Mbona haujataja utitili wa magazeti ya Mzee Mengi??tumekuwa wahanga wa jambo tusilolijua!Bila shaka wamekupata GAME THEORY. Tuna tatizo kubwa sana Tz. Kuna watu bila aibu wanathubutu kuwatetea mafisadi! Hebu waanzishe Forum yao tujue moja: kwamba wanawatetea mafisadi kwa maslahi yao. Watuachie hii JF tupambane kwa lengo la kuirejesha nchi yetu kwenye mwelekeo sahihi. Magazeti uliyoyataja yanamilikiwa na mafisadi kama ifuatavyo: Sauti Huru (Subash Patel), Nyundo/Tazama (Lowassa), Mtanzania/Rai (Rostam Aziz), Taifa Tanzania (Nazir Karamagi). Na sasa fisadi Tanil Somaiya ameinunua Channel 10. Hebu sikilizeni upuuzi kwenye TV station hii iliyokuwa inaheshimika kabla ya kuangukia mikononi mwa mafisadi. Inasikitisha. Lakini ushindi katika vita hii ngumu dhidi ya ufisadi ni lazima!
hata mie nawaona mkuu hamtoki hapa au vipi?Hatuondoki Ng'o!
Wakati haya mapambano yanaanza hata mengi mwenyewe alikuwa kimya kabisa hakuna hata gazeti lake lililokuwa linaandika haya. Baadaye wakaanza kwanini no body knowz.
umependa nini zaidi?habari yenyewe kuwa umelipwa na Mengi kumtetea au?
Period!
umependa nini zaidi?habari yenyewe kuwa umelipwa na Mengi kumtetea au?
Period!
Mimi siko kwenye payroll ya Mengi wala Rostam, lakini kwenye orodha ya ufisadi, ni kitendawili kujua haswa nani anayemzidi mwenzake kati ya hawa wawili. SIWATETEI!
neutrality is the position of the weak and those who don't want to offend.. (MM)