Je yule alimvuta Kikwete miguu jukwaani Mwanza alikuwa na maono gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je yule alimvuta Kikwete miguu jukwaani Mwanza alikuwa na maono gani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by commonmwananchi, Sep 27, 2012.

 1. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,180
  Likes Received: 487
  Trophy Points: 180
  wana JF,takriban miaka saba imetimia tangu tukio la mtu mmoja alipomvamia ghafla Mh JK,katika uwanja wa CCM kirumba kutoka jukwaani alipokuwa akihutubia umati wa wana CCM katika kapeni ambazo hatimae zilimuingiza ikulu.

  Yule bwana alidhibitiwa na vyombo vya usalama na baadae kuhukumiwa kifungo na alitumikia na sasa nina imani kuwa ni raia huru ingawa sina uhakika na uwepo wake.

  My take hapa ni kwamba yule bwana hakuweza kutafutwa walau na chombo chochote cha habari ili walau aweze kuulizwa na kusema nini ilikuwa dhamira yake na je ni maono gani alikuwa ameyaona kwa mtazamo wake labfda wengi tungeweza kuwa na uhakika.tofauti tulivyoaminishwa kuwa alikuwa na matatizo ya akili.
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2012
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  yule bwana siyo walipiga mpaka akajifia?!
   
 3. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  naskia alishakufa yule, ila aliona KJ ni janga na kuwa ataiua Tz ndo maana alitaka wale wachawi waliokuwa wanampa ndumba kwa kisingizio cha kumtawaza chifu wa wasukuma washindwe
   
 4. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  hapo kwenye red unaongelea mhimili wa nne wa dola mkuu.
  wajuzi wa mambo wanadai kuwa huu mhimili umetetereka sana na huenda ndio unachangia kwa kiasi kikubwa sana matatizo tuliyonayo. Na kwa sababu uwepo wake hautegemei ridhaa ya wananchi ndio sababu ya Watanzania wengi hawahoji uwepo au kutokuwepo kwake.
  Kwa kifupi HATUNA WAANDISHI!

   
 5. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kama polisi walimuua Mwangosi asiye na kosa unategemea huyo aliyemvuta miguu muungu wao wamfanye nini? Tanzania ni nchi ya ajabu. Ukiiba kuku unahukumiwa kifo tena cha pale pale lakini ukiiba mabilioni unaongezewa ulaji na sifa ya tajiri, mfanyabiashara maarufu na hata mheshimiwa.
   
 6. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,180
  Likes Received: 487
  Trophy Points: 180
  Mimi nakubaliana na wewe maana hawa waandishi wetu wengi hata waki mhoji mkubwa yeyote maswali .hawulizi yale wananchi tunayotarajia kuwasikia viongozi wetu wakiulizwa na badala yake wanawauliza maswali ambayo kwa uwazi kabisa ni kama ya kupangwa.ili kuwafagilia hao viongozi.....mifano hai ni Semunyu na dakika 45 zake pale ITV
   
 7. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,180
  Likes Received: 487
  Trophy Points: 180
  Inawezekana mkuu!
   
 8. K

  Kolero JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2012
  Joined: Apr 11, 2010
  Messages: 493
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mkuu mawazo yako ni sawa, lakini naomba nitofautiane nawe katika hitimisho lako, WAANDISHI TUNAO, ila labda tuangalie mazingira wanayofanyia kazi na vyombo vya habari wanavyofanyia kazi. Niliwahi kuchunguza na nikaona, tatizo si waandishi, bali wamiliki wa vyombo vya habari na mfumo wa habari nchini. Wamiliki wana sera za habari katika kwenye vyombo vyao, kumbe unaweza ukawa umebobea katika tasnia ya habari lakini ukakatishwa tamaa na sera za chombo cha habari unachofanyia kazi, ukalazimika wakati mwingine kukubaliana nazo na ukaacha hata yale ambayo yamoo katika fani yako, mfumo wa habari nao unachangia katika hili hasa katika wahusika wanaotoa habari, na urahisi wa kumpata mtu na kumhoji. Sidhani kama ilikuwa rahisi sana baada ya tukio lile kupata urahisi wa kumhoji yule jamaa, na mbaya zaidi kama wahusika wangekuwa tayari kukupa ushirikiano wa kupata habari unazotaka juu ya tukio lile na hata hatima ya yule mtu. Bado mfumo haujaenzi mhimili huu wa nne katika nchi, ni wachcahe tu wanajua kuwa huu ni mhimili mhimu, wengine wanaona kama ni wa kawaida. Kumbe Mkuu, bado kuna mengi ambayo Waandish wa habari wanakumbana nayo, kama si utayari wao wa kututumikia kwa karamu zao, hata haya machache wasingeyafuatilia.
  Kuhusu kuchangia matatizo tuliyo nayo sababau mbili hizo ndizo zinahusika, WAMILIKI NA MFUMO, bado naona waandishi hawahusiki moja kwa moja bali wanalazimishwa kuhusika.
   
 9. share

  share JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 22, 2008
  Messages: 2,294
  Likes Received: 2,278
  Trophy Points: 280
  Yule kijana alikuwa na akili timamu, siyo kichaa. Jela hawafungwi vichaa. Unapimwa akili kwanza kujiridhisha kabla ya kufunguliwa kesi iwapo tendo ulilolifanya si la kawaida. Haiyumkini yule kijana kufungwa hali alitenda hivyo akiwa kichaa! Ikidhihirika kuwa alifungwa akiwa kichaa basi huo ni uovo mwingine wa jeshi la Polisi na Muhimili wa Mahakama. Nadhani yule kijana alikuwa na nia njema tu! Alimuona jamaa anakaribia kudondoka kama kawaida yake. Alikimbia kumnusuru kwa kumshika mguu!
   
 10. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  utafikiri (kwa nchi zenye waandishi) kuwa wanakuwa wameshakutana masaa 48 kabla na wanakubaliana kuwa utaniuliza maswali haya alafu anampangia muda. Naona pamoja na kutaarifiana huko lakini bado hawa jamaa wanashindwa kujibu na hivyo inabidi awafuate nyumbani kwake. Yaani nia aibu kwa kifupi!
  Wataalamu wanatoa ushahidi kuwa pale mhimili huu uliposhindwa kazi zake nchi zilitumbukia either kwenye umasikini wa kupindukia au machafuko.

   
 11. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #11
  Sep 27, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Hivi kweli mtu wa historia kama yule anaweza kupoteza habari kiasi hiki? Huku JF hakuna hata jirani yake? Nina hakika JF kisima cha habari atatokea wa kutujuza alipo huyu shujaa maana kwa kitendo kile mhhhh hatari sana huyu.
   
 12. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #12
  Sep 27, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  umeeleza mkuu lakini jaribu kukumbuka haya:
  Mkulima kazi yake ni kulima
  Dereva kazi yake ni kuendesha gari
  Hakimu kazi yake ni kutoa tafsiri ya sheria
  Daktari kazi yake ni kutibu nk nk nk
  Mwandishi wa habari kazi yake ni kudadisi habari hence
  Chombo cha habari kazi yake ni kutangaza.
  Haya uliyoyaorodhesa hayako kwenye viapo vya hii fani kama ilivyo kwa viapo vya fani nyingine. Na hivi viapo vyote vinahusiana na imani za watu na kama unaona huwezi kuhimili fani husika huna haja ya kula kiapo, kitendo cha kula kiapo (kushika Kitabu Kitakatifu) then ukakikiuka ndicho cha cha laana zote tunazoziona katika nchi hii.
  Huwezi kumshawishi mtu yeyote kuwa mshahara wa hakimu ni mdogo na mazingira ya kazi ni magumu hivyo ni lazima afuate matekwa ya mshitakiwa au mwajiri bila kujali kama wako ndani au nje ya sheria, cha muhimu wametoa pesa (za ziada) kwa hakimu!

  Kwa vyovyote vile ilipasa waandishi walioshuhudia hilo tukio na kutuhabarisha mwishowe waje na hitimisho (where, when, how, who, what etc) bila woga nasi tungelijua huyu bwana alikusudia nini lakini they just reported on where and when only ambacho inawaondolea uhalali wa kuwa waandishi kwa maana mengine waliyajua lakini kimya!

   
 13. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #13
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,798
  Likes Received: 36,830
  Trophy Points: 280
  Aisee yule jamaa alikua atuokoe na hili janga.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 14. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #14
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,180
  Likes Received: 487
  Trophy Points: 180
  Umesema kweli mkuu,tatizo lingine ukiondoa njaa za wahariri wa hivi vyombo vyetu vya habari.lakini pia kuna uingiliwaji wa utendaji wao ,ukiacha wamiliki lakini pia hata saa nyingine na mhimili mwingine wa dola ambao na maarufu kwa sasa kama uhasama wa taifa.

  Pia sheria kandamizi zilizopitwa na wakati za ufungiaji kiholelea wa vyombo vvya habari kama tulivyoona hivi karibini kwa mwanahalisi,

  Halafu watala wameanza mtindo mbaya kabisa wa kuvuruga mhimili wa nne kwa kuwahonga baadhi vyeo kadhaa serikalini jambo ambalo linawafanya na hawa wengine kuwa na tamaa ya madaraka na hivyo kuanza kujipendekeza kwa watawala badala ya kusimamia maadili ya kazi zao
   
 15. K

  Kolero JF-Expert Member

  #15
  Sep 27, 2012
  Joined: Apr 11, 2010
  Messages: 493
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Uko sawa Mkuu, unachosema ni kukosekana kwa 'follow-up' ya story hiyo kama sehemu ya stori za kitafiti, nadhani umefanya vizuri kukumbushia hilo kama sehemu ya jamii, na wahusika nina uhakika wataanza kulifuatilia si tu kwa maslahi ya taifa bali hata taaluma ya uandishi wa habari. Pia nakupongeza kwa hilo maana kiukweli habari inapofuatilia mpaka tujue mwisho wake inapendeza, kama wanavyofanya katika habari za kesi mbalimbali mahakamani. Nilipotoa maelezo sikumaanisha kuwa Waandishi wavunje kiapo chao cha kutumikia jamii kwanza kwa kalamu zao bali nilijaribu kukueleza vikwazo ambavyo waandishi wa habari wanakumbana navyo ikiwa ni pamoja na hizo 'media house policy' mitazamo binafsi ya wamiliki wa vyombo hivyo, urasimu wa utoaji habari toka kwa watoa habari na wakati mwingine na jamii kwa ujumla nikiwepo mimi na wewe. Kuna matukio mengi sana ambayo kama ushirikiano ungekuwepo hakika habari juu ya matukio hayo tungezipata na hapo kazi za Waandishi wa habari tungeifurahia pengine sawa kama vile kazi ya madaktari na walimu. Kazi ya uandishi wa habari inategemea vitu vingi lakini kwanza taaluma, pili kujitoa kutumikia jamii, tatu, jamii kuwa tayari kutoa ushirikiano katika kazi hiyo muhimu, sera ya habari kutoa ushirikiano kwa waandishi katika kufanikisha kupatikana kwa habari na utoaji wake. Maana Mwandishi anaweza pata habari na akaamua kuifuatilia ili aweze kujiridhisha na kulidhisha maadili ya taaluma,hatua hiii inahitaji ushirikiano sana, mfano katika hili ulilotoa la huyo mtu, ushirikiano toka kwa ndugu, viongozi wa kijiji, polisi, magereza na vitu kama hivyo. Pamoja na hayo, ukishapata habari hiyo, bado Mmiliki wa chombo cha habari anala kusema pia kulingana na maslahi ya habari hiyo ingawa kimsingi Mwandishi ameshaifanyia kazi zote hizo, na hapo ndipo nilipomaanisha kuwa kuna mlolongo wa matukio na vikwazo. Kumbe WAANDISHI TUNAO, WANAFANYA KAZI KWA KIWANGO CHAO, LAKINI BADO KUNA MATATIZO KIBAO YA KIKAZI NA KIMAZINGIRA YANAYOKWAMISHA KAZI ZAO. Mimi na wewe tunaweza tukawa sehemu ya vikwazo wanavyokumbana navyo wana habari kwa kutowapa ushirikiano pale unapohitajika.
   
 16. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #16
  Sep 27, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mkuu umenena...
   
 17. HUGO CHAVES

  HUGO CHAVES JF-Expert Member

  #17
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 1,852
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Watakuja wenye kumfahamu vizuri
   
 18. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #18
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  sijui aliishia wapi, poor him!
   
 19. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  hakuna kitu cha hatari nacha aibu kama mtafiti(mtafuta habari) anaposingizia kuwa study population haikumpa ushirikiano, stupid and poor journalistss wa tanzania hutoa habari ya mtu aliyewapa bahasha, priority yao siyo jamii inataka nini bali wao(yeye) atapata nini imediately, shame. Ndoo maana walaji hatupati habari za maana , utafikiri hawalipwi mishahara na media houses zao.
   
 20. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #20
  Sep 28, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  pamoja na wachangiaji wengine wananyoosha kidole kwa media houses.
  Hivi tujiulize, hwa akina Jenerali Ulimwengu, Said Kubenea, Vick Ntetema unadhani ni nini kiliwasukuma kuanzisha 'media houses' zao wenyewe? Kwa maana kama kweli ni jasiri na mkweli huwezi kuendelea kuwaaminisha wasomaji/watazamaji/wasikilizaji kuwa "1+1=11" kwa maana mwenye chombo ndivo anataka, utabisha kuwa hiki ndio chanzo cha huu umasikini na ujinga tunaouona!?
  Leo Kubenea, Ulimwengu nk wanaweza kuwa na kasoro zao lakini kila mmoja akifuata huo mtazamo mwishowe tutatoka. Huko kulikoendelea nao wana itikadi zao za uandishi lakini si katika mambo yanayohusiana na maslahi ya taifa. Hii inakosti wengine lakini historia yao inakuwa na heshima zaidi ya waliobaki hai, chukulia mfano wa Stanislaus Katabaro (Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi) na Loliondo 'yake', atasomwa more positively katika historia japo hatujui watoto wake wanaishije lakini nao wataona fahari huko mbeleni kuwa na baba jasiri badala ya baba 'mpokea bahasha'.
  tafakari swali hili la kijinga: ...unadhani mwandishi mwenye kujiamini na upeo anaweza kwenda kuajiriwa pale 'kijitonyama'??
  Kwa hiyo badala ya kusema suala la huyu jamaa linahusu system ni bora kuwaeleza alioshuhudia 'akimdondosha' mkulu badala ya kimya
   
Loading...