Je, yaliyotokea Kenya, Congo, na Uganda ni kushindwa kwa ubepari?


Mkandara:

Mtu yoyote atakayeleta suala la amani ni lazima aangalie historia yetu. Machafuko makubwa yalikuwa wakati wa majimaji na baada ya hapo nchi imekuwa ya amani.

Tunachojua ni kuwa amani siku zote inakuja na maendeleo ya kijamii. Ukiona watu wana amani kwa muda mrefu na maendeleo hayapatikani ni lazima kutakuwa na kitu kinachowakwamisha.
 

Sasa huo ndio ufafanuzi wako au unaamua kupindisha kile ambacho umekiandika?

Nakuwekea hapa chini jinsi ulivyoandika:



Swali langu

Tufafanulie ni kitu gani kilichokuwepo? Au wewe binafsi ni mchango gani umetoa kulinganisha na wa Mwalimu Nyerere (RIP)kuhusiana na amani iliyopo Tanzania.

Kwenye amani unayoiongelea labda kama unataka kusema Kiswahili kuwa lugha ya taifa ni ujamaa? Kwa sababu hiyo ndio nyenzo kubwa ambayo ilikuwa ya kwanza kuweza kuwaunganisha wabongo kabla ya jambo lingine lolote na hapo credit ni kwa Julius au tukupe wewe? Ndio nikauliza where was your contribution if any? Na hili sio jambo dogo kama unavyotaka members hapa wakubaliane na wewe, lingekuwa jambo dogo Uganda, Kenya na baadhi ya nchi zingine wasingeanza kujifunza Kiswahili kwa nguvu zote.

Tukumbuke credit hutolewa kwa wale ambao ni exceptional labda uniambie u-exceptional wako wewe katika kulipa kodi etc. ...................which I believe that's normal to the majority of the citizens.

Mshikamano ambao Julius aliufanya huwezi hata kulinganisha na nchi yoyote Afrika sasa kama hapo hutaki kutoa credit wakati wengi leo hii duniani wanatoa credit napata mashaka na kusudio lako.

Mkandara

You are missing the point, angalia swala lililozuka hapo juu, Kulinganisha Tanzania na Malawi au Zambia ni matusi kwa sababu hizi ni nchi tatu tofauti unalinganisha kitu gani? Hoja yangu ukisoma hapo juu utaelewa ni kuhusu ufafanuzi wa swali na wala sio kupindisha hoja. Kenya, Malawi, Congo former Zaire, Somalia walikuwa wanajulikana kwa kutumiwa na western countries hadi leo hii hizi ni nchi ambazo zimekuwa protrayed vizuri kuliko Tanzania kwa muda mrefu na hii sio siri. Wakati wa awamu ya kwanza hatukuwa na MAFISADI kama tulivyonao leo.
 


Kasome shule kwanza, bishara ya utumwa na pembe za ndovu ilisambaza sana kiswahili kuliko mipango uliyoletwa baada ya uhuru. Babu yangu alisoma shule ya mjerumani alisoma kwa kiswahili. Shule za mwingereza zilifundisha kiswahili mpaka darasa la nne.

Na historia inaonyesha kuwa uhuru ulipatikana mapema kwa sababu ya kiswahili. wakati wa harakati za uhuru lugha iliyotumika ni kiswahili.

Na mchango wa Nyerere katika kiswahili ni kufanya kitumike kuanzia darasa la tano mpaka la saba. Kitendo ambacho mwenyewe alikubali kuwa alifanya makosa ambayo yameshusha kiwango cha elimu.

Kama kuna mchango aliofanya ambao unaona ni exceptional hupo lakini sio katika amani au kiswahili. Hivi ni vitu kiongozi yoyote hatakiwi kuchukua credit yoyote (period and end of story).

Na kuhusu contribution, msimamo wangu huko palepale. Kwa umri nilionao na nafasi yangu ya kijamii, kufanya kazi, kulipa kodi na kutofanya uhalifu ni mchango mkubwa kwa taifa na najivunia kwa kile nachofanya kwa taifa langu.
 
 
Masanja,Dua,Rev.Kishoka,FMES,Bin Maryam,

..Mimi nadhani hii amani yetu inatokana na ukweli kwamba Watanzania hatuna hamu na uchu wa maendeleo.

..Inaelekea Watanzania tumeridhika sana na hali ya umasikini uliotuzunguka.

..Vilevile Watanzania tumeshindwa kuunganisha umasikini wetu na viongozi tunaowachagua.

..Watawala wetu wamevuruga nchi na uchumi lakini hatuishi kuwaenzi na kuwatukuza.
 
Ni akili ndogo tuu ya waafrika ndio maana tumefeli kila kitu na umaskini unatuandama tangu enzi na enzi,hatuwezi kujisaidia tumekalia kusafiri kwenda kuomba misaada ndio policy ya maendeleo then tunategemea tutaenda mbele,kama sio akili ndogo ni nini? wananchi wanachagua CCM kwa kishindo huku wakijua hao ndio mwanzo wa rushwa kama sio akili ndogo ni nini? rushwa ya billion 133 kwa nchi maskini kama yetu na wanaohusika bado wako kazini kama sio akili ndogo ni nini? mimi naamini hatuna akili ndio maana ni maskini,tungekuwa timamu huko vichwani tusingekula rushwa wala kuchagua wala rushwa wanaotutengenezea mifumo mibovu kwenye jamii yetu...naamini siku tukipata viongozi wenye akili tutaendelea sana.
 

Kuna Mwarabu mmoja kutoka Tunisia aliandika kitabu kabla ya karne 12. Na kuna watu wanaosoma uchumi wa jamii wanadai kuwa huyu jamaa ni kama baba wa uchumi wa duniani.

Katika kitabu chake anazungumzia masuala ya utumwa. Anasema jamii nyingi zimepitia utumwa. Kilichomshangaza ni kuwa jamii zingine zilitumia utumwa kupanga ngazi kati jamii na wangine kuwa watawala. Lakini kwa watu weusi kuridhika kwa utumwa ni kilikuwa ni kitu cha kawaida. Nikipata muda naweza kukupa reference ya kitabu chenyewe.

Amani ya Tanzania ni kuridhika. Chumvi inakosekana na bado wananchi wanaandamana kumpongeza rais. Huo ni utumwa.
 

Mkuu Joka,

Heshima mbele, ni kweli kabisaa hii mkuu, very strong argument mkuu.
 
Jokakuu,
Safi sana mzee wangu nakubaliana nawe mia kwa mia.

Dua,
Jamani nimesema kitu gani hapa cha kuonyesha nimerukia na kubadilisha hoja?...
Ama siruhusiwi kuchangia mada hii?...
Nalichosema mimi kinahusu mchango wa Mwalimu JKN ktk kuleta Amani na Utulivu, na kama unakumbuka huyu ndiye kipenzi changu na hata siku moja sintamweka nyuma. Lakini ktk swala hili ati kuwa yeye ndiye sababu ya kuwepo amani nchini hapo ndipo nilipotoa mawazo yangu kulingana na reality kwani hii amani tunaizungumzia leo kwa kulinganisha na nchi nyinginezo...Laa sivyo sijui ni kipimo gani kingetumika kuonyesha kuwa Tanzania tuna amani na Utulivu hali kila nchi ina amani.
Kama unakumbuka vizuri Mwalimu alipokuwa akifanya propaganda za Uhuru alikaribishwa kila mkoa na wenyeji wake Na haikuwa kazi kubwa sana kwa chama Tanu kujipatia wanachama bila kutumia nguvu....dalili ya kuwa amani ilikuwepo kabla ya hata Uhuru wetu. Nikatoa pia mfano wa Utumwa ambapo tulikusanywa kama ndama na hakuna historia ya kuonyesha resistance ya Utumwa Tanzania nzima kama sio baadhi ya chiefdom kwa kutaka gharama kubwa zaidi. In fact watumwa tuliwakusanya sisi wenyewe kina Tip Tippu (wanyapala) ati wafanya biashara na walivaa vilemba kujifananisha kama waarabu. Na hakuna historia ya kuonyesha Tip Tippu alikuwa wanted ktk maisha yake -ndio Utulivu wetu huo ulikoanzia. Tukaja tawaliwa na Mjarumani, Tunamwona Mkwawa tu aliyejaribu kupigana nao lakini wengine woote walimpokea na mnara katuachia wa Bismini ambao hadi leo ni alama kubwa ya jiji la Dar. Muingereza yale yale tena basi alikuwa bado akiendeleza biashara ya Utumwa wakati Zenj wameisha acha na kupiga marufuku...
Ndugu yangu Amani na Utulivu ni kilema kwetu ambacho kimekuwa jadi ya Mdanganyika. Kwa hali hiyo ndio maana sikubaliani na habari za kuwa Nyerere ndiye mwanzilishi wa Amani na Utulivu kwani hii ni sifa mbaya kwangu na sidhani kama inamfaa marehemu mwalimu JK Nyerere. Uzembe wa kuabudu binadamu wengine ni kimila chetu wenyewe ambacho nafikiri kimetokana na kutokuwa na ELIMU, elimu ya kuweza kutofautisha utumwa na ubwana kwani hadi leo hii tunavyozungumza heshima hupewa mwenye kitu hata kama ni jambazi na wapo wanaokaribia kumwabudu tajiri....Hii ndiyo hali halisi ya Mdanganyika ambayo hatuwezi kuiepuka sote.
Sasa, inapofikia Ufisadi kuwa ni neema yote hii imetokana na uzembe wetu wenyewe, haya Huyo Balali amnatafutwa leo hali ni serikali ilomwacha kwenda pata matibabu US...Jeetu Patel na wengine wote waliohusika na scandal zote nchini wanafika Ikulu yetu bila hodi na mitaani hupishwa viti wao wapate kukaa kwanza....
Mjomba amni usiamini tunapozungumzia Amani haina Mjamaa wala Pebari isipokuwa uongozi wa mtu. Kama Nyerere ndiye aliyeleta amani Tanzania basi hata Kaunda na Banda ndio walileta amani nchi hizo kwani nao wapo kundi moja nasi ktk kipimo cha amani, yet tunaongoza ktk umaskini....Umaskini hauchagui Mjamaa wala Bebari kama vile Amani na utulivu haina rangi.
 

Masanja,

Wakati wa Mwalimu, watu walikuwa waoga kuiba na hasa kijinga kama ilivyo sasa hivi watu hawana aibu wala heshima kwa mkuu wao wa kazi.

Suala si kukosekana kwa uhuru wa maoni na habari, au kukosa pa kuongelea.

Nyerere alikuwa akipenda kuwapa watu nafasi ya pile mpaka ya nne wajifunze kutokana na makosa. kuanguka kwa mashirika mengi haukutokana na Wizi au Ufisadi, bali ni mipango mibovu ya utekelezaji na udhaifu katika ufanisi.

La zaidi, mashirika haya yaliishia kuwa "welfare" organs, kutoa ajira kwa kila mtu, kutoa huduma bure za afya, nyumba, usafiri, chakula hata uniforms!

Matumizi yalizidi mapato kutokana na msukumo wa kujenga "middle class" kutumia mishahara na si ubunifu wa uzalishaji na kuruhusu ajira binafsi, kuendeleza biashara na huduma na kukuza kilimo kutoka kilimo cha heka moja na kuwa kilimo cha kibiashara!

Mwalimu alileta plan nzuri, tulimsubiri aingie kazini na afanye kila kitu yeye mwenyewe huku tukiandamana kumtukana mkoloni na kumsifu mwenyekiti huku tukikimbia umande kukwepa kwenda kazini kuwa hodari wa kazi na wabinifu.

Kaondoka Nyerere tumepata uhuru wa kuongea, kujiajiri binafsi na hata kuwa na miradi ya pembeni, lakini hali zetu ni zile zile, goi goi, wazembe, wavivu, wabangaizaji na sasa tamaa imetugeuza mafisadi!
 

Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu....
 
Mzalendohalisi:

I honestly respect every word of what you said::::Ni hitimisho la Msingi la kilakitu.....Eee Mwenyenzi Mungu Ibariki Tanzania
 
Bob Mkandara,

Ukweli utajidhihirisha pale wale wenye nia ya kweli watakapoanza kujitolea bila masharti. Katika miaka yangu 10 ya mitandao hii ya Watanzania, nimejifunza mengi na kuona kwa dhati ni jinsi gani tlivyofanana na CCM na Serikali yetu.!

Rev.

That is very important indeed!!!"kujitolea bila masharti" Basicaly uongozi wa kweli haulipwi. Kufikiria vinginevyo is the root of all problems! Kama wananchi wanjitegemeea kwa jasho lao, then viogozi wajitegemee bila kuwatumia jasho la wananchi kabisa..Hakuna njia ya kweli ya kufanya hivyo..Bila kuufanya uogozi usiwe unalipwa!!! Uogozi usiwe ni capital ya aina yeyote..I am telling you this looks upside down but ..ndio jibu!!

One day i will be able to explain this much more better.

But for now, kama pakawa na sheria inayoliwezesha hilo kutekelezeka..Ni viogozi wangapi wangebakiA kazini? Ni wabunge wangapi wangebaki kwnye nyadhifa? Huwezi kuamini hao ambao wangebaki hata ungewalipa wangekuwa honest and to the people. But beliave me one day science will come up with confrmation of waht i am saying.."UNOGOZI HAULIPIKI" hasa unavyozidi kuwa wa ngazi za juu!!!Its a free thing ni almost kitu cha kujitolea tu!!!
 
1. According to UN office on drugs and crimes -nimeona hii data ktk Mkutano unaendelea Bali hii leo!

2. Je do we need AID? Tuzibe kapu linalovuja- tunaibiwa 10 times ya misaada! Sasa eti tunajivunia Tz tumeweza kuvutia misaada na JK anajipiga kifua!

Siku tukisema misaada basi- ndo tutaanza kusonga mbele na kuendelea!

The amount of money extorted and stolen each year from developing countries is over 10 times the approximately $100bn in foreign assistance being provided by all governments and civil organizations in the world.
 
Why capitalism triumphs in the West, but failed everywhere!!!? By prof. Hernando De Soto.

"A must read"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…