Je, Zanzibar inasonga mbele au nyuma?

Astaghfirullah. hivi ni nani wanaotegemea zaidi kutoka (sadaka, ruzuku au hisani za Nje) Ni Zanzibar kweli? na siyo Tanganyika ilivyofanya mbinu na hila za kuchukua kilicho-kingi kupindukia kati ya kile Tunachogaiwa Tanzania?

Mkuu sasa kiswahili kinakupiga chenga ,hapo naeleza kuwa Tanganyika wao humwagiwa mapesa kutoka katika bajeti za mataifa hayo kila mwaka na kama watasita basi ndio itakuwa mwisho wa jeuri zote na kujitapa kwao.
 
JF Member Kinyikani,

Umenukuu "Maoni ya Mhe. Juma Duni na jinsi anavyoelezea Tanganyika ilivyofilisi Zanzibar. Katika utafiti wa Juma Duni kuna mambo ambayo mimi binafsi natajwa kwa vile nilihusika nikiwa Permanent Secretary katika Wizara ya Fedha na baadaye Gavana mwanzilishi wa Benki Kuu (BoT). Naona ni vizuri nifafanue kadri ninavyokumbuka na ninavyoelewa mpangilio wa kulipia huduma za serikali.

Kwanza mimi sisomi JF mara kwa mara, na sikuona post hii ya 14 Juni 2009 mapema. Nasikitika kwamba maelezo yangu yanatolewa kwa kuchelewa.

Pili, yahusuyo Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki (East African Currency Board) na muundo wake miaka ya 1961 mpaka 1965, pamoja na juhudi za wanahisa kujaribu kuubadilisha ili kukidhi mahitaji ya nchi huru, ni sahihi. Jacob Namfua akiwa Permanent Secretary wa Wizara ya Fedha (sio Waziri) baada ya Makubaliano ya Muungano ya 26 Aprili,1964, aliandika barua June 1964 kuelezea kwamba Zanzibar ingeendelea kuwa na haki zake kama member kwa vile "banking na currency" wakati huo hayakuwa ni mambo ya Muungano katika makubaliano.

Tatu, nilichukua nafasi ya J.D. Namfua Septemba 1964 na nakumbuka mkutano wa kwanza wa Bodi niliohudhuria, Bwana mmoja akiitwa ?Shah, aliwakilisha Wizara ya Fedha ya SMZ. John de Loynes, Mwingereza aliyekuwa ameteuliwa na Bank of England kusaidia kuendesha EACB, alikuwa virtually ndiye General Manager, na hakuandika ile barua ya Septemba 1964 kwa Secretary wa Board kutokana na msukumo wa Dunstan Omari, Mtanganyika aliyekuwa Chairman. Huu ulikuwa ni msimamo wake de Loynes binafsi, akitaka Tanzania, Kenya na Uganda wawe sawa baada ya Muungano wa 26 April 1964. Omari na mimi tulitaka sehemu ya Zanzibar iendelee kutambuliwa.

Kwa bahati mbaya, mwaka 1965 mikwaruzano baina ya viongozi wa Tanzania na Kenya iliongezeka, kwa vile matumaini ya East African Federation yalitoweka; na hapo ndipo tukaanza kuzungumza kuvunja EACB. Katika bajeti ya Juni 1965 ilitangazwa rasmi kwamba kila nchi itakuwa na sarafu yake na Benki Kuu yake. Baada ya hapo ndipo tulipoanza kutayarisha muswada wa Sheria ya BoT. Kabla ya Muswada huu kujadiliwa na Bunge ilikuwa ni lazima Interim Constitution ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ibadilishwe ili kuingiza "Banking, Currency na Exchange Control" kama ni mambo ya Muungano.

Hapa ndipo Profesa Shivji anapotosha kwa kusema Makubaliano hayakuwa na Banking. Ni kweli mwanzoni hayakuwa na banking na currency, lakini wakubwa walikubali kurekebesha.

Naamini kwamba Mwalimu Julius Nyerere na Makamu wake wa Kwanza, Abeid Amani Karume, walikuwa wakiaminiana sana na makubaliano ya kuongeza mambo haya katika Orodha ya Mambo ya Muungano yalionekana ni dhahiri (obvious in the circumstances). To imply that Mwalimu played a trick to have Abeid Amani Karume sign the Assent to make the Amendment a legal document is to be unfair to both parties. Mwalimu alikuwa nje, na Bill for BoT Act could not be debated without the Costitution first being amended.

Baada ya Currency na Banking kuwa Union Matters na Sheria ya BoT kupitishwa, niliteuliwa Gavana na kutokana na uzoefu na majukumu yangu mapya niliwakilisha Tanzania katika EACB mpaka ilipokuwa "dissolved".

Ni kweli kwamba distribution ya dividends na residual assets za EACB were based on Tanganyika, Kenya na Uganda being equal na Zanzibar kupokea takriban 3.5% zaidi. Na hili liliendelea kusisitizwa, hata kama ni mimi nilikuwa nawakilisha Tanzania.

Lakini nifafanue pia jambo moja ambalo linaonekana halijaelezwa; nalo ni kwamba Serikali zozote zina treat hizo dividends ni mapato yake katika bajeti. Kwa hiyo fedha zilizotokana na dividends za EACB (na baadaye BoT) zililipwa kwa Serikali ya Muungano kama ndiyo yenye hisa. Na itambulike kwamba, licha ya EACB kutoa mchango katika kuanzisha BoT na benki kuu nyingine za Kenya na Uganda, Serikali ya Muungano ilijazia ili mtaji utosheleze kabla ya BoT kuanza shughuli.

Mimi nafikiri pia ni vizuri itambulike kwamba Serikali ya Muungano inalipia mambo yote ya Muungano ambayo yanafanyika Zanzibar au yanahusisha Wazanzibari. Kwa mfano Jeshi la Ulinzi, Jeshi la Polisi, Idara za Uhamiaji na Magereza, Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mabalozi yetu nje. Hata Ofisi za Rais na Makamu wake zinahusu Zanzibar kwa kiasi. Haya yote hayawezi kutolewa kwa Zanzibar bure. Kwa hiyo kama fedha zitokanazo na faida ya EACB na BoT zinatumiwa na Serikali ya Muungano, sehemu ambayo ina chanzo cha Zanzibar kuchangia hisa za BoT ni kidogo sana.

Ni matumaini yangu kwamba maelezo haya yatasaidia kuondoa manung'uniko ya Wazanzibari.

Edwin Mtei
 
Last edited:
Ni faraja kubwa kupata maelezo toka kwa mhusika mkuu kama Mzee Mtei. Mie nadhani Mzee Mtei atalisaidia sana taifa kama ataandika memoirs zake (au tayari ameshaziandika?)

Mzee Mtei, Mzee Rashid Kawawa, Mzee Aboud Jumbe na Rais Ali Hassan Mwinyi ni watu ambao ni muhimu waliachie taifa kumbukumbu binafsi kwa kuandika memoirs zao. Tuwasihi wafanye hivyo.
 
Kwa haya nayoyaona sasa...kujaribu kuona kila tatizo linaletwa na watu wa nje ya Zanzibar ikiwemo Bara, na kurupuka kwa viongozi na kutoa matamshi bila kujari athari zake, napata hisia jamaa wameanza kufanya reverse motion.Itawagharimu somewhere along the way unless wakue na kubadilika
 
JF Member Kinyikani,

Umenukuu "Maoni ya Mhe. Juma Duni na jinsi anavyoelezea Tanganyika ilivyofilisi Zanzibar. Katika utafiti wa Juma Duni kuna mambo ambayo mimi binafsi natajwa kwa vile nilihusika nikiwa Permanent Secretary katika Wizara ya Fedha na baadaye Gavana mwanzilishi wa Benki Kuu (BoT). Naona ni vizuri nifafanue kadri ninavyokumbuka na ninavyoelewa mpangilio wa kulipia huduma za serikali.

Kwanza mimi sisomi JF mara kwa mara, na sikuona post hii ya 14 Juni 2009 mapema. Nasikitika kwamba maelezo yangu yanatolewa kwa kuchelewa.

Pili, yahusuyo Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki (East African Currency Board) na muundo wake miaka ya 1961 mpaka 1965, pamoja na juhudi za wanahisa kujaribu kuubadilisha ili kukidhi mahitaji ya nchi huru, ni sahihi. Jacob Namfua akiwa Permanent Secretary wa Wizara ya Fedha (sio Waziri) baada ya Makubaliano ya Muungano ya 26 Aprili,1964, aliandika barua June 1964 kuelezea kwamba Zanzibar ingeendelea kuwa na haki zake kama member kwa vile "banking na currency" wakati huo hayakuwa ni mambo ya Muungano katika makubaliano.

Tatu, nilichukua nafasi ya J.D. Namfua Septemba 1964 na nakumbuka mkutano wa kwanza wa Bodi niliohudhuria, Bwana mmoja akiitwa ?Shah, aliwakilisha Wizara ya Fedha ya SMZ. John de Loynes, Mwingereza aliyekuwa ameteuliwa na Bank of England kusaidia kuendesha EACB, alikuwa virtually ndiye General Manager, na hakuandika ile barua ya Septemba 1964 kwa Secretary wa Board kutokana na msukumo wa Dunstan Omari, Mtanganyika aliyekuwa Chairman. Huu ulikuwa ni msimamo wake de Loynes binafsi, akitaka Tanzania, Kenya na Uganda wawe sawa baada ya Muungano wa 26 April 1964. Omari na mimi tulitaka sehemu ya Zanzibar iendelee kutambuliwa.

Kwa bahati mbaya, mwaka 1965 mikwaruzano baina ya viongozi wa Tanzania na Kenya iliongezeka, kwa vile matumaini ya East African Federation yalitoweka; na hapo ndipo tukaanza kuzungumza kuvunja EACB. Katika bajeti ya Juni 1965 ilitangazwa rasmi kwamba kila nchi itakuwa na sarafu yake na Benki Kuu yake. Baada ya hapo ndipo tulipoanza kutayarisha muswada wa Sheria ya BoT. Kabla ya Muswada huu kujadiliwa na Bunge ilikuwa ni lazima Interim Constitution ya Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ibadilishwe ili kuingiza "Banking, Currency na Exchange Control" kama ni mambo ya Muungano.

Hapa ndipo Profesa Shivji anapotosha kwa kusema Makubaliano hayakuwa na Banking. Ni kweli mwanzoni hayakuwa na banking na currency, lakini wakubwa walikubali kurekebesha.

Naamini kwamba Mwalimu Julius Nyerere na Makamu wake wa Kwanza, Abeid Amani Karume, walikuwa wakiaminiana sana na makubaliano ya kuongeza mambo haya katika Orodha ya Mambo ya Muungano yalionekana ni dhahiri (obvious in the circumstances). To imply that Mwalimu played a trick to have Abeid Amani Karume sign the Assent to make the Amendment a legal document is to be unfair to both parties. Mwalimu alikuwa nje, na Bill for BoT Act could not be debated without the Costitution first being amended.

Baada ya Currency na Banking kuwa Union Matters na Sheria ya BoT kupitishwa, niliteuliwa Gavana na kutokana na uzoefu na majukumu yangu mapya niliwakilisha Tanzania katika EACB mpaka ilipokuwa "dissolved".

Ni kweli kwamba distribution ya dividends na residual assets za EACB were based on Tanganyika, Kenya na Uganda being equal na Zanzibar kupokea takriban 3.5% zaidi. Na hili liliendelea kusisitizwa, hata kama ni mimi nilikuwa nawakilisha Tanzania.

Lakini nifafanue pia jambo moja ambalo linaonekana halijaelezwa; nalo ni kwamba Serikali zozote zina treat hizo dividends ni mapato yake katika bajeti. Kwa hiyo fedha zilizotokana na dividends za EACB (na baadaye BoT) zililipwa kwa Serikali ya Muungano kama ndiyo yenye hisa. Na itambulike kwamba, licha ya EACB kutoa mchango katika kuanzisha BoT na benki kuu nyingine za Kenya na Uganda, Serikali ya Muungano ilijazia ili mtaji utosheleze kabla ya BoT kuanza shughuli.

Mimi nafikiri pia ni vizuri itambulike kwamba Serikali ya Muungano inalipia mambo yote ya Muungano ambayo yanafanyika Zanzibar au yanahusisha Wazanzibari. Kwa mfano Jeshi la Ulinzi, Jeshi la Polisi, Idara za Uhamiaji na Magereza, Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mabalozi yetu nje. Hata Ofisi za Rais na Makamu wake zinahusu Zanzibar kwa kiasi. Haya yote hayawezi kutolewa kwa Zanzibar bure. Kwa hiyo kama fedha zitokanazo na faida ya EACB na BoT zinatumiwa na Serikali ya Muungano, sehemu ambayo ina chanzo cha Zanzibar kuchangia hisa za BoT ni kidogo sana.

Ni matumaini yangu kwamba maelezo haya yatasaidia kuondoa manung'uniko ya Wazanzibari.

Edwin Mtei
Kumbe na wewe ni mmoja kati ya walioimaliza znz,umejitahidi kujitete lkn umeharibu.. Historia itakuhukumu ipo siku kwa ubaya wako. Nakuheshimu lkn umechemsha.
 
Wakati mwengine hujuiuliza uamuzi gani huchukuliwa kuchagua viongozi, Poor management, bad politics na chuki binafsi. Viongozi ndio wanayoirudisha nyuma Zanzibar. Waziri anaishutumu Marekani kwa kuwakataza raia wake wasiende pemba , kuwa wao ndio wanaozusha zogo huko, tafadhali nani asiyejua kuwa mnawanyanyasa raia wa pemba. Muwanyime maendeleo kisha muwanyang'anye haki zao za kura.
 
Back
Top Bottom