Je! yawezekana CCM wanamuandaa Mwigulu Nchembe kugombea urais 2015?

Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,536
2,000
Waswahili husema siri ya mtungi aijuaye kata!
Kwa muda sasa nimekuwa nikimsoma sana kiongozi huyu akinadi siasa za CCM na hakika amekuwa tofauti sana na CCM tuloizoea. Kwa mwenye kufikiri na kutafakari sera za huyu bwana zimekuwa majibu makubwa ya kero za wananchi na haijatokea hata mara moja akapingwa ama kupigwa vita na wana CCM wenyewe japo sii mrengo wao.

Kwa muda wa mwaka kama sii miezi, kiongozi huyu ametoka ngazi ya chini kabisa ya umaarufu na kuwa chimbuko la kizazi kipya ndani ya chama hiki cha CCM ambacho kimekuwa kikipoteza umaarufu wake kwa vijana nchini na kwa haraka sana hasa. Na kwa kuzingatia kauli mbiu ya JK kuwataka vijana wamchague kiongozi kijana, hizi habari za kusisitiza rais kijana na kadhalika inanipa picha kubwa zaidi ya kwamba huyu kijana anaandaliwa kwa njia moja ama nyingine kuwa mgombea wa mwaka 2015 kwa sababu ndiye pekee ktk jukwaa la CCM amewavuta na ataendelea kuwavuta wadanganyika wengi..

Nasema wadanganyika kwa sababu, toka mwaka 1984 tulipoingia Ubepari, siasa zetu zimekuwa hadith za alinacha na haziwezekaniki kama vile tembo kupita ktk tundu la sindano wanapotumia neno hili - Maisha bora kwa kila mwananchi!.

Nyie wanabodi wenzangu mnafikiri kweli huyu kiongozi anayasema haya kwa dhati na kwamba kweli CCM ipo tayari kubadilika kutokana na siasa za Kiongozi Mwigulu Mchemba!
 
Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,903
2,000
Ccm ina hazina ya wagombea urais. Wapo wazee kwa vijana. Mtajiju nyie mnaotegemea vikongwe wawili tu
 
sosoliso

JF-Expert Member
May 6, 2009
8,523
2,000
Mkuu unaposema ccm wanamuandaa Mwigulu unamaanisha ccm gani hao..? Maana ninachokiona kuna wagombea wengi mule ambao wameonyesha nia.. Na ukichukulia ccm ina wenyewe wachache ambao ndo king makers na ambao huyu Mwigulu hayumo kabisa kwenye hesabu zao..!
 
kizaizai

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
4,064
2,000
Katika CCM hakutatokea mgombea uraisi aliyeaminiwa na Watanzania kama JK,baada ya kuingia Ikulu ni majanga kwa kwenda mbele, MUNGU tu ndie anaeturehemu na kuilinda Tanzania.
 
Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
18,947
2,000
Katika CCM hakutatokea mgombea uraisi aliyeaminiwa na Watanzania kama JK,baada ya kuingia Ikulu ni majanga kwa kwenda mbele, MUNGU tu ndie anaeturehemu na kuilinda Tanzania.
Majqnga ndiyo nini au kujenga barabara kila sehemu ndiyo majanga.
 
The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
13,089
2,000
Kikwete kisha amua kuendelea na rafiki yake Lowasa ................................ wengine ni wasindikizaji tu!!
 
Faridi

JF-Expert Member
Apr 2, 2008
672
250
Mwigulu hafai kabisa kuongoza hii nchi kwanza kutokana na wizara yake kuhusika na wizi huu wa pesa za Escrow wao kama wizara ya fedha ilikua wasiruhusu pesa hizi zisitoke katika akaunti ya Escrow, lakini kwasababu inaonyesha walihusika kwenye mgao wamefumba macho pesa zitolewe na ukitilia maanani pia kauli alioitoa bungeni ilikua dhaifu saana kama kiongozi kuagizia pesa zilizoibiwa au kupewa watu bila kufuata taratibu zilipiwe kodi mara moja badala ya kuagiza zirudishwe au zichunguzwe uhalali wake na kama kuna sheria imevunjwa washitakiwe wahusika washitakiwe mara moja.Kwa agizo hilo alionyesha kuwa na nia ya kusafisha pesa chafu.
 
Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,648
2,000
Nami nina mawazo kama yako kuhusu huyu Mwigulu. Naona hivi sasa anajinadi sana na kukinadi chama na baadhi ya vijana katika mitandao ya kijamaa wanamuona kama Sokoine mpya.
 
bantulile

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
1,571
2,000
Sema unampigia upatu usizunguke. Kwa taarifa yako CCM hamwandai mtu bali mtu hujiandaa mwenyewe.
Waswahili husema siri ya mtungi aijuaye kata!
Kwa muda sasa nimekuwa nikimsoma sana kiongozi huyu akinadi siasa za CCM na hakika amekuwa tofauti sana na CCM tuloizoea. Kwa mwenye kufikiri na kutafakari sera za huyu bwana zimekuwa majibu makubwa ya kero za wananchi na haijatokea hata mara moja akapingwa ama kupigwa vita na wana CCM wenyewe japo sii mrengo wao.

Kwa muda wa mwaka kama sii miezi, kiongozi huyu ametoka ngazi ya chini kabisa ya umaarufu na kuwa chimbuko la kizazi kipya ndani ya chama hiki cha CCM ambacho kimekuwa kikipoteza umaarufu wake kwa vijana nchini na kwa haraka sana hasa. Na kwa kuzingatia kauli mbiu ya JK kuwataka vijana wamchague kiongozi kijana, hizi habari za kusisitiza rais kijana na kadhalika inanipa picha kubwa zaidi ya kwamba huyu kijana anaandaliwa kwa njia moja ama nyingine kuwa mgombea wa mwaka 2015 kwa sababu ndiye pekee ktk jukwaa la CCM amewavuta na ataendelea kuwavuta wadanganyika wengi..

Nasema wadanganyika kwa sababu, toka mwaka 1984 tulipoingia Ubepari, siasa zetu zimekuwa hadith za alinacha na haziwezekaniki kama vile tembo kupita ktk tundu la sindano wanapotumia neno hili - Maisha bora kwa kila mwananchi!.

Nyie wanabodi wenzangu mnafikiri kweli huyu kiongozi anayasema haya kwa dhati na kwamba kweli CCM ipo tayari kubadilika kutokana na siasa za Kiongozi Mwigulu Mchemba!
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
14,341
2,000
Waswahili husema siri ya mtungi aijuaye kata!
Nyie wanabodi wenzangu mnafikiri kweli huyu kiongozi anayasema haya kwa dhati na kwamba kweli CCM ipo tayari kubadilika kutokana na siasa za Kiongozi Mwigulu Mchemba!

Hili swali angeuliza mzee wa kisomo cha ngumbalu kutoka kijiji cha ndani kabisa angalau ningeelewa lakini mtu kama wewe kuja na swali kama hili imenifanya niamini kuwa kweli watanzania akili zetu ni kama za nyumbu. Hujui gilba za wanasiasa wa kiafrika au tatizo ni nini! Huyu Mwingulu amefanya kitu gani hata kiwe kidogo kama punje ya haradani kinachokufanya uone kabadilikka? Usanii anaouonyesha kwenye maneno bila vitendo au ni nini! Tafadhali msituletee tena balaa nyingine... hii tuliyoibeba ya Kikwete, itachukuwa miongo mingi kuondoa uvundo wake...
 
Bramo

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
12,141
2,000
Waswahili husema siri ya mtungi aijuaye kata!
Kwa muda sasa nimekuwa nikimsoma sana kiongozi huyu akinadi siasa za CCM na hakika amekuwa tofauti sana na CCM tuloizoea. Kwa mwenye kufikiri na kutafakari sera za huyu bwana zimekuwa majibu makubwa ya kero za wananchi na haijatokea hata mara moja akapingwa ama kupigwa vita na wana CCM wenyewe japo sii mrengo wao.

Kwa muda wa mwaka kama sii miezi, kiongozi huyu ametoka ngazi ya chini kabisa ya umaarufu na kuwa chimbuko la kizazi kipya ndani ya chama hiki cha CCM ambacho kimekuwa kikipoteza umaarufu wake kwa vijana nchini na kwa haraka sana hasa. Na kwa kuzingatia kauli mbiu ya JK kuwataka vijana wamchague kiongozi kijana, hizi habari za kusisitiza rais kijana na kadhalika inanipa picha kubwa zaidi ya kwamba huyu kijana anaandaliwa kwa njia moja ama nyingine kuwa mgombea wa mwaka 2015 kwa sababu ndiye pekee ktk jukwaa la CCM amewavuta na ataendelea kuwavuta wadanganyika wengi..

Nasema wadanganyika kwa sababu, toka mwaka 1984 tulipoingia Ubepari, siasa zetu zimekuwa hadith za alinacha na haziwezekaniki kama vile tembo kupita ktk tundu la sindano wanapotumia neno hili - Maisha bora kwa kila mwananchi!.

Nyie wanabodi wenzangu mnafikiri kweli huyu kiongozi anayasema haya kwa dhati na kwamba kweli CCM ipo tayari kubadilika kutokana na siasa za Kiongozi Mwigulu Mchemba!

Tokea kuwa Gaid mlipuaji Mabomu na Msukaji wa kesi na kubambikia watu Mpaka kupaizwa juu kabisa kudhaniwa kuwa Raia namba moja wa Tanzania.
Hii ndio CCM,Taasisi ya U Rais imenajisisiwa vya Kutosha
 
Bramo

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
12,141
2,000
Nami nina mawazo kama yako kuhusu huyu Mwigulu. Naona hivi sasa anajinadi sana na kukinadi chama na baadhi ya vijana katika mitandao ya kijamaa wanamuona kama Sokoine mpya.

Kwa nchi zinazoheshimu utu na utawala bora,jamaa alipaswa kuwa anatumikia Kifungo cha Kunyongwa ama Maisha jela,lakin kwetu anafikiriwa kabisa kuwa atakuwa Rais,na watu wengine wameenda Mbali zaidi na kumuita Sokoine kama sio yeye anayejiita hivyo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom