Jee Bunge La Dharura Kuitishwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jee Bunge La Dharura Kuitishwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, May 4, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,548
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  JK ameteua wabunge watatu wapya na kuna uwezekano wawili kati yao atawateua mawaziri!.

  Ili mtu kuteuliwa waziri lazima kwanza uwe mbunge. Mtu akiteuliwa Mbunge, hawi mbunge bali huwa mbunge mteule mpaka baada ya kuapishwa!.

  Mbunge mteule hawezi kuteuliwa kuwa waziri mpaka kwanza awe mbunge!.

  Hivyo jee kutaitishwa kikao cha bunge la dharura ili hao wateuliwa wapya waukwae uwaziri, au JK atatuvunjia tena katiba kwa kututeuliwa mawaziri ambao sio wabunge bali ni wabunge wateule?!.

  Ila kama atambadili PM basi ni lazima kwanza bunge la dharura likutane kupitisha jina la PM, then PM na Rais ndio wakae chini kupendekeza baraza la mawaziri!.

  Subirieni taarifa ya kikao cha bunge la dharura!.

  Pasco.
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  May 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Pasco tangia juzi tumekuwa tukiongelea suala hili na tulikuwa tukiongelea kama Rais angetaka kumtumia Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa UN kwenye baraza lake la mawaziri. Ingebidi amteue kuwa mbunge kwa mujibu wa Ibara ya 66 (1) (e). Na mbunge anatakiwa aaape. Lakini nimepata hii ibara 68 inasema hivi, "Kila mbunge atatakiwa kuapishwa katika Bunge kiapo cha uaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za bunge ..." Labda watatumia haka kakifungu kwamba anaweza akashika madaraka ya uwaziri lakini kabla hajashiriki shughuli za bunge akaapishwa. Jinsi nionavyo huenda hakuna Bunge la dharura. Angeliitisha kabla hata hajatangaza wateule. Kwa kuwa huwezi kuitisha bunge la dharura ndani ya siku mbili; nadhani kwa uchache inabidi wapate taarifa hata wiki moja kabla.
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Ni lini JK alivunja katiba?
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kuendelea na Pinda ni kurudi kulekule Misri!
  Pinda atasababisha hata mawaziri waliokuwa wazuri waanze kuiba hela zetu, maana watajihakikishia kutoguswa na mtu!
  Whatever new faces that the president could employ into his cabinet, with Pinda being the PM, everything will go into shambles...ni kama mmasai kuingia disco na sime!
   
 5. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Soma Mwananchi ya leo ufafanuzi uko kwenye gazeti hili
   
 6. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,257
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  ...labda mabadiliko ni juni.
  Au wataapa baadae kama sio ofisi ndogo za bunge.
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,733
  Trophy Points: 280

  ....Mkuu nakubaliana nawe lakini si Pinda pekee hata kuendelea kuwepo msanii pale Ikulu ni janga kubwa la Taifa. Sioni kipya chochote ha kuwatia moyo Watanzania kuhusu mabadiliko katika utendaji Serikalini kati ya sasa na 2015.
   
 8. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #8
  May 4, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145

  Mkuu Kimbunga,
  Hata mimi nilikuwa na mashaka sana juu ya jambo hilo, kwamba mbunge mteule anawezaje kuteuliwa kuwa waziri kabla hajaapishwa?
  Kama ulivyofafanua, ndivyo niliisikia BBC jana jioni wakim-quote katibu wa bunge kwamba wanaweza kuteuliwa kuwa mawaziri na wakaendelea na majukumu yao isipokuwa yale tu ya kibunge. Kwa mfano kujibu maswali bungeni.

  Kwahiyo Kikwete atakuwa ameshapata ushauri mapema kabla ya kufanya uteuzi wa wabunge ili akamilishe kazi yake ya kulisuka upya baraza la mawaziri. Sitegemei kabisa kuwepo kwa bunge la dharura kwa ajili ya hoja ya kumjadili waziri mkuu. Hata hivyo matarajio yangu ni kwamba Pinda ataendelea kuwa waziri mkuu hadi akamilishe ngwe yake sioni dalili za kikwete kumtosa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Ndani ya katiba hakuna mnachoita "Bunge la Dharura". Hata hivyo, uwezekano wa kuitwa hilo mnaloliita "Bunge la Dharura" kwa hali ya sasa kinaweza kutokea kwa sababu mbili:

  1:
  JK asipoteua leo Cabinet, basi Jumatatu Zitto na wale wenzake 70 wataanza kumbana Spika kuwa anasubiri nini kuhusu hoja yao ambayo kikatiba inataka kuanzia Jumatatu uanze mchakato wa kuwaita wabunge Dodoma wapige kura ya kutokuwa na Imani na PM. Hoja hii inajitegemea na haina uhusiano na siasa au porojo zinazoendelea nje ya Bunge, bila kujali ni Ikulu, magzetini au mitandaoni. Kuna mada tuliijadili hapa last week imeliweka vizuri sana hili. Link yake hii hapa:

  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/259819-kitanzi-cha-zitto-kinavyomtesa-spika-serikali.html


  2:
  JK akiteua Mawaziri na aakaondokana na Pinda, basi hilo BUnge lazima liitwe.

  NB:

  Haya ni mambo mawili ambayo lazima moja litokee ili bunge liitwe ndani ya hizi wiki mbili. Na kutokana na mazingira inaelekea mojawapo linaweza kutokea.
   
 10. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #10
  May 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Naaam Mwita Maranya nimekuwa nikipitia Katiba ndio nikaona hilo. Ila kama angemtoa Waziri Mkuu ingebidi kwanza atangaze kulivunja baraza la mawaziri (au PM ajiuzulu - automatically baraza linavunjika) , aitishe bunge kumpitisha jina la PM kisha wakae na PM kushauriana kuunda baraza jipya.

  Kwa hali ilivyo sasa kinachofanyika ni mabadiliko ya baraza la mawaziri na Pinda ndiye Waziri Mkuu pasipo na shaka yoyote.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Hivi kwa nini tunakimbilia kudhani lazima apate ushauri kwa masuala mengine ambayo ni rahisi sana. Hebu tusome ibara zifuatazo za Katiba, ili tuone ilivyo wazi hata mtoto wa primary akisoma ataelewa:


  {KATIBA: 55(4)}:
  Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka miongoni mwa Wabunge

  {KATIBA: Ib. 56}:
  Waziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ila mpaka awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.

  {KATIBA: Ib. 51(1)}:
  Muda wa kushika madaraka ya Waziri na Naibu Waziri utaanza tarehe atakapoteuliwa kushika madaraka hayo.
   
 12. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #12
  May 4, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Mamlaka ya rais ni kuteua Mbunge kuwa waziri ila Hana mamlaka ya kumteua Mbunge mteule ie Mbunge ambaye hajala kiapo kuwa waziri. Maelezo ya katibu wa bunge yanaishia kwenye bunge tuu, hatuwezi kustretch kwa mawaziri. Ndio maana hata marehemu sumari alipofariki pamoja na kuwa hakuwa ameapa na hakufanya kazi yoyote ya kibunge lakini lakini bunge lilimtambua Kama hivyo.

  Waziri asiye Mbunge akila kiapo cha uwaziri basi kiapo litakuwa batili.

  Hayo hapo juu hayaharamishi rais kuteua Mtu asiyenasifa kuwa waziri, lakini hatafanya kazi ya uwaziri aliyoteuliwa mpaka atakapoapa.
   
 13. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #13
  May 4, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Unauliza ni lini JK alivunja katiba au ni lini JK hajavunja katiba?
   
 14. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #14
  May 4, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Vuta pumzi kidogo Nikupateje ili uelewe kinachozungumzwa hapa.
  Ndio maana kuna ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, kikwete ama raisi yeyote hawezi kufanya/kujua kila kitu, vinginevyo asingehitaji kuwa na Jaji Werema.

  Ibara hii, hasa huo mstari nilio-highliht ndio ulisababisha madukuduku yote hadi tukaanza kuhoji na kutafuta ushauri kwa wajuzi wa sheria, na bila shaka hata raisi kikwete alim-consult werema ili kuona kwamba kama atawateua wabunge wateule kuwa mawaziri asikiuke katiba.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  May 4, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,548
  Trophy Points: 280
  Nikupateje, bunge la dharura lipo, niko mobile nikitulia nitakuletea vifungu
   
 16. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #16
  May 4, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Ni lini alivunja katiba?
   
 17. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #17
  May 4, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu Ngambo Ngali, kama sijakuelewa vizuri ama unajichanganya maelezo yako.

  Unasema raisi hawezi kumteua mbunge mteule kuwa waziri kwakuwa bado hajala kiapo.
  Lakini hapo hapo unamtaja marehemu sumari ambaye hakuwa ameapishwa kuwa mbunge lakini alipofariki alipewa heshima zote za mbunge, sasa hapo tofauti ni nini kati ya mbunge mteule na mbunge aliyekula kiapo?


  Kama unakubali na kutambua kwamba maelezo ya katibu wa bunge yanaishia kwenye bunge tu, na katibu huyo wa bunge amaefafanua kwamba waziri atakayeteuliwa huku akiwa mbunge mteule atafanya kazi zote za uwaziri isipokuwa tu zile zinazohusiana na bunge mathalani kuingia bungeni kujibu maswali n.k, kwa maana hiyo basi raisi anaweza kumteua mbunge mteule kuwa waziri na hatokuwa amevunja katiba.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #18
  May 4, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Pasco,
  Nasikia mmeitwa ikulu, bila shaka cabinet imesukwa hadi ikasukika.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #19
  May 4, 2012
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,799
  Likes Received: 6,309
  Trophy Points: 280
  Hakuna ajuaye kama atamteua yeyote kati ya wale watatu kuwa Waziri.
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  May 4, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,548
  Trophy Points: 280
  Kifungu hicho kimemaliza kila kitu!. Kiukweli hakuna uhakika wabunge walioteuliwa ndio sura mpya kwenye BM yote ni speculations tuu!.

  Ila lazima nikiri baadhi ya teuzi za JK leave much to be desired!. Sikuona mantiki ya kumteua Mama Meghji mpaka sasa sina kumbukumbu kama amewahi kuchangia chochote!.

  Bunge lililopita aliwateua Mama Mbene na Jussa kuwa wabunge at 11th hour!. Kwa kumbukumbu yangu Mama Mbene alichangia mara 1 tuu mpaka bunge lilipovunjwa!. Sasa kama kamteua tena asipompa uwaziri au unaibu then sisi tunaomfahamu vizuri JK tutajua huo ni uteuzi wa asante kwa mambo yetu yale!.
   
Loading...