Jedwali la Mengi: Nani hayumo?

Ndiyo nililipiwa kwa kuwa sikuwa ma uwezo..ila kupewa pesa siyo kosa ziwe za kifisadi ama la
So wanaofadhiliwa na kina RA like Simba (UWT), JK (Upresident 05) et al hawana kosa heheeeee!

Pia unataka kusema kwakuwa watanzania walio wengi ambao ni masikini wa kutupwa waendelee kupokea vimisaada toka kwa mafisadi eti kwakuwa wao hawana uwezo badala na kupambana na hao mafisadi kwa nguvu zote kuikomboa nchi?


ila nililipiwa na nani?hapo ndipo haujui kabisa....ona unavyopotea,leta ushahidi
Hili swali halina mantiki, kwa kuwa umekubali kusomeshwa kwa pesa za mafisadi eti ulikuwa huna uwezo......wewe kama kweli ni mzalendo mtaje huyu fisadi aliyekusomesha tumshughulikie!
 
NI thread ya kipuuzi sana hii. Bila shaka imeandikwa na ROSTAM au LOWASSA. Hebu tuondelee ujinga huu ili Watanzania waendelee kuwafahamu vizuri mafisadi wanaoikamua nchi yao wakiongozwa na huyu MBURUSHI ROSTAM.
 
NI thread ya kipuuzi sana hii. Bila shaka imeandikwa na ROSTAM au LOWASSA. Hebu tuondelee ujinga huu ili Watanzania waendelee kuwafahamu vizuri mafisadi wanaoikamua nchi yao wakiongozwa na huyu MBURUSHI ROSTAM.

Swadakta..!
 
NI thread ya kipuuzi sana hii. Bila shaka imeandikwa na ROSTAM au LOWASSA. Hebu tuondelee ujinga huu ili Watanzania waendelee kuwafahamu vizuri mafisadi wanaoikamua nchi yao wakiongozwa na huyu MBURUSHI ROSTAM.

wewe nawe,

kila kitu lazima uchangie..si ukae kimya!

Mie hata Rostam sijawahi kumuona..unaona sasa hauna tofauti na mimi,tuna katabia ka kuhisi mambo tu
 
Soma katikati ya mistari,ukichukua sentensi zote utapotea..hii thread ni matayarisho tu ya weekend mkuu..

Nyani Ngabu yuko wapi?

tunavuta pumzi kidogo...akili zatu zimejaa Mengi ...mara Rostam...tumesahau kujadili mambo ya muhimu...

Mtindio vipi uko upande gani?
 
When it comes to Jokes we normally accept em buddy.

BTW: Nilisema "Nahisi" na wala sikuthibitisha.

I can ban myself, simply report to me!

Jamani kama ni utani basi ipelekwe kwenye Jukwaa lake la Jokes/Utani mana nimepoteza kama 30min nasoma thread baada ya thread sijapata kitu cha maana aaah... siku JF inapodolola basi inakua taabu kweli watu wanaanza kubuni Topic za kifikilika.
 
Nyani Ngabu yuko wapi?

tunavuta pumzi kidogo...akili zatu zimejaa Mengi ...mara Rostam...tumesahau kujadili mambo ya muhimu...

Mtindio vipi uko upande gani?

Nasubiria cheque kutoka kwa Mengi.
 
Nyani Ngabu yuko wapi?

tunavuta pumzi kidogo...akili zatu zimejaa Mengi ...mara Rostam...tumesahau kujadili mambo ya muhimu...

Mtindio vipi uko upande gani?

Gembe, usinisahau na mimi niko kwenye pay-roll ya Mengi. Hili swali nililoliandika hapa JF lilitumika wakati wa press conference ya Mengi juzi:
"Kama Rostam ataamua kumshambulia Mengi kwa kudai naye ana mabaya ambayo amefanya...aulizwe ni kwanini anataja hayo mabaya sasa hivi baada ya yeye kutuhumiwa kuwa ni fisadi papa............?"
 
NI thread ya kipuuzi sana hii. Bila shaka imeandikwa na ROSTAM au LOWASSA. Hebu tuondelee ujinga huu ili Watanzania waendelee kuwafahamu vizuri mafisadi wanaoikamua nchi yao wakiongozwa na huyu MBURUSHI ROSTAM.

Mwingine huyo.... ongeza kule kwenye PAYROLL
 
Duh mkuu na wewe umo nini?
Pesa taaaaamu jamani kha!

Kwa hiyo hapa kuna vita ya upande wa Mengi na upande wa RA duh wote hawa wapambe...wengi wa wapambe wa Mengi naona wanakataa kuwa Mengi si mwizi,muhujumu kazi kweli kweli....

Mkuu Fidel naona uwanja wa politic mgumu sana kwako........nashauri endelea kujiimarisha kuleeeeeeeeeee!
 
Wakuu siamini kama kuna watu wanafanya maamuzi siku hizi kwa kufuata hisia.Huyu bwana Gembe anashangaza sana na naweza kumfananisha na Idd Amin aliyemuua mwanae kwa kuhisi kuwa atampindua. Bwana Gembe afanye utafiti kwanza kabla ya kukurupuka na kutoa maneno ambayo kwangu naona kama ndoto za mchana. Kwanza kwa mzalendo mwenye uchungu na mali ya taifa letu hawezi kupost kitu namna hii vinginevyo yeye ni mlinda mafisadi na pengine yeye ndo yuko kwenye payroll ya Rostam.Watu wa namna hii ndo wanaosema rais kashindwa kazi wakati kazi ni ya watanzania wote kupiga vita ufisani. LET US STAND UP AND FIGHT FOR OUR RESOURCES.
 
Nilishajitoa kujadili haya maswala lakini nimegundua halikuwa jambo la busara. Ni ushauri wangu kwa wanaJF tusipoteze muda na hawa watu...mi nawaona wote wahuni tu. Gembe hujatumia busara kuwataja watu fulani kuwa wako kwenye payroll wakati huna hata salary slip zao, suala la kutoa maoni limegawanyika katika makundi tofauti, kwa mfano:

1. Kuna watu wako tayari kutia pamba masikioni ili kumuunga mkono au kumtetea mtu yeyote hata kama hawamjui kiundani ili mradi wanatoka kumoja, kabila moja, dini moja au ni mapenzi binafsi tu na jina au wasifu.

2. Kuna watu hawako tayari yaani piga ua, kumsema mtu ambaye kwa namna moja au nyingine jina lake linatamkika vizuri masikioni pake, anamapenzi binafsi na rangi ya mtu huyo, au alishawahi kupokea fadhila muhimu hapo nyuma.

3. Wengine wanaweza kukuunga mkono mtu ni kwasababu hawezi kukaa kimya penye mjadala kama huu wetu, ni sawa na kuangalia mpira ukasema mi timu yangu fulani hata kama unayo timu yako ambayo kwa muda ule haichezi. Kwa mfano: ilipocheza Man na Arsenal kuna wapenzi wa Chelsea na Livepool waliamua kuishangilia Arsenal si kwa kuipenda timu hiyo ila kwa maslahi yao binafsi.

Sasa wandugu tukirejea kwenye jukwaa letu. Ishu ya Mengi na RA haina mwisho....wapo wanaomuunga mkono RA kwa rangi yake na sura yake ya kimanga pengine hata kwa kuwa amesemwa sana na wameanza kusympathisize nae au kama wanavyosema wadau...wamenufaika na uwepo wake. Pia kuna wanamuunga mkono Mengi kwa rangi yake nyeusi na pengine wamemsikia mara nyingi akichangia vijisenti kwa wanyonge japo hawajui kama moyo huo upo pia kwa wafanyakazi wake.

Mimi binafsi nilikuwa upande wa RA na kundi lake kwa kuwa naamini hawakutendewa haki katika MTAJO wa Mengi...interest yangu ilikuwa ni misingi ya sheria inapofikia kuwataja watuhumiwa. Baadae nilibadilika na kuwaona wote WAHUNI kwani nao wakatumia njia ile ile ya Mengi ambayo kwangu si njia sahihi katika kutatua matatizo makubwa kama haya. Hivyo nawahisi ndugu zangu tuweke kando ubinafsi, chuki, fitina na hata mapenzi binafsi na tusimame katika taratibu za sheria....tuwahamasishe watanzania wafuate misingi hii na ikiwezekana twende mtaani kuwaambia watu HAWA wakabidhi malalamiko yao mbele ya vyombo vya sheria na sisi tuhakikishe haki inatendeka. TUKIFANYE HAYO TUTATENDA JAMBO LA MAANA KWA NCHI BADALA YA KUONYESHANA UMWAMBA WA KUJENGA HOJA VICHAKANI.
 
Kwa hiyo hapa kuna vita ya upande wa Mengi na upande wa RA duh wote hawa wapambe...wengi wa wapambe wa Mengi naona wanakataa kuwa Mengi si mwizi,muhujumu kazi kweli kweli....

Labda kama kuna riport tofauti za Mwakyembe na DK.Slaa ambazo zimtaja RA. na si RM si vibaya ukinikumbusha.
 
mahakamani akafanye nini ? Kwani yeye ni bwana mashtaka ???? Aidha anaweza kwenda police au takukuru....wao sasa ndio kazi yao kuchunguza.....
Amefanya jambo jema sana....watu majungu sana......fisadi ni fisadi tu..kama ni papa au nyangumi.....anachosema mengi ..ni tuhuuma na alichosema rostam ni tuhuma.....lakini kwa uchache alichotuhumiwa rostam ni marejeo ya akina dakitari slaa...lakini alichotuhumiwa mengi ni mapya...nani alijua kama nico chini ya mengi katumia hela za walalahoi za nico 2.5 billioni kazikaanga kwenye kiwanda chake??// na tena kimefilisika....kwa mtindo ule ule kopa tumia kidogo kwa kulisha pilau kwa albino...nyengine tumbua mwenyewe.....halafu ua kiwanda kilichokopa kifilisiwe...ndio utajiri wake.....kule usa kulikua na vitendo kama hivi....mnakumbuka kampuni iitwayo enron walikua na mtindo huu wa kukopa sana bank kwa kutuo mahesabu ya uongo kwamba company inafanya vizuri..then company vuuuu inafilisika....bank hawajui waanzie wapi kupata hela zao....hatimae wakurugenzi wake wako jela wanakula ugali....huwezi kuua company tu....ili usidaiwe na banks...ni wizi wakiaina....hatukujua..haya.....kuna lile la account ya billion 40 ya account ya ukimwi..rostam hakuitaja hii lakini.....inashangaza kidogo.......kweli mtu ataenda kufungua account kwa jina la mengi na kuingiza kiasi chote hicho cha pesa then mengi meza aseme yeye haijui account hio????? Kawaida banki zetu wanakupigia simu...wakati zikitolewa...hakuna bank isiyomjua mengi meza....huyu yumo ni nyangumi tu..kama mnampnda labda kwa kuwa hii forum ni ya wa moshi basi mapenzi yenu kwake ni haki yake....lakini ni fisadi kama wenzake...mimi nasema kama angekua vita hiii kaianzisha dt shein ama pinda basi hawa ndio safi tuliobakiwa nao tz yote..lakini sio mengi.....yeye ni mmoja wao
 
Mie mpaka sasa nimeona mambo matano

1.Kuna kundi la watu ambalo linatamani kabisa kuwamo katika payroll za Rostam ua Mengi ila halina uwezo wa kuingia huko na wanota siku waitwe.

2.kuna kundi ambalo linatetea maslahi la watu waliowadhamini na kufika mpaka hapo walipo,hawa wako tayari kumtetea mtu hata mpaka mwisho hata bila malipo yoyote.

3.Kundi la la tatu ni la watu ambo wenyewe wapo tu kwa maslahi ya wakubwa,hawa wako karibu na viongozi na hao wanoitwa mafisadi nyangumi na mafisadi papa.kazi yao ni kujua nani anasema nini,nani yuko wapi ana mipango gani na kupeleka ripoti kwa watu wao ,na mara nyingine huwasaidia kujibu hoja mbali mbli!

4.kundi la nne ni la wale ambo wanapenda sana pesa ,ila kwa wakati mwingine ni wapiganaji wa haki za watanzania(hawa ni ndumila kuwili).

5.Kundi la tano ni la watu wanaopenda kupigania haki za kila mtanzania,wanoangali hoja na wasio na ushabiki kwa mtu yeyote!



Baaada ya kutaja makundi hayo naomba kutoa maswali haya

a.Je wewe uko kundi gani?

b.unatamani kuwa kundi gani?

c.Je unahisi ni kundi lipi amblo ni la hatari zaidi?

Hii biashara ya makundi ndiyo inasababisha mafisadi wasikamatwe,hatarakati za maendeleo zisiwepo na hii ndiyo sababu iiliyotufikisha hapa,umasikini maisha duni na ya shida yamechangiwa na tabia ya kujenga makundi na wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutuingiza katika makundi hayo na tumeingia bila kujua na sasa tunawatumikia wao!

Makundi yameweza kutugawa na hakuna umoja wa kitaifa,watu wanalia kila siku ila uchawi umesababishwa na makundi na siye ni waumini tu!

Tafakari na chukua hatua,dhambi ya kutugawa itatupeleka kubaya...!


 
Mkuu Fidel naona uwanja wa politic mgumu sana kwako........nashauri endelea kujiimarisha kuleeeeeeeeeee!

hahahaha kweli mkuu umenena mimi humu ni mtazamaji maana uzoefu sina kabisa nitaandika nini huku zaidi ya kushangaa tu mkuu...lakini kule mkuu mi ndo kwenyewe nina uzoefu nako sana tu...
 
Nalikumbuka swali kwenye thread moja huko nyuma la, wewe umeifanyia nini Tanzania? Niliiona list ndefu kweli ya nini bwana mmoja aliyoifanyia hii nchi yetu tukufu. Duuh! Nikapata hisia kuwa nyingine ni sound tu.Pengine Mengi alihamasika na jinsi mtu mmoja alivyoweza kufanya mengi akaenda further step kusema aliyotaka sema!!
Demokrasia inaleta raha sana mana kila wazo lina nafasi yake.
Sioni kwanini Mengi asiseme anayotaka kusema mana anayo haki kikatiba.Kuna shaka so far hakuna ushahidi RA ni fisadi, sidhani pia kama kuna ushahidi wa payroll ya Mengi yumo nani? Kama upo utolewe vinginevyo ni zilezile porojo
 
Back
Top Bottom