Je, Waziri Mkuu anajitenga na Serikali?

Je, Waziri Mkuu anajitenga na Serikali?

Kila nchi hupitia Changamoto tofauti kwa Nyakati Tofauti, Katika Nchi yetu kuliwahi kuwa na Gumzo Masuala Ya Tozo, Tukaja Suala La Umeme na Maji na Sasa Suala la Upandaji wa Mafuta Kidunia.

Katika Masuala Yote haya Waziri Mkuu Hukuwahi Kutoka mbele na Kusemea au Kutetea Masuala haya Hadharani Kuonekana yupo pamoja na Serikali Inayoendeshwa na Rais Samia. Amekuwa akimlaghai Rais Kwa Kuonekana anafanya vikao vya ndani Kutatua Matatizo ila Ukweli Hukuwahi Kutoka nje na Kusemea Serikali na Hatua anazochukua kama kiongozi wa Mawaziri katika kila sakata linalotokea nchini.

Wizara ambayo ipo chini yako ndio kinara wa kuwa na Kiwango cha Chini cha utendaji, Kuna Suala la mwenge lipo kimya husemi kitu (na Taarifa juu ya Hujuma za Mbio za Mwenge unazozitengeneza wakuu wa wilaya na mikoa ambayo tayari Mwenge umekwisha kupita wanafahamu jinsi hali ilivyo) lakini pia kuna suala la Sensa nalo upo kimya hili ni jukumu lako chini ya sera na uratibu.

AMEZOA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA YA KUENDESHWA.
Katika suala ambalo linanipa ukakasi ni kwamba vikao unavyofanya kumuonesha Rais Unamsaidia ni vya uongo, umezoea kuendeshwa kama ulivyokua ukiendeshwa awamu iliopita lakini huku Unatoenesha wazi huna uwezo wa kifikra wala kuwa kiongozi wa Mawaziri na hizi Hujuma kwa Rais.

Katika awamu ya tano ya uwaziri mkuu wake, mh majaliwa, kiukweli (kwa mtazamo wangu), alikuwa kama mtu mwenye wasiwasi mno asiyejiamni sana. Alizoea kufokewa na kutishiwa 'nitapiga mpaka shangazi zako' hakuwa ni mtu wa kujiamini n.k.

Awamu hii ya sita mambo yamebadilika mambo mengi huanzia bungeni kwanini majaliwa anashindwa kuyadhibiti kuanzia huko ni mtu wa maigizo anayetaka kuonekana ana mikono misafi anataka kuonekana serikali inatengeneza matatizo na kuyatatua. Hii si awamu ya ndiyo mzee ni awamu ya kuonyesha uwezo.

ANAYEISHI KINAFKI
Uislamu unaelekeza mnafiki ana sura tatu kwanza akihaidi atimizi, muongo tatu ameficha uzuri kwenye ubaya kufanya kihiyana. Sura aliyoitengeneza na kutoa matamko kwenye mambo madogo ni sura ya unafki mbona hatumuoni akizungumzia masuala ya sensa, mbona hazungumzi masuala ya mwenge, haonekani kwenye kuzungumzia bei ya mafuta serikali imesimama wapi. Waswahili wanasema kama umeamua kuuza utumbo usiogope nzi. Majaliwa anataka kujitengeneza kuwa yeye ni msafi siasa za janja janja kama za RUTO.

MTENDAJI MKUU WA SHUGHULI ZA SERIKALI NI NANI KAMA SI WAZIRI MKUU?.
Wakati huu ambapo tupo kwenye kupanda kwa bei za mafuta na nishati nyinginezo waziri mkuu yupo kimya na lawama zote ni kwa Waziri wa nishati,

Matatizo ya kukosekana kwa maji lawama ni kwa Rais na waziri wa Maji, Yakifungiwa magazeti, vifurushi vikipanda lawama ni kwa Rais na waziri wa habari. Waziri Mkuu anasimamia jambo gani? badala yake yupo kushanga kupanda kwa bei ya mchele ambao unalimwa hapa nchini kwamba hajui athari ni suala la kupanda kwa bei ya mafuta ndiyo kuna athiri uzalishaji hivyo bei kupanda?

Ukitazama mfumo huo aliojiwekea anataka kuonekana msafi kuna ajenda nyuma ya pazia na genge lake. Kama Huna Uwezo Jiuzulu kama Una Ndoto za Urais Jiuzulu, Usiharibu nchi kwa kutaka Rais Aonekane Mbaya na Wewe Mzuri kwa Kuweka Mikono yako Safi.

Tunafahamu kuna baadhi ya wabunge Livingstone Lusinde (kibajaji), Luhaga Mpina Kuanza kupishana kwa kauli ndani ya chama ni mgogoro inayotengenezwa na genge la Waziri mkuu. mtifuano wa hoja zinazo kinzana katika siasa ya CCM. Katika awamu ya tano hatukuwahi kusikia kauli za kushangaza kutoka kwa wabunge kutupia lawama Mawaziri siku zote maswali ya kitaifa bungeni hujibiwa na Waziri mkuu ambaye ni mtendaji mkuu wa Serikali.

WAVURUGAJI WA AWAMU YA SITA
Wamepanga kuleta mtikisiko wa siasa za kistaarabu zilizoanza kutamalaki na kwa kuanza kuchokonoa na kuharibu taswira ya mwenyekiti. Mawaziri wanatukanwa na wabunge kwa kashfa za hovyo Waziri Mkuu hatoi uelekezi wa ajenda kama nchi tunasimama wapi?

Mh, Rais tunakuomba muangalie Waziri wako mkuu kwa jicho la tatu kama anakutosha.
Ha ha ha mmeanza kumsagia meno majaliwa wa watu. Ndo majizi mlivyo, maana jamaa anapiga kazi hata kuliko sterling wenu.. Bora yeye angalau anatoka na kujitutumua kwa kupiga mikwara hata kwenye Ile miradi na taasisi mlizo kunwa vizuri na majizi. Nonsense
 
Angekuwa msafi asingechukua hela kwa Boss Nasri wa GBP Kwa taarifa yenu OilCom, State Oil Na Lake Oil wameungana na kuhonga bilioni 3 walete shehena ya mafuta na wote wana vimeo vya kodi TRA. TRA kuweni makini msiseme hamkuwa na taarifa.
 
Juzikati PM aliongea redioni kimamlaka akikemea upigaji wa kutisha wa MSD tena kwa kutoa takwimu za bei halisi na pia akavamia na kukemea uzembe katika ujenzi wa meli ya hapa kazi tu sasa sijui tunataka afanye kazi ngapi? haya sio majungu jamani au udini at work?
 
Kila nchi hupitia Changamoto tofauti kwa Nyakati Tofauti, Katika Nchi yetu kuliwahi kuwa na Gumzo Masuala Ya Tozo, Tukaja Suala La Umeme na Maji na Sasa Suala la Upandaji wa Mafuta Kidunia.

Katika Masuala Yote haya Waziri Mkuu Hukuwahi Kutoka mbele na Kusemea au Kutetea Masuala haya Hadharani Kuonekana yupo pamoja na Serikali Inayoendeshwa na Rais Samia. Amekuwa akimlaghai Rais Kwa Kuonekana anafanya vikao vya ndani Kutatua Matatizo ila Ukweli Hukuwahi Kutoka nje na Kusemea Serikali na Hatua anazochukua kama kiongozi wa Mawaziri katika kila sakata linalotokea nchini.

Wizara ambayo ipo chini yako ndio kinara wa kuwa na Kiwango cha Chini cha utendaji, Kuna Suala la mwenge lipo kimya husemi kitu (na Taarifa juu ya Hujuma za Mbio za Mwenge unazozitengeneza wakuu wa wilaya na mikoa ambayo tayari Mwenge umekwisha kupita wanafahamu jinsi hali ilivyo) lakini pia kuna suala la Sensa nalo upo kimya hili ni jukumu lako chini ya sera na uratibu.

AMEZOA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA YA KUENDESHWA.
Katika suala ambalo linanipa ukakasi ni kwamba vikao unavyofanya kumuonesha Rais Unamsaidia ni vya uongo, umezoea kuendeshwa kama ulivyokua ukiendeshwa awamu iliopita lakini huku Unatoenesha wazi huna uwezo wa kifikra wala kuwa kiongozi wa Mawaziri na hizi Hujuma kwa Rais.

Katika awamu ya tano ya uwaziri mkuu wake, mh majaliwa, kiukweli (kwa mtazamo wangu), alikuwa kama mtu mwenye wasiwasi mno asiyejiamni sana. Alizoea kufokewa na kutishiwa 'nitapiga mpaka shangazi zako' hakuwa ni mtu wa kujiamini n.k.

Awamu hii ya sita mambo yamebadilika mambo mengi huanzia bungeni kwanini majaliwa anashindwa kuyadhibiti kuanzia huko ni mtu wa maigizo anayetaka kuonekana ana mikono misafi anataka kuonekana serikali inatengeneza matatizo na kuyatatua. Hii si awamu ya ndiyo mzee ni awamu ya kuonyesha uwezo.

ANAYEISHI KINAFKI
Uislamu unaelekeza mnafiki ana sura tatu kwanza akihaidi atimizi, muongo tatu ameficha uzuri kwenye ubaya kufanya kihiyana. Sura aliyoitengeneza na kutoa matamko kwenye mambo madogo ni sura ya unafki mbona hatumuoni akizungumzia masuala ya sensa, mbona hazungumzi masuala ya mwenge, haonekani kwenye kuzungumzia bei ya mafuta serikali imesimama wapi. Waswahili wanasema kama umeamua kuuza utumbo usiogope nzi. Majaliwa anataka kujitengeneza kuwa yeye ni msafi siasa za janja janja kama za RUTO.

MTENDAJI MKUU WA SHUGHULI ZA SERIKALI NI NANI KAMA SI WAZIRI MKUU?.
Wakati huu ambapo tupo kwenye kupanda kwa bei za mafuta na nishati nyinginezo waziri mkuu yupo kimya na lawama zote ni kwa Waziri wa nishati,

Matatizo ya kukosekana kwa maji lawama ni kwa Rais na waziri wa Maji, Yakifungiwa magazeti, vifurushi vikipanda lawama ni kwa Rais na waziri wa habari. Waziri Mkuu anasimamia jambo gani? badala yake yupo kushanga kupanda kwa bei ya mchele ambao unalimwa hapa nchini kwamba hajui athari ni suala la kupanda kwa bei ya mafuta ndiyo kuna athiri uzalishaji hivyo bei kupanda?

Ukitazama mfumo huo aliojiwekea anataka kuonekana msafi kuna ajenda nyuma ya pazia na genge lake. Kama Huna Uwezo Jiuzulu kama Una Ndoto za Urais Jiuzulu, Usiharibu nchi kwa kutaka Rais Aonekane Mbaya na Wewe Mzuri kwa Kuweka Mikono yako Safi.

Tunafahamu kuna baadhi ya wabunge Livingstone Lusinde (kibajaji), Luhaga Mpina Kuanza kupishana kwa kauli ndani ya chama ni mgogoro inayotengenezwa na genge la Waziri mkuu. mtifuano wa hoja zinazo kinzana katika siasa ya CCM. Katika awamu ya tano hatukuwahi kusikia kauli za kushangaza kutoka kwa wabunge kutupia lawama Mawaziri siku zote maswali ya kitaifa bungeni hujibiwa na Waziri mkuu ambaye ni mtendaji mkuu wa Serikali.

WAVURUGAJI WA AWAMU YA SITA
Wamepanga kuleta mtikisiko wa siasa za kistaarabu zilizoanza kutamalaki na kwa kuanza kuchokonoa na kuharibu taswira ya mwenyekiti. Mawaziri wanatukanwa na wabunge kwa kashfa za hovyo Waziri Mkuu hatoi uelekezi wa ajenda kama nchi tunasimama wapi?

Mh, Rais tunakuomba muangalie Waziri wako mkuu kwa jicho la tatu kama anakutosha.
Kama ulizoea kuona ccm ikiwa na sauti moja basi umepotea, hii si mara ya kwanza kukutana na bunge la chama kimoja lakini kuna upinzani ndani yake. Tumewahi kuwa na G55 kama ulikuwa bado unanyonya basi jifunze kupitia kina Luhaga Mpina akili kubwa. G55 nusura hoja yake ipelekwe kwenye referundum, thanks to Mwl, alipojitosa kama yeye kuoka jahazi. Tulia upate madini
 
Mi naona anataka tu kumaliza miaka 10 kama sumaye maana wengi waliopita hio nafasi hakumaliza miaka 10
 
Juzikati PM aliongea redioni kimamlaka akikemea upigaji wa kutisha wa MSD tena kwa kutoa takwimu za bei halisi na pia akavamia na kukemea uzembe katika ujenzi wa meli ya hapa kazi tu sasa sijui tunataka afanye kazi ngapi? haya sio majungu jamani au udini at work?

Kwani huu upigaji si wa kipindi cha kambale ahahahahaha alikuwa wapi yeye mpaka CAG akague. Mahoka
 
Tumerudi nyuma miaka 50 kwa kuwa wengi tunawazia kuwafitinisha wenzetu.

Tunatakiwa tufanye kazi kwa bidii ili tufikie mafanikio na malengo.Lakin kaz ni fitina,majungu,uongo Kama huu ulioleta.Hata Rais naye badala ya kufanya kazi ,amekalia kumsengenya na kumparura JPM.

JPM ameshalala kwenye pumziko la milele.Hata umseme ,hasikii .Na machawa wa mama naona mpo kazini.Lakini atafeli tu.
Chief Hangaya na chawa wake wanajua kuwa wanapomsema vibaya Magufuli implicitly wanamsema pia makamu wake Mpango? Pengine ndio maana wanamtenga!
 
mhuu wewe kweli ni bibititi 1.......Huo muda ungechukua jembe kwenda kulima ungekuwa umemaliza ekari. Mwache PM wa watanzania
PM wa kina Luhaga mpina, Kibajaji Livingstone, Mwenyekiti wa Wazazi Taifa Mndolwa, Bashiru na wajinga wengine wa umoja party.
 
Chief Hangaya na chawa wake wanajua kuwa wanapomsema vibaya Magufuli implicitly wanamsema pia makamu wake Mpango? Pengine ndio maana wanamtenga!

Ukali wa magufuli na sabaya akaumiza mamilioni ya watanzania Wema wa Magufuli unatokea wapi hapo. Huyu alikuwa muaji akitumia propaganda za usafi ndani yake.
 
Wewe acha hizo,PM anajua jinsi ya kucheza na mziki wa dj. Yaan ngoma inaachiwa ya Mike Jackson,wew unataka acheze style ya rhumba ya Congo😄😄
 
Nafasi ya Waziri Mkuu katika Muundo wa Katiba yetu ni udanganyifu, ubadhirifu wa pesa na tabia ya kupeana madaraka kwa nia za kimkakati (strategic positioning).

Haiwezekani Waziri Mkuu awe na mamlaka na mawaziri na naibu mawaziri asiowateua wala kuwatengua. Waziri Mkuu si muundaji wa serikali!! Rais anaitwa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri! Halafu Waziri Mkuu ni Kiongozi wa Mawaziri Bungeni!!!

Nchi hii haipaswi kuwa na Waziri Mkuu kama anayeunda serikali ni Rais. Nchi hii haipaswi kuwa na naibu waziri kama tuna Katibu Mkuu wa wizara na wakurugenzi!!

Tunakosa maendeleo kwa sababu fedha kidogo tunazozipata kwenye kodi tunazitumia kununua magari, kulipia makazi, marupurupu nk kuanzia ngazi za wilaya mpaka taifa!! Kuanzia Serikalini, Mahakamani na hata Bungeni!!

Just too bad!
 
Unaelewa majukumu na kazi za hao unao waona hawana maana?!

Kwahiyo kwa kauli yako Shule hazipaswi kuwa na Mwalimu Mkuu?

Kwahiyo kwa kauli yako Jeshi alipaswi kuwa na Chief of Defence Forces?

Ebu ficha ujinga wako.

Hao wote wanateuliwa na wala hawachaguliwi na wale waliochini yao.
 
Shida sio PM shida ni sa100 kaamua kushirikiana na mashetani na mafisadi papa kuuza nchi.

Pm hawez pata back up kama mkuu wa nchi naye ni moja ya dalali wa nchi.

Ingawa pm naye sio msafi.

Kiufupi hii nchi imelaaniwa kupitia viongozi wake.

#MaendeleoHayanaChama

Sa100....[emoji23][emoji23]. Nimeipenda hiyo mkuu!
 
Tatizo kubwa na Majaliwa ni uongo na unafiki. Mtu akishakuwa na sifa hizo mbili jitahidi kutokumuamini kwa chochote kile. Mkwepe, mpinge na mkosoe kila wakati.
 
Uliposema tu Mtendaji Mkuu wa Shughuli za Serikali bila kusema ni wapi anakuwa mtendaji mkuu nikaona ni walewale tu.
 
Back
Top Bottom