Waswahili husema siri ya mtungi aijuaye kata!
Kwa muda sasa nimekuwa nikimsoma sana kiongozi huyu akinadi siasa za CCM na hakika amekuwa tofauti sana na CCM tuloizoea. Kwa mwenye kufikiri na kutafakari sera za huyu bwana zimekuwa majibu makubwa ya kero za wananchi na haijatokea hata mara moja akapingwa ama kupigwa vita na wana CCM wenyewe japo sii mrengo wao.
Kwa muda wa mwaka kama sii miezi, kiongozi huyu ametoka ngazi ya chini kabisa ya umaarufu na kuwa chimbuko la kizazi kipya ndani ya chama hiki cha CCM ambacho kimekuwa kikipoteza umaarufu wake kwa vijana nchini na kwa haraka sana hasa. Na kwa kuzingatia kauli mbiu ya JK kuwataka vijana wamchague kiongozi kijana, hizi habari za kusisitiza rais kijana na kadhalika inanipa picha kubwa zaidi ya kwamba huyu kijana anaandaliwa kwa njia moja ama nyingine kuwa mgombea wa mwaka 2015 kwa sababu ndiye pekee ktk jukwaa la CCM amewavuta na ataendelea kuwavuta wadanganyika wengi..
Nasema wadanganyika kwa sababu, toka mwaka 1984 tulipoingia Ubepari, siasa zetu zimekuwa hadith za alinacha na haziwezekaniki kama vile tembo kupita ktk tundu la sindano wanapotumia neno hili - Maisha bora kwa kila mwananchi!.
Nyie wanabodi wenzangu mnafikiri kweli huyu kiongozi anayasema haya kwa dhati na kwamba kweli CCM ipo tayari kubadilika kutokana na siasa za Kiongozi Mwigulu Mchemba!