Je yawezekana?

The dirt paka

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
371
66
Hivi inawezekana mtu (mume/mke) kuishi peke yake bila mwenzi na akawa na furaha mpaka kufa kwake?
 
Hivi inawezekana mtu (mume/mke) kuishi peke yake bila mwenzi na akawa na furaha mpaka kufa kwake?
Mh! Mkuu hujafunguka sana ila Kimaisha yaani kazi,fedha,utajiri n.k yawezekan, lakini yote haya bila familia ni sufuri.Kama ni wewe jitahidi uwe na mwenza ili ui-enjoy! Samahani lakini
 
Ndiyo injwezekana
source and refference ni KAKA YANGU AMBAYE SASA NI PAROKO(Padre)
 
napenda nikujibu kwa kunukuu kisa fulani cha mwanafalsafa wa kale aitwae SOCRET:

SOCRET, alikuwa mlevi sana wa pombe kiasi kilichopelekea kupata kipigo kikali kutoka kwa mkewe hasa aliporudi nyumbani akiwa amelewa chakali. siku moja rafiki yake ambaye ni jirani yake akaamua kumuuliza socret na mazungumzo yao yalikuwa hivi;

rafiki yake: kwa nini mkeo anakupiga hivyo ukiwa umelewa, JE KUNA HAJA YA KUOA?
SOCRET: kuoa ama kutokuoa yote ni majibu sahihi ila UTAJUTA MWENYEWE

naishia hapo mkuu hivyo tafakali chukua hatua!!!!!!!!
 
Ndiyo injwezekana
source and refference ni KAKA YANGU AMBAYE SASA NI PAROKO(Padre)

1.Unajuaje kama ana furaha ya kweli? 2. Na, je, unajuaje kama hafanyi mapenzi? Uparoko ni ajira tu kwa experience yangu.
 
Hajaulizia kuhusu kufanya ngono! Anaongelea connection kati ya kuoa na kuwa na furaha hata atakapokufa! Padri anaweza kuwa na furaha bila kuoa na bila kufanya ngono pia! Kuoanga ni kuchagua

Nijuavyo mimi ajira inatoa malipo yaliyokubaliana je analipwa ngapi?
 
Otis nieleze kivipi? Mmmh..! Na Kumbe kuna furaha ya kweli, ni vipi viashiria vya furaha hiyo jamani?
 
wenye ndoa wanalalama kila siku shida coz cheating imeshika kas, km hilo sio shida oa au olewa
 
Kuoa au kutokuoa wala kupata au kukosa chochote hakumpi binadamu furaha. Ndiyo maana wote wanaodhani kuwa furaha hupatikana kwenye vitu huishia kwenye kuchanganyikiwa.
 
Huyo sio mume/mke tena. kua mume/mke maana yake una mwenzio.
Hao wamesha rudi kua single tena.
 
Hajaulizia kuhusu kufanya ngono! Anaongelea connection kati ya kuoa na kuwa na furaha hata atakapokufa! Padri anaweza kuwa na furaha bila kuoa na bila kufanya ngono pia! Kuoanga ni kuchagua
Kwa hapo sina lingine, nimeelewa. Lakini si unajua kuwa kuna ndoa nyingine ambapo mwenzi hana furaha kwa sababu ama ya kunyimwa ngono au kutotoshelezwa kimapenzi?
 
Nijuavyo mimi ajira inatoa malipo yaliyokubaliana je analipwa ngapi?

Malipo ya ajira sio lazima pesa. Ukipewa chakula, nguo, gari, simu, ukafanyiwa kazi yote za nyumbani, utahitaji fedha za nini?
 
Mi naona inawezeakana sana.ht miye na mpango wa kutokuoa nahisi ndio ntakua nafuraha kuliko m2 aliyeoa .........ukiwa na mitoto yako miwili ya kiume hapo ndani ya kukusumbua!! kuoa ya nn.
 
Mi naona inawezeakana sana.ht miye na mpango wa kutokuoa nahisi ndio ntakua nafuraha kuliko m2 aliyeoa .........ukiwa na mitoto yako miwili ya kiume hapo ndani ya kukusumbua!! kuoa ya nn.

Popo unamiasira sana! Kumbe single ni better na ndoa chanzo cha matatizo na hasa stress...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom