Je, Zanzibar inasonga mbele au nyuma?

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Nov 30, 2008
1,518
22
Ninapotafakari mahali Zanzibar ilipo kwa sasa kimaendeleo;
Najiuliza kama inasonga mbele au inasonga nyuma, au imedumaa?

kati ya mambo machache, Kumbukumbu zinasema kuwa:-
- Zanzinbar ilikuwa ya kwanza kuwasha umeme katika mitaa yake kulinganisha na mji wowote katika Afrika Mashariki.Hii ilifanyika mwaka 1904.

Ninyi mwaonaje wana JF mlioko hapa Afrika ya mashariki?

Angalia hizi Videos:

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=FCyPll_PQb0"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=XfJ0e6UoYUs"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=Lo8OCdl-Tbw"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=g2Ij2_sJ8BM"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=FRR5hAns4ng"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=LyQy6zRNd7Q"]YouTube - Broadcast Yourself.[/ame]
 
According to Wikipedia, Zanzibar was the first region in Africa to introduce color television in 1973, but it currently ranks low among African countries due to poor services offered and lack of modern production tools as well as experienced staff.
Najiuliza kama inasonga mbele au inasonga nyuma ...
Ila hapo sidhani kuna usahihi katika terminology ya 'kusonga nyuma'
 
Ninapotafakari mahali Zanzibar ilipo kwa sasa kimaendeleo;
Najiuliza kama inasonga mbele au inasonga nyuma, au imedumaa?

kati ya mambo machache, Kumbukumbu zinasema kuwa:-
- Zanzinbar ilikuwa ya kwanza kuwasha umeme katika mitaa yake kulinganisha na mji wowote katika Afrika Mashariki.Hii ilifanyika mwaka 1904.

Ninyi mwaonaje wana JF mlioko hapa Afrika ya mashariki?
Mbona hueleweki hapa. Kusonga nyuma- kulikoni? Au una maana ya kurudi nyuma. Kuwa muwazi. Tutachangia baadaye.
 
Si watu wanadai Visiwani inapaa kama Singapore?? Do we have hark working Zanzibaris as Singaporeans??

Au ni maneno na siasa tu?
 
Jamaa kuchwa kutwa wanapigana/kuzozana wataendelea saa ngapi?
Acha kuongopa wewe? Hebu nenda katembelee ufike Kikwajuni, upite Miembeni uishie Daraja bovu , na bahati yako ukute kuna beni au taarb inapigwa pahala -uone wanagombana au wanaburudika na kurushana roho tu.
 
Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano. Sasa ni vipi sehemu ya mwili hiwe zaidi ya nyingine!?

Maendeleo ya Bara ndio Maendeleo ya Visiwani.
 
Ni aibu Zanzibar hata Mchele wanaagiza bara wakati ardhi nzuri iko Visiwani kibao!

Sasa hapo nani wa kulaumiwa? Hivi Bara wanaagiza nini toka Zanzibar???
 
Wakati wa mkoloni Zanzibar ilikua inapiga hatumi kumi kumi za kimaendeleo ndio tunapata hayo mambo ya TV za rangi, Umeme n.k.

Wakati wa Karume na Nyerere Zanzibar imepiga hatuma mia mia nyuma mpaka tulipofikia. Kama tumekua katika safari ndefu basi wale waliopo nyuma wametupita na hatuoni haya ukingo wao. Hakuna haja kubabaishana, yote haya ni dhulma iliyofanya na mwalimu nyerere na karume kwa kutuletea umasikini. Na wanafunzi wao ndio wanayaendeleza sasa.

Kila umri unaporefuka, mali za Zanzibar zinazidi kuteketezwa na Tanganyika. Leo imekua tunakusanyishwa kodi, na zinahamishwa kwenda Tanganyika kuwanufaisha wao. Hii ni dhulma ambayo tunaweza kuilinganisha na Hitla. Ili upite uadilifu, ni lazima Tanganyika waache tabia yao hii chafu. Shukran

Wazanzibar kudai utu wetu na haki zetu sio ukhalifu. Mwenye ez Mungu ibariki Zanzibar Amin
 
Mbona hueleweki hapa. Kusonga nyuma- kulikoni? Au una maana ya kurudi nyuma. Kuwa muwazi. Tutachangia baadaye.

PAKACHA NA WENGINE,
Maneno KUSONGA NYUMA yasiwape taabu.
Maana ya neno SONGA kwa Kiingereza ni MOVE.
Hivyo nlimaanisha "MOVE BACKWARDS".
Unajua tena upungufu wa kiswahili.

Tuendelee na mada wakuu.

Kuhusu ZANZIBAR, Watu wengi walidhani kuwa, Muungano wake na TANGANYIKA ungezidisha maendeleo kwa kasi.
Nadhani walwaza vibaya.
Au siyo wakuu?
 
Zanzibar ilikuwa na maendeleo wakati karafuu ina soko duniani baada ya soko la karafuu kushuka na uchumi wa Zanzibar ukashuka. Zanzibar ni nchi yenye rasilimali chache kulinganisha na bara kuanzia population na hata natural resources. Uchumi wa Zanzibar una sukumwa na utalii tu kwa sasa. Sasa jamani nchi kama U.A.E. ambao ni matajiri wa kufaa wana panua wigo wa soko lao leo hii Wazanzibar wali tegemea kuendelea na karafuu na utalii tu? Kama uchumi ulikuwa una tegemea karafuu na utali basi it was bound to fail Muungano or not. Blame it on a lack of vision kama Zanzibar imeshindwa kudevelop other industries na kama kweli Tanganyika ndiyo tatizo blame it on Zanzibar leaders who lack the courage. Ni rahisi sana kulaumu wengine hata kama unajua ufumbuzi ni nini. Complaining never got anyone anywhere na hata kwenye maisha ni vigumu kukutana na mtu yoyote mlalamishi mwenye maendeleo.
 
zanzibar ingeangalia visiwa vingine vimefanyaje kupata maendeleo. Waangalie sehemu kama Monte Carlo, nk. Tafuta njia za kuvutia watalii, kama tax free zone, legalising gambling, nk
 
Zanzibar imeanza kurudi nyuma mara tu! Baada kuanza kutawaliwa na TANGANYIKA
 
Back
Top Bottom