Je, Zanzibar ni koloni la Tanganyika?

Je, Zanzibar ni koloni la Tanganyika?

Hongera CCM kwa ushindi wa kishindo. Chini ya uongozi wa makamanda mahiri JPM na Dkt Shein hatimaye ccm imeteka Pemba . Kwa mara ya kwanza mfumo wa vyama vingi CCM imeshinda viti vyote Pemba. Hongera dkt.
 
Kwani ccm huwa inashinda kiti cha urais? Si bars wala visiwani, ccm huwa haishindi hicho kiti.
 
Hongera sana CCMkwa ushindi wa kishindo kuliko tsunami
Zidum fikra sahihi za mwenyekiti.
Chama kiendelee kushika
Hatamu na utamu.
Kiwafyeke mabepari na makabaila
Wazururaji wote wapelekwe gezaulole..
Kituletee maendeleo zaidi
Maji safi yapo...elimu bora chama kimesimamia
Umeme upo kila sehemu...wakulima wanapata pembejea kwa urahisi
Na soko la mazao yao bila shida...
CCM juu ndio juuu juuuu zaidiii.............
 
Kinachopelekea Wazanzibari, kudai Mamlaka Kamili ya nchi yao ni kitendo kama hich.......Inakuwaje kiongozi kamili wa nchi lakini, wakati huo huo kuwa waziri wa kawaida wa nchi nyingine ya kigeni Ni kitendo cha udhalilishaji na kiini macho

Zanzibar ni nchi kamili iliyopata uhuru wake Desemba 10, 1963 kutoka kwa Muingereza na kuwa na serikali kamili yenye mamlaka yote, pamoja na uwanachama wa Umoja wa Mataifa na taasisi zake zote.

Kadhalika, Zanzibar baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964 chini ya Abeid Aman Karume na baada ya hapo chini ya Aboud Jumbe, Rais wa Zanzibar hakuwahi kuapishwa kuwa waziri asiye na wizara maalumu.

Hivi kweli Wazanzibari, hawajitambui?. Wote ni woga na hofu ya kuiogopa Tanganyika kwamba itawauwa kwa vifaru na mizinga au ni umamluki wa viongozi wa juu wa Zanzibari, kutokujitambua na kutambua kuwa Zanzibar ni nchi kamili kama ilivyo kwa Tanganyika?.

Swali: katika hali ya kutawaliwa kama hii, kweli Zanzibar, viongozi wake na wananchi kwa jumla wanatarajia kwamba ipo siku nchi yao itaondokana na kudhia ya kutawaliwa, kudhia ya umasikini, kudhia ya kuweza kusonga mbele na kupata maendeleo?.

Swali: Kwa nini wananchi wa Zanzibar, wanashindwa kubuni mbinu na mpango mbadala wa kuweza kujinasuwa na makucha ya utawala wa Tanganyika…Wazanzibari wanaridhika kuwa ni koloni la Tanganyika, mtawala mweusi tena masikini wakutupwa?.

Haijapata kutokea duniani popote, wala hatujawahi kusikia duniani popote kuwa Rais Kamili wa Nchi, aliyechaguliwa na wananchi wake kwa asilimia 91.4, lakini wakati huohuo kukubaliwa kuwa waziri asiyekuwa na wizara maalumu
Ndiyo maana inaaminika kuwa Zanzibar, inatawaliwa na mamluki kutoka Tanganyika.

Wazanzibari wamevumilia sana, wakitaka wasitake lazima walione hili leo bila kufika kesho, kuwa Zanzibar ni Jamhuri, hivyo hivyo na Tanganyika ni Jamhuri, kwa nini mmoja awe bwana (mtawala) dhidi ya mwingine.

Tunauliza: Wazanzibari wameleweshwa mvinyo gani na Tanganyika?. Wazanzibari wameridhika kutawali na Tanganyika kwa miaka nenda miaka rudi. Hivyo, kweli Wazanzibari wameridhika au hawana budi.

Hivyo, kweli Wazanzibari wemeridhika kuishi maisha ya dhiki na umasikini wa kutupwa huku, wakitawali kibabe-babe, hovyo hovyo na hadi lini au hadi mwisho wa dunia. Hali hii ndiyo itabaki kuwa hivi hadi kiama?.

Lakushangaza: Rais wa Zanzibar, anasikika anatamba akiwa juu ya jukwaa kuwa yeye ni rais, anatamba akiwa ndani ya Zanzibar tu. Kitendo cha kula kiapo kama waziri akiwa Tanganyika, kwa Wazanzibari kinawadhihirishia nini?.

Jambo la kustaajabisha sana ni kwamba, wasomi waliyopo Zanzibar na akili zote walizonazo Wazanzibari, wanashindwa kupata mwafaka kwa njia za amani kuweza kuepukana na ukoloni wa Tanganyika, ukoloni usiyokuwa na tija wala maslahi kwa Zanzibar na watu wake, zaidi ya shari na kuwagombanisha wenyewe kwa wenyewe.

Ni dhahiri kwamba, Wazanzibari wamepigwa changa la macho kutokana na kutawaliwa kwa mbinu na kwa kiini macho na mkoloni Tanganyika, wameleweshwa kama samaki wa pono kwa majani ya utupa.

Kuna msemo kwamba, ‘hakuna marefu yasiyokuwa na mwisho’ lakini lazima juhudi maalumu zichukuliwe ili kuweza kujikwamua na makucha ya mkoloni Tanganyika, vyinginevyo Zanzibar, arijojo..
 
Zanzibar ni koloni la Tanganyika kimuundo na kiutawala, hakuna mwenye akili anayeweza kubisha hilo.

Ulishaona wapi Rais wa nchi anaapishwa na Rais mwingine ili aingie kwenye kikao cha rais na mawaziri wake.??
 
Huu muungano no wa design ya ajabu. Rais wa nchi anakuja waziri wa muungano??
 
Wazanzibar tulieni bhana mbona kama mnawashwa
 
JE, ZANZIBAR NI KOLONI LA TANGANYIKA?

Rasimu ya Katiba mpya,sasa iko mikononi mwetu.Hii ni nafasi pekee kwetu Watanzania,kuisoma,kuielewa na kutoa maoni ya ama kuboresha,kuongeza au kupunguza chochote.Lakini sasa ni wajibu wa Mabaraza ya Katiba ya Kata na bunge la Katiba kuhakikisha wanajadili rasimu hiyo kwa kuweka masilahi ya Taifa mbele.

Kuna mapendekezo mengi sana katika rasimu ya katiba mpya.Lakini moja lililonigusa ni suala la Muungano.Tume ya mabadiliko ya Katiba mpya baada ya kupitia maoni ya watanzania imekuja,na mfumo wa serikali tatu,Tanzania bara (Tanganyika),Zanzibar na serikali ya Shirikisho.Kwa maana hiyo,kama mapendekezo hayo yatapitishwa na Mabaraza ya kata ya katiba,Bunge la Katiba na baadae kupigiwa kura na wananchi,ni wazi kwamba ule mfumo wa serikali mbili ambao umetumika kwa miaka 49 utakuwa umefika kikomo.

Mimi ni miongoni mwa watu wanaopinga pendekezo hilo.Sababu nitatoa.Kabla sijatoa sababu za kupinga mfumo wa serikali tatu,ningependa tujikumbushe japo kidogo tulikotoka.Historia ni mwalimu mzuri japo haiwezi kutufanya kuwa watumwa.

Ni miaka takribani 50 tangu nchi nyingi za Afrika zipate uhuru .Kizazi cha kwanza cha viongozi ambacho kilionja chungu ya ukoloni kwa kukamatwa,kupigwa,kuteswa na kuawa kiliona umuhimu wa bara la Afrika kuungana.Juhudi za kuungana kwa bara la Afrika ili kuwa na sauti moja kimataifa ziliongozwa na Kwame Nkrumah (Ghana) na Mwl.Nyerere (Tanzania).Japo miamba hii ya Afrika ilikuwa na maono/mawazo tofauti ya jinsi ya kufikia lengo la kuungana (AFRICAN UNION),lakini lengo lao lilikuwa ni moja,kuona Afrika inaungana na kukabiliana na ukoloni mamboleo (NEO-COLONIALISM),ambao kwa sasa tuungeita ni utandawazi (GLOBALIZATION).

Mwalimu Nyerere alikuwa ilipendekeza,ili kufikia lengo la kuwa na Afrika moja,basi ingekuwa vema kuanza na ushirikiano wa kikanda (REGIONAL INTEGRATION) kama vile EAC.Wakati Dr.Kwame Nkrumah alitaka kuharakisha kuungana kabla ya ukoloni mambo leo hajakita mizizi na kabla ya viongozi wapya wa Afrika huru hawajaona utamu wa madaraka.Mijadala ya wakati huo ilikuwa imegawanyika katika makundi hao,huku viongozi wengi wakipendelea wazo la Mwalimu Nyerere.

Ukisoma vitabu vya Nkrumah hasa AFRICA MUST UNITE (1963) na NEO-COLONIALISM (1965) ungeweza kuona dhamira ya wazi ya Nkrumah na hofu yake kwa ukoloni mambo leo.Viongozi wengi wa Afrika walimpinga na kumchukia Nkrumah huku wengine wakimwiita mroho wa madaraka.Lakini historia imethibitisha kwamba Nkrumah alikuwa ameona mbali sana.Hata katiba ya Ghana huru,ilikuwa na kipengele cha kwamba Ghana ingesalimisha mamlaka yake kwa Serikali ya Muungano wa Afrika endapo ingeundwa.Hata Mwalimu Nyerere akiongea kwenye maadhimisho ya miaka 40 ya uhuru wa Ghana,mwaka 1997 alikiri kuwa wazo la Nkrumal lilikuwa sahihi.

Baadaye tumeendelea na harakati za Pan-Africanism,ambayo mimi ni muumini,ingawaje kwa sasa imebaki jina tu.Mambo muhimu ambayo Pan-Africanism ilitakiwa kusimamia ni pamoja na maendeleo ya Afrika,kuimarisha demokrasia ndani ya bara la Afrika na kupinga ukoloni mambo leo.

Hata Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ilikuwa njia ya kuelekea kwenye umoja wa Afrika,japo kuna maelezo mengi kuhusu chanzo/sababu za Muungano huo,lakini kwa mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kupinga dhana ya kuungana.Kwa wakati ule inawezekana muundo wa Muungano ulikuwa safi.Na hili limewahi kuzungumzwa sana Mwalimu Nyerere.Kwamba isingekuwa rahisi sana kuunda serikali moja kutokana na historia.Wakati Tanganyika ilipoteza mamlaka yake,Zanzibar ikabaki na mambo kadhaa.Kutoka na sababu za kihistoria na udogo wa Zanzibar (geography and demography),ingeonekana kuimeza Zanzibar kwa kuunda serikali moja.

Lakini lengo lilikuwa kuona Zanzibar na Tanganyika zinaelekea kwenye serikali moja hatua kwa hatua.Lakini mambo yaliyoendelea baada ya Muungano kutoka pande zote mbili (Mwalimu Nyerere na Karume),pengine yaliharibu dhana nzima ya Muungano na kuzusha manunguniko kutoka pande zote mbili,hasa upande wa Zanzibar.Inasemekena Karume,kabla ya kifo chake alikuwa najiandaa kuvunja Muungano kwa kile kilichoitwa Mwalimu Nyerere kukiuka makubaliano ya awali,akitumia sentensi muungano ni kama koti likukubana unavua.

Kuna watu wachache wanaamini kwamba Zanzibar ni koloni la Tanganyika,na hili linatokana na namna masuala/hoja za Muungano zilizokuwa zinashughulikiwa.Moja ni namna mambo ya muungano yalivyoongezwa kutoka 11 hadi 22,ambayo tafsiri yake ingekuwa kupoteza Mamlaka ya Zanzibar.Hili lilisababishwa na udhaifu wa Karume ambaye hakujali mambo ya kisheria na ubabe wa Mwalimu Nyerere kwa upande wa pili.

Lakini suala la pili ambalo naliona ni kubwa zaidi ni kulazimishwa kujiuzuru aliyekuwa rais wa Zanzibar (1972-1984) Aboud Jumbe,kwa kuhoji mambo ya Muungano.Tafsiri ya suala hili,lingeonyesha kwamba Zanzibar sio nchi huru.Inakuwaje rais wa nchi anaondolewa kwa namna ile,bila hata kuwashirikisha wananchi wa Zanzibar?

Suala la tatu ni namna mijadala ya Muungano ilivyokuwa inashughulikiwa na kuzimwa.Japo hata Tanzania bara (Tanganyika) kulikuwa na mijadala lakini upande wa Zanzibar ilichukua sura nyingine (Nationalism).Waliokuwa wanahoji Muungano walikuwa wanaitwa wahaini.(REJEA KESI YA AKINA MALIM SEIF).Chama cha Wanannchi Cuf ni matokeo ya ubabe wa chama katika kushughulikia mambo ya Muungano.Hata Malim Seif,ambaye mimi namwona msaliti wa Wazanzibar,alionja joto la jiwe.

Kimsingi tukubaliane tu kwamba kulikuwa na makosa kadhaa katika namna ya kushughulikia kero za Muungano.Kutokana na udhaifu huo,ndio umezaa Zanzibar Nationalism,na sasa tunalazimika kuifufua Tanganyika.Wakati unabadilika.Waasisi wa Muungano walifanya kazi yao.Badala ya kuwalaumu,ni vema na sisi kizazi hiki tukatizama namna ya kushirikiana kama njia ya kutimiza wajibu wetu.Hatupaswi kuambiana maneno ya kuudhi,na kutumia neno ukoloni vibaya.Tuangalie historia,tuangalie mahitaji ya wakati huu na wakati ujao.

Suala la serikali tatu halijaanza leo.Tume ya Jaji Nyalali iliyoundwa na Rais Mwinyi mwaka 1992 kuangalia uwezekano wa kuanzisha vyama vingi,ilikuja na mapendekezo ya serikali tatu ikiwa ni njia ya kutatua kero za muungano ambalo hata hivyo halikutekelezwa.Mwaka mmoja baadaye kundi la wabunge lililopachikwa jina la G55 likaja na hoja ya serikali tatu,ambayo kimsingi bunge lilipitisha kabla ya Mwalimu Nyerere hajaizima hoja hiyo.(REJEA KITABU CHA UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA KILICHOANDIKWA NA MWALIMU NYERERE).

Mwaka 1998,Tume ya Jaji Mstaafu Kisanga iliyoundwa na Rais Mkapa ikaja na pendekezo la kuwa na serikali Tatu.Mambo yakawa yaleyale,pendekezo hilo likatupwa tena kapuni.Wakati ule,kama nilivyosema awali kujadili mambo ya Muungano ilionekana ni uhaini na hivyo kuzalisha manunguniko mioyoni mwa watu.

Sasa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nayo imekuja na wazo la serikali tatu.Kuna tofauti kubwa sana ,wakati ule na wa sasa.Kwa sasa wananchi wako huru kujadili suala la Muungano,hakuna vitisho.Lakini kwa upande wa Zanzibar hali ni tofauti.Katiba mpya kwao inamaanisha Muungano.Kuna wakati sauti zinasikika kutoka Zanzibar,kwa sasa ni wakati wa Zanzibar kutua mzigo.Japo ni wachache,lakini kuna watu wanaamini kwamba Zanzibar ni koloni la Tanganyika,na kwamba sasa ni wakati wa Zanzibar kupata uhuru.Sauti hizi zinatoka kwa viongozi wa chama na serikali,kuliko hata wananchi wa kawaida.

Hivi karibuni nilimsikia Ismail Jussa akiongea na idhaa ya Kiswahili ya DW,na kwamba sasa ni nafasi ya Zanzibar kupata mamlaka kamili,akitaja hasa Benki Kuu,Mambo ya Nje,Uhamiaji na Mambo ya Ndani.Tafsiri yake ni kwamba hapo hakuna Muungano.Huwezi kuwa kwenye Muungano na ukabaki na mamlaka kamili.

Binafsi napenda sana kumsikiliza Ismail Jussa akiongea mambo ya Muungano.Upendo wangu kwa Jussa hautokani na vile anavyojenga hoja,bali jinsi anavyoshindwa kuficha hisia zake na chama chake cha CUF.Kwa kiasi fulani nawafahamu Wazanzibar.Ukikutana na Mzanzibar msomi,utapenda jinsi anavyoongea taratibu,kwa umakini na kujenga hoja,huku akiwa na msimamo usiyoyumba kwenye masuala ya msingi.Sasa najiuliza,huo ndio mwisho wa zama za Zanzibar,kwa kuwa na vijana wanaopiga kelele badala ya kujenga hoja?

Tumeishi na Wazanzibar bila matatizo yoyote.Wazanzibar wengi wana makazi Tanzania bara kama ambavyo watu wa bara wana makazi Zanzibar.Tumeishi kama ndugu.Leo tunaposema Zanzibar ni koloni la Tanganyika,tunamaanisha nini?nini tafsiri yake?Mimi naona huu ni ubinafsi wa viongozi wetu wachache ambao wanataka kuneemeka kwa kuvunjika kwa Muungano.Na dhambi hii itaendelea kututafuna Waafrika.Wakati Mataifa yenye nguvu dunia yanaungana,sisi tunaona kujitenga ndio muhimu.

Bara la Afrika tuko nyuma sana kimaendeleo kuliko vile ninavyoweza kusema,hivyo umoja ndio unaweza kutusaidia kama Nkrumah na Mwalimu walivyoona miaka 50 iliyopita.Umuhimu wa Afrika kuungana leo ni mkubwa zaidi kuliko hata zama za Nkrumah.Sasa tunapojadili suala la Muungano,hebu tuangalie kwa jicho la mbali.

Mimi napinga mfumo wa serikali Tatu na badala yake tuwe na serikali moja tu.Kimantiki mfumo wa serikali tatu,unamaanisha unavunja Muungano.Pili kuendesha serikali Tatu katika hali tuliyonayo,ya uchumi dhaifu,ni kuleta mzigo mkubwa kwa walipa kodi,na utachelewesha maendeleo.Tatu,lengo letu liwe kuelekea kwenye Muungano wa Afrika.Hivyo ni vema tukawa na serikali moja,huku Tanganyika na Zanzibar tukizipa kisogo.

Ni jambo gani la kimaendeleo ambalo lilishindikana wakati wa serikali mbili,na sasa litawezekana kwa kuwa na serikali tatu?Je,kukwama kimaendeleo ya Tanzania,ni kwa sababu ya muundo wa serikali mbili?Wananchi wanachotaka ni maendeleo hata kama tungekuwa na serikali 20.Wananchi wengi wa kawaida hawana shida na Muungano.Tatizo lipo kwenye viongozi wachache ambao wanataka kuanzisha himaya za utawala kwa kuwa na viserikali vingi.Je,Zanzibar haijaendelea kwa sababu ya Muungano?

Ni vema wakati wa kutoa maoni yetu kuhusu Muungano,tutoe hoja na kuwasikiliza wengine.Kupiga kelele,hakuwafanyi watu wengine wakusikilize.Pia,wakati tunatoa hoja/maoni yetu kuhusu aina ya muungano tunaotaka,ni vema tukatumia lugha nzuri na za staha,huku tukiheshimiana.Kutumia maneno kama vile ukoloni si vizuri hasa ukiangalia tulivyoishi vizuri,kama ndugu.

IMEANDIKA NA BABA TUSAJIGWE (MUGO)
MAPAMBAZUKO TANZANIA
Ndio zanzibar ni koloni la Tanganyika, na mwinyi anaandaliwa kuwa gavana wa koloni hilo
 
Ndio zanzibar ni koloni la Tanganyika, na mwinyi anaandaliwa kuwa gavana wa koloni hilo
Mbona mnakuwa na mawazo haya? Wazanzibari si Watanzania? Zanzibar ni sehemu ya Tanzania si koloni yakhe!
 
Back
Top Bottom