakini walifanywa nini na Ndumi la kuiwi Nyerere kwa kumtia sumu mbaya Karume.
Nyerere aliona kumuua tu Father K haito tocha kama hawa Wazanzibar halisi wasomi wana Afroshirazi na wana mapinduzi na Wafrica bado watakuwepo, alichokifanya alitumia mrija wa sumu kati ya hawa na Karume kwa kuwagonganicha vichwa.
Kilicho fanywa na Master plan Nyerere mara hii ilikuwa sio plan ya Sultani (warabu) kurudi na kumpinduwa ni kulete mfarakano wa Karume na wana mapinduzi wana Afro-Shirazi wenzake akina Mdugi Ussi na wenzake kugonganichwa vichwa.
Technique ya mara ya mipango ya Nyerere ni ufisadi wa kupika sumu ya fitna na kumpa Karume kwa kumwambia kuwa kama huja washuhulikia hawa akina Mdungi Ussi na wenzake basi kuna hatari ya kukupinduwa hawa ni Wazanzibar safi na wasomi walio bobea.
Baada ya Nyerere kufanikiwa hivyo Karume ikawa hana raha tena na watu hawa ndipo pale alipoanza kuwa sumbua na takribani wengi walikimbilia Tanganyika kutokana na kuhisi kuwa mafahamiano na Karume yamekuwa madogo.
Hawa hawakupata mapokezi mazuri kwa Nyerere ilikuwa bora ya wale Sultan(Warabu) Nyerere aliwapokea na kuwapa hifadhi kuliko hawa wana mapinduzi wana wa Afro-Shirazi na Wafrika.
Hofu ya Nyerere kwa hawa ilikuwa ni kushindwa kutimiza zima yake ya kuitawala Zanzibar kama bado watakuwa hai, ndio akaamua kupeleka fitna zakwamba hawa wana anjenda ya kukupinduwa kwa hio Nyerere akawapeleka Zanzibar na kwenda kuwawa.
Kwa hio Nyerere hakuwa na zamira nyema na Zanzibar ,mapinduzi wala Karume na Kundi lake la Afro-Shirazi.
Jee Wazanzibar tujiulize hawa akina Mdugi Ussi,Ubwa Jaha,Othani Shariff na wenzake kosa lao nini na hawa walikuwa wana mapinduzi ,Afro –shirazi,Wazanzibar na Wafrika weusi jee vifo vyao mpaka leo vina utata, jee kosa lao nini?.
Mungu ibariki Zanzibar na Wazanzibar wote.
 
Yule askari alitempiga risasi Karume na Sheikh Thabit Kombo inasemekana alikuwa analipiza kisasi cha marehemu baba yake aliyeuawa na Karume; sasa hapo Nyerere anaingiaje? Acha spin zenu nyie wazenj!
 
Muungano umefikia pabaya watanganyika na wazanzbar kila mtu aachiwe nchi yake maisha yaendelee.Hizi chokochoko hazisaidii."kama koti limewabana bakini na shati"kuliko kupga tikitaka ukiwa umevaa msuli
 
"kama ningeweza kukivuta kisiwa kile mpaka katikati ya bahari ya hindi, ningefanya hivyo, kwa kweli sitanii nina wasiwasi kitatuletea matatizo makubwa sana huko mbeleni" by J K Nyerere-1961.
 
"kama watu wa zanzibar wakiona kwamba muungano hauwafaidii kitu, na kama kweli watu wa zanzibar wanaona hivyo, mimi siwezi hata kidogo kuwaua wananchi wa zanzibar. kama waliingia katika muungano kwa hiari yao wanaweza pia kujitenga kwa hiari yao. hatukuishinda zanzibar vitani" by J K Nyerere.
 
Endeleeni kujifariji, mke akiichoka ndoa huanza kuleta visa na vituko ili apewe talaka, mume mwerevu humbembeleza mkewe na talaka hatowi!. Tanganyika ni mume mwerevu hakuna talaka!.

Tena sio tuu Tanganyika ni mume mwerevu, pia ni mume mstahimilivu, alimsamehe mkewe hata alipotembea nje ya ndoa kwa kugawa penzi kwa OIC!. Alimsihi mke asigawe tena na mapenzi ya wawili hawa yanaendelea murua!.

Dawa ya mke mkorofi ni kumuongezea wake wenza, atatulia na kwa mujibu wa sharia mwisho wake wanne!.Sasa tumechumbia Uganda, Kenya, na Rwanda na Burundi katika ndoa ijayo ya federation!. Mke Zanzibar sasa atashika adabu!.

Ushauri kwa wachokonozi wa muungano wetu adhimu!, " Choko choko mchokoe Pweza, Binadamu Hutamweza!".

Mwal. Nyerere, Baba wa Taifa, Pumzika kwa Amani!. Safari ya kumtangaza Mwenye Heri, inaendelea!.

Raha ya Milele umpe eeh Bwana!, na Mwanga wa Milele Umwangazie, Apumzike kwa Amani.... Amen!.
 
Muungano umefikia pabaya watanganyika na wazanzbar kila mtu aachiwe nchi yake maisha yaendelee.Hizi chokochoko hazisaidii."kama koti limewabana bakini na shati"kuliko kupga tikitaka ukiwa umevaa msuli

Mkuu wabaki na shati na joto hili? mimi nadhani wabaki na BIKINI
 
wazanziberi bwana!Karume awaue maadui zake kwa sabab za kutokujiamini kwake kisha lawama mumtupie Nyerere! so lame!!

Zanziberi lazma iendelee kuwa chini ya Tanganyika coz tukiwaachia tu nyie watu,Al qaeda,Alshabab na wenzie kambi yao kuu inakua zenji..we can not afford that!Mi natoa big up kwa Nyerere hapo alicheza kama Messi hapo manake sa hv tungekua na taab sana!

Tatizo mzee wenu yule alikua hazimtoshi kiaina!!
 
endeleeni kujifariji, mke akiichoka ndoa huanza kuleta visa na vituko ili apewe talaka, mume mwerevu humbembeleza mkewe na talaka hatowi!. Tanganyika ni mume mwerevu hakuna talaka!.

Tena sio tuu tanganyika ni mume mwerevu, pia ni mume mstahimilivu, alimsamehe mkewe hata alipotembea nje ya ndoa kwa kugawa penzi kwa oic!. Alimsihi mke asigawe tena na mapenzi ya wawili hawa yanaendelea murua!.

Dawa ya mke mkorofi ni kumuongezea wake wenza, atatulia na kwa mujibu wa sharia mwisho wake wanne!.sasa tumechumbia uganda, kenya, na rwanda na burundi katika ndoa ijayo ya federation!. Mke zanzibar sasa atashika adabu!.

Ushauri kwa wachokonozi wa muungano wetu adhimu!, " choko choko mchokoe pweza, binadamu hutamweza!".

Mwal. Nyerere, baba wa taifa, pumzika kwa amani!. Safari ya kumtangaza mwenye heri, inaendelea!.

Raha ya milele umpe eeh bwana!, na mwanga wa milele umwangazie, apumzike kwa amani.... Amen!.

great,greater,greatest thinker
 
hii itabaki kuwa tetesi tuu , lakini ni kweli yule askari alikuwa analipiza kisasi kwa karume kuua ndugu zake , alikuwa komandoo , nyerere alihusika kwani boti iliyokuwa iwachukue huyu askari kukimbilia dar es salaam baada ya mauaji , boti ilimwacha walinzi wakamuua , wale waliokuwa kwenye boti walipewa hifadhi bara na vyeo lukuki ....ndo chanzo cha wana ccm kumuhusisha salim kwenye mauaji ya karume kipindi cha uchaguzi 2005 ..lakini all in all mkono unamwelekeza nyerere ...source: mtoto wa huyo askari yupo ughaibuni alikimbia ,kama ni mfuatiliaji utajua mama yake yaani mke wa huyu askari x , alichukuliwa akawekwa kizuizini wakati mjauzito na huyu mtoto . nyerere nooma aiseee
 
Banda la Uani mna mambo nyie,
Mkimaliza ya Nyerere mtuletee ya Kawawa basi!

Hapo kwenye red umenikosha wallahi! ila hata uswazi kwenye nyumba za kupanga huwa wapangaji wa mabanda ya uani hawaishi visa na chokochoko, tushawazoea hao akina yakheee! watunzi maarufu wa hekaya.
 
Back
Top Bottom