Je, Zanzibar ni koloni la Tanganyika?

Je, Zanzibar ni koloni la Tanganyika?

Hili la uchumi siliafiki kabisa, sasa hivi hakuna huduma za jamii lakini kila kukicha watawala wanaota kuanzisha MIKOA, WILAYA na hata baraza la MAWAZIRI ni kubwa mno. Pana waziri pale kateuliwa kumtetea rais tu basi lakini haya HAMUYAONI kwa sababu ya rasilimali tuliyonayo ya UJINGA.
 
kama nilivyosema hii nchi ilikuwa moja na sasa no matter ni sababu za kijiografia, kiuchumi, kisiasa, kiuongozi au vyovyote vile, ilifika sehemu ikawa nchi mbili tofauti. Kiungwana na hasa kuangalia asili ya binadamu inabidi tuungane lakini kama upande mmoja hautaki huo muungano basi hakuna haja ya kulazimishana bali historia itatueleza ukweli huko mbeleni. Na Muungano mzuri ni wa serikali moja tofauti na hapo ni kuongeza gharama bila sababu kwa nchi masikini kama hii.

Haki ni haki hatopotea kama nilivyo tanguliza maoni yangu ktk. thread za awali kuwa LUGHA moja, UTAMADUNI mmoja, WATU waMoja,ELIMU moja, na vingi vya kushirikiana pamoja kwahiyo nchi moja!! WanaSiasa wenye magonjwa Lazima wafyekwe na kuwazuia kamwe, huu ni mswada wa wananchi peke. Wengi wanataka nchi moja.
 
nini maana ya mkoloni? labda apo ndo tutapata jibu muafaka?
 
Porojo tupu. Mbona hatukuona nchi nyengine kuungana na Tanzania na kuacha MAMLAkA Yake yote?. Ina Serikali 3 au basi Ukoloni wa Tanganyika
 
Inawezekana kweli zenj tuna wa-kolonise,kwanini hatutaki kuwasikiliza? Na kama tumewasikia mbona tunawang'ang'ania? Tukiachana sasa inaweza kuwa nzuri zaidi kuliko mda mwingine wowote na kama sisi mabingwa wa kuishi kwenye miungano twende burundi na rwanda!
Serikali mbili ndiyo tiba kamili,zenj mjirani zetu tukutane Eac.
 
Nauita ni ukoloni kwanini watanganyika hamjashawishi nchi nyengine kujiunga na muungano huu mna lazima iwe zanzbr pekee?ni miaka 49 sasa hamna liwalo,tumechoka na ukoloni mweusi na kama mna nia nzuri kwa nini kusiwe na muungano wa mkataba ili kuzipa nafasi nchi nyengine kujiunga?
 
kama ni kweli watanganyika wanapenda umoja kwa nn JK ASIENDE nairobi kuomba muungano wa kisiasa,au uganda si mliwasaidia kumuondoa idd amin kaunganeni nao maana mnafanana mpaka tabia au malawi ili muondoshe mzozo wa mpaka mlisha peleka majeshi mpakani eti mtapigana kulinda ziwa tu maji maji maji mnataka kuwa ndugu zenu....basi unganeni na msumbiji wao wana wamakonde na nyinyi mnao tatizo liko wapi...kenya,uganda,burundi, rwanda walitaka kuwe na jeshi la EAC na ardhi iwe EAC peke yenu mkakataaaa wanafiki wakubwa .
nguvu na akili zenu kwa visiwa vidongo vya bahari ya hindi ZANZIBAR huku mnataka serekali moja hamkuaza nyinyi kuvipenda visiwa hivi walikuja wareno,wajerumani hawakuweza kuingia,waingereza mwisho wakaviachia huru, warabu wa omani wakahamishia makao makuu znz wao walisha pafanya kwao tukawatoa kwa nguvu sasa zamu ya tanganyika game is over wajomba wakoloni weusi.wakoloni weupe.
itakuwa kosa kubwa tanganyika ikitumia nguvu kulazimisha muungano na znz ...
 
He, weee. dogo hilo? katoto ketu kamepata taaabu sana kumfuata babake. we unaona dogo hilo? na kasingekuwa na ujasiri wa kwetu mbeya kangefika? acha izo bwana....
Matoto yenu yanatupwa baharini kila leo yanaliwa na papa!! na wengine wanakamtwa na unga na kunyongwa huko ulaya na mangine yatumiwa humu humu jijini kuhudumiya wanaume na mengine yanaua kafara na washirikina ovyo!! na malbino mangapi wanatendewa mabaya!! sasa wenu alikuwa kwa muungwana bi.Mzuri alimlea ipasavyo na kuongoza aje huko Mbeya. shukuru hawa watu wema sana. long live Mwanaunguja!!
 
Sio kihivyo bali mimi naliangalia hivi: ukiangalia kwa miaka mingi nyuma unaiona Zanzibar kama kisiwa cha Mafia kwa maana kwamba wakaazi wake wa asili wanatokea bara (Tanganyika). Alafu historia inawaleta wafanyabiashara wa aina tofauti ikiwamo na ya utumwa hali iliyopelekea Sultan wa Oman kuhamishia makazi yake Zanzibar kama ilivyokuwa Kilwa kisiwani miaka ya mwanzoni. Ndio maana asili ya Wanzibari wengi (indigenous) ni mchanganyiko wa makabila.
Kwa maana hiyo Kijiografia ni sehemu ya bara na kihistoria inakuwa koloni la Sultani (Oman) hadi mapinduzi yalipofanyika.
Sasa angalia katika hili vuguvugu la kujitenga/kuungana:

  1. Baadhi ya Wazanzibar (sio vizuri kuwataja) wanataka wajitenge ili iwe rahisi kupata misaada ya nje hasa Oman ambao wanaweza kuweka kabisa makazi hapo mradi pesa imepatikana.
  2. Wengine wanapinga kurudi kwa ukoloni na kujiona wako sawa tu na hali iliyopo maana inawawezesha kushirikiana na ndugu zao wa bara bila vikwazo na wako tayari hata kwa serikali moja.
  3. Kundi la tatu ndilo lisilofaidika na siasa na hawagombei nafasi za utawala kama hayo makundi mengine lakini wanategemea upepo wenye kasi kutoka kwa hayo makundi mengine.

Kama ilivyokwisha kuelezwa hapo mwanzoni kuwa ili nchi iendelee inahitaji vifuatavyo:

  • ardhi
  • watu
  • siasa safi
  • uongozi bora

Inawezekana hivyo vitatu vipo na ndio maana Muungano ukawepo lakini hapo kwenye red ndicho kimekosekana sasa ikipelekea sababu ya yote haya kutokea.
Nchi zote duniani zinaungana kwa sababu kuna watu wa kuwaongoza kuwaunganisha. Kumbuka Canada walishataka kutengana eti kwa sababu upande mmoja unaongea Kifaransa na mwingine Kiingereza!!

Kinachotaka kufanyika sasa ni chuki za watu na njaa kwa ngazi ya binafsi na makundi na ndio maana hata wakitengana kama alivyosema Mwalimu utangano huo hautaishia hapo.
Tafakari kama haka kamchoro kanafanana na hali ya Zanzibar:
View attachment 97112

Nimependa sana uchambuzi wako. Lakini kuna hili. Ili uchambuzi huu kuwa na maana, unahitaji watu wanaoweza kuulewa pande zote mbili. Na ninaamini jibu ambalo lingepatikana ni kupata serikali moja ili tuelekeze nguvu zetu zote kwenye kuleta maendeleo kwenye hilo taifa letu moja litalozaliwa kwa kutumia hivi unavyoviorodhesha hapa:
ardhi
watu
siasa safi
uongozi bora

Tatizo ni kwamba je hili la serikali moja litawezekanaje katika mazingira ya ushawishi wa maseperatist kama kina Jusa na Seif?
 
kama ni kweli watanganyika wanapenda umoja kwa nn JK ASIENDE nairobi kuomba muungano wa kisiasa,au uganda si mliwasaidia kumuondoa idd amin kaunganeni nao maana mnafanana mpaka tabia au malawi ili muondoshe mzozo wa mpaka mlisha peleka majeshi mpakani eti mtapigana kulinda ziwa tu maji maji maji mnataka kuwa ndugu zenu....basi unganeni na msumbiji wao wana wamakonde na nyinyi mnao tatizo liko wapi...kenya,uganda,burundi, rwanda walitaka kuwe na jeshi la EAC na ardhi iwe EAC peke yenu mkakataaaa wanafiki wakubwa .
nguvu na akili zenu kwa visiwa vidongo vya bahari ya hindi ZANZIBAR huku mnataka serekali moja hamkuaza nyinyi kuvipenda visiwa hivi walikuja wareno,wajerumani hawakuweza kuingia,waingereza mwisho wakaviachia huru, warabu wa omani wakahamishia makao makuu znz wao walisha pafanya kwao tukawatoa kwa nguvu sasa zamu ya tanganyika game is over wajomba wakoloni weusi.wakoloni weupe.
itakuwa kosa kubwa tanganyika ikitumia nguvu kulazimisha muungano na znz ...
Ustadhi, Wasemaje waende na waganda au Wamalawi....wenzenu hawakuamini kupata Wanzaibari....nyie wazuri !!
nani awaachie watakufa nayie!! Wewe bhanaa! eti waende kwa Wamakonde? hakuna nyie tu nyie wetu!!
 
Ile dhambi ya "sisi" na "wao!" Yetu macho na masikio!

Mkuu,

Serikali moja tu finito! Unguja na Pemba ni visiwa vya Tanzania/Tanganyika kama vilivyo Mafia na Ukerewe. That way, hiyo dhambi haipo.
 
Kwani kwa sasa Bara inafaidika na nini na kanchi kadogo ka Zanzibar ka watu 1 milioni?
 
La Msingi Wazanzibari hawautaki muungano hata ungeimba mpaka asubuhi....
Sioni kwanini sisi Watanganyika tunawalazimisha.

Ivi tunafaida gani kiuchumi na hata kisiasa kuungana na hawa watu?


Pengine nielimishwe kwani naona hasara zaidi ya faida.
Tunatawala wote Tanzania bara lakini Tanzania visiwani marufuku na hata ukiwaita hivyo hawataki

Ngoja aje Barubaru na kina embe Boribo hapa wakutolee uvivu!!

Let Zanzibar go Let Uamsho go, tunaitaka TANGANYIKA YETU tuliyopewa na Mungu!


Changamoto za Serikali ya Tanganyika ni hiz.

1. mauaji ya Albino na vikongwe.
2. nani mwenye haki ya kuchinja kati ya waislam na wakristo.
3. Issue ya MoU ya kanisa na Serikali.
4. Malalamiko ya waislam kuhusu BAKWATA, Mahakama ya kadhi, siku ya mapumziko ya kiserikali n.k
5. Gesi kutoka Mtwara.
6. Kujiunga na OIC
7. Mfumo kristo unaondesha Serikali.
8. Husda na fitna za UDINI.


Je mmujipanga vipi kukabiliana nayo. Nafikiri ungepoteza muda wako mwingi kufikiria hayo badala kuifikiria Znz ambayo siku ya pili tu baada ya kupata Mamlaka kamili inajiunga na OIC.

Ondoa boriti katika jicho lako kwanza kabla kuangalia jicho la mwenzako.


Pole sana
 
Hivi watanganyika hamjiulizi ni kwanini nyerere ilimshinda kuimeza z'br wakati huo ambapo waz'br walikuwa laki 3 tu?kuimeza zanzibr ni ngumu ni sawa kuambiwa umeze mkuki,watanganyika wa sasa hamtoweza kuimeza z'br kwa sababu tayari wazbr wa leo wamejielewa,wamesoma,uzalendo zidi ya taifa lao umewajaa.
 
Kwa hapa tulipofika, Tanganyika bara haiwezi kuimeza Zanzibar tena. Hiyo miaka 49 plus nadhani imetosha sasa.

Kuna kipi cha ajabu kwa muungano kuiacha ZNZ iwe na mamlaka yake kamili kama nia ni nzuri?

Kwanini iwe tabu kwa ZNZ kuachiwa mambo ya nje, uraia na ushuru?

Hakuna kisiwa masikini duniani.

Zanzibar kwanza, upuuzi baadae.
 
Kwani kwa sasa Bara inafaidika na nini na kanchi kadogo ka Zanzibar ka watu 1 milioni?

Wewe huwezi jua wabara tunafaidika na nini,lkn walioko kwenye system ndio wanaojua ila hawasemi wanakaa kimya na ndio maana hd hatutaki kuwaachia wazenji,lipo tunalofaidika nalo.
 
Tushazoea porojo za wakoloni weusi, watu laki saba eti waungane na milioni 45 mlimpata kweli karume Enzi za ujinga wake hivi akilini kweli inaingia hivi nyie wadanganyika mkiskia tunkula urojo ndo wajinga kiasi hicho tena mlivo waajabu hata utaifa wenu hamuujui kama mbili zimeshinda then eti tuunde moja kama mnataka muungano undenu wenu wa Tanzania na Tanganyika mtapata seikali moja ila ZANZIBAR UTAIFA KWANZA hiyo ndio fahari yetu na hili jiti mmejitia wenyewe mwaka huu serikali tatau kuelekea malaka kamili ZANZIBAR KWANZA
 
tushasema hatutaki moja, mbili, wala tatu ni mamlaka kamili jitieni uziwi ila mwaka huu ndo mwisho wa ukoloni wa Tanganyika ZANZIBAR KWANZA porojo hazitutishi na kwa kuanzia hizo tatu zinatosha coz hicho ndo kifo cha ccm mlinzi wa muungano
 
Back
Top Bottom