Je, Waziri Mkuu anajitenga na Serikali?

Bibititi1

JF-Expert Member
Sep 28, 2014
464
218
Kila nchi hupitia Changamoto tofauti kwa Nyakati Tofauti, Katika Nchi yetu kuliwahi kuwa na Gumzo Masuala Ya Tozo, Tukaja Suala La Umeme na Maji na Sasa Suala la Upandaji wa Mafuta Kidunia.

Katika Masuala Yote haya Waziri Mkuu Hukuwahi Kutoka mbele na Kusemea au Kutetea Masuala haya Hadharani Kuonekana yupo pamoja na Serikali Inayoendeshwa na Rais Samia. Amekuwa akimlaghai Rais Kwa Kuonekana anafanya vikao vya ndani Kutatua Matatizo ila Ukweli Hukuwahi Kutoka nje na Kusemea Serikali na Hatua anazochukua kama kiongozi wa Mawaziri katika kila sakata linalotokea nchini.

Wizara ambayo ipo chini yako ndio kinara wa kuwa na Kiwango cha Chini cha utendaji, Kuna Suala la mwenge lipo kimya husemi kitu (na Taarifa juu ya Hujuma za Mbio za Mwenge unazozitengeneza wakuu wa wilaya na mikoa ambayo tayari Mwenge umekwisha kupita wanafahamu jinsi hali ilivyo) lakini pia kuna suala la Sensa nalo upo kimya hili ni jukumu lako chini ya sera na uratibu.

AMEZOA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA YA KUENDESHWA.
Katika suala ambalo linanipa ukakasi ni kwamba vikao unavyofanya kumuonesha Rais Unamsaidia ni vya uongo, umezoea kuendeshwa kama ulivyokua ukiendeshwa awamu iliopita lakini huku Unatoenesha wazi huna uwezo wa kifikra wala kuwa kiongozi wa Mawaziri na hizi Hujuma kwa Rais.

Katika awamu ya tano ya uwaziri mkuu wake, mh majaliwa, kiukweli (kwa mtazamo wangu), alikuwa kama mtu mwenye wasiwasi mno asiyejiamni sana. Alizoea kufokewa na kutishiwa 'nitapiga mpaka shangazi zako' hakuwa ni mtu wa kujiamini n.k.

Awamu hii ya sita mambo yamebadilika mambo mengi huanzia bungeni kwanini majaliwa anashindwa kuyadhibiti kuanzia huko ni mtu wa maigizo anayetaka kuonekana ana mikono misafi anataka kuonekana serikali inatengeneza matatizo na kuyatatua. Hii si awamu ya ndiyo mzee ni awamu ya kuonyesha uwezo.

ANAYEISHI KINAFKI
Uislamu unaelekeza mnafiki ana sura tatu kwanza akihaidi atimizi, muongo tatu ameficha uzuri kwenye ubaya kufanya kihiyana. Sura aliyoitengeneza na kutoa matamko kwenye mambo madogo ni sura ya unafki mbona hatumuoni akizungumzia masuala ya sensa, mbona hazungumzi masuala ya mwenge, haonekani kwenye kuzungumzia bei ya mafuta serikali imesimama wapi. Waswahili wanasema kama umeamua kuuza utumbo usiogope nzi. Majaliwa anataka kujitengeneza kuwa yeye ni msafi siasa za janja janja kama za RUTO.

MTENDAJI MKUU WA SHUGHULI ZA SERIKALI NI NANI KAMA SI WAZIRI MKUU?.
Wakati huu ambapo tupo kwenye kupanda kwa bei za mafuta na nishati nyinginezo waziri mkuu yupo kimya na lawama zote ni kwa Waziri wa nishati,

Matatizo ya kukosekana kwa maji lawama ni kwa Rais na waziri wa Maji, Yakifungiwa magazeti, vifurushi vikipanda lawama ni kwa Rais na waziri wa habari. Waziri Mkuu anasimamia jambo gani? badala yake yupo kushanga kupanda kwa bei ya mchele ambao unalimwa hapa nchini kwamba hajui athari ni suala la kupanda kwa bei ya mafuta ndiyo kuna athiri uzalishaji hivyo bei kupanda?

Ukitazama mfumo huo aliojiwekea anataka kuonekana msafi kuna ajenda nyuma ya pazia na genge lake. Kama Huna Uwezo Jiuzulu kama Una Ndoto za Urais Jiuzulu, Usiharibu nchi kwa kutaka Rais Aonekane Mbaya na Wewe Mzuri kwa Kuweka Mikono yako Safi.

Tunafahamu kuna baadhi ya wabunge Livingstone Lusinde (kibajaji), Luhaga Mpina Kuanza kupishana kwa kauli ndani ya chama ni mgogoro inayotengenezwa na genge la Waziri mkuu. mtifuano wa hoja zinazo kinzana katika siasa ya CCM. Katika awamu ya tano hatukuwahi kusikia kauli za kushangaza kutoka kwa wabunge kutupia lawama Mawaziri siku zote maswali ya kitaifa bungeni hujibiwa na Waziri mkuu ambaye ni mtendaji mkuu wa Serikali.

WAVURUGAJI WA AWAMU YA SITA
Wamepanga kuleta mtikisiko wa siasa za kistaarabu zilizoanza kutamalaki na kwa kuanza kuchokonoa na kuharibu taswira ya mwenyekiti. Mawaziri wanatukanwa na wabunge kwa kashfa za hovyo Waziri Mkuu hatoi uelekezi wa ajenda kama nchi tunasimama wapi?

Mh, Rais tunakuomba muangalie Waziri wako mkuu kwa jicho la tatu kama anakutosha.
 
Tumerudi nyuma miaka 50 kwa kuwa wengi tunawazia kuwafitinisha wenzetu.

Tunatakiwa tufanye kazi kwa bidii ili tufikie mafanikio na malengo.Lakin kaz ni fitina,majungu,uongo Kama huu ulioleta.Hata Rais naye badala ya kufanya kazi ,amekalia kumsengenya na kumparura JPM.

JPM ameshalala kwenye pumziko la milele.Hata umseme ,hasikii .Na machawa wa mama naona mpo kazini.Lakini atafeli tu.
 
Waziri ni tumaini fulani hivi wana ccm wanalo kichwani

Mtakao piga kura mtanichagulia kiongozi mi nishajichagulia maisha yangu
 
Kwa mfumo wetu wa nchi , waziri mkuu utaweza Tu kuleta impact endapo raisi atakupa backup, Alipokufa Jiwe , tuliona ambavyo Majaliwa alijitahd kutembea na Moto ule ule , akaja kugundua anaowakemea indirect anajikuta anamkemea Raisi , kilichopo ni kupiga kimya , ma,-mae hata ningekuwa Mimi napiga mkunjo tu nasubir mafao yangu ..... The same to Kikwete na Pinda ..Pinda alikuwa pambo tuu
 
Ukimwangalia PM kwa jicho la tatu utaona wazi ama hakubaliani sana na jinsi mambo yanavyoenda kwenye hii serikali, au ndani ya serikali hakuna uwajibikaji wa pamoja.

-Wakati CJ (Chui Jike)anashadadia kwa furaha fulani juu ya bidhaa kupanda bei...PM amekuwa anatoa kauli za kujaribu kuzuia wale walanguzi kupandisha bei kiholela.

-Cj ..anasema na bado mafuta yataendelea kupanda(kama vile anafurahia tunavyoungua)....PM anasema serikali itaangalia namna ya kupambana na athari za mfumko wa bei za mafuta.
 
Ukimwangalia PM kwa jicho la tatu utaona wazi ama hakubaliani sana na jinsi mambo yanavyoenda kwenye hii serikali, au hakuna uwajibikaji wa pamoja.

-Wakati CJ (Chui Jike)anashadadia kwa furaha fulani juu ya bidhaa kupanda bei...PM amekuwa anatoa kauli za kujaribu kuzuia wale walanguzi kupandisha bei kiholela.

-Cj ..anasema na bado mafuta yataendelea kupanda(kama vile anafurahia tunavyoungua)....PM anasema serikali itaangalia namna ya kupambana na athari za mfumko wa bei za mafuta.

Huyu ambaye hafahamu Kwanini Mchele wa Mbeya unauzwa bei juu ...?
 
Mi nilimtoa maana kwenye kifo cha Magufuli.. inaonekana hata hawakumuambia kinachoendelea kuwa jamaa kafa, yeye akajimaliza kwa kusema"Rais yupo anachapa kazi, Mnataka aonekane kariakoo?" Alijishushia heshima sana
 
Kila nchi hupitia Changamoto tofauti kwa Nyakati Tofauti, Katika Nchi yetu kuliwahi kuwa na Gumzo Masuala Ya Tozo, Tukaja Suala La Umeme na Maji na Sasa Suala la Upandaji wa Mafuta Kidunia.

Katika Masuala Yote haya Waziri Mkuu Hukuwahi Kutoka mbele na Kusemea au Kutetea Masuala haya Hadharani Kuonekana yupo pamoja na Serikali Inayoendeshwa na Rais Samia. Amekuwa akimlaghai Rais Kwa Kuonekana anafanya vikao vya ndani Kutatua Matatizo ila Ukweli Hukuwahi Kutoka nje na Kusemea Serikali na Hatua anazochukua kama kiongozi wa Mawaziri katika kila sakata linalotokea nchini.

Wizara ambayo ipo chini yako ndio kinara wa kuwa na Kiwango cha Chini cha utendaji, Kuna Suala la mwenge lipo kimya husemi kitu (na Taarifa juu ya Hujuma za Mbio za Mwenge unazozitengeneza wakuu wa wilaya na mikoa ambayo tayari Mwenge umekwisha kupita wanafahamu jinsi hali ilivyo) lakini pia kuna suala la Sensa nalo upo kimya hili ni jukumu lako chini ya sera na uratibu.

AMEZOA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA YA KUENDESHWA.
Katika suala ambalo linanipa ukakasi ni kwamba vikao unavyofanya kumuonesha Rais Unamsaidia ni vya uongo, umezoea kuendeshwa kama ulivyokua ukiendeshwa awamu iliopita lakini huku Unatoenesha wazi huna uwezo wa kifikra wala kuwa kiongozi wa Mawaziri na hizi Hujuma kwa Rais.

Katika awamu ya tano ya uwaziri mkuu wake, mh majaliwa, kiukweli (kwa mtazamo wangu), alikuwa kama mtu mwenye wasiwasi mno asiyejiamni sana. Alizoea kufokewa na kutishiwa 'nitapiga mpaka shangazi zako' hakuwa ni mtu wa kujiamini n.k.

Awamu hii ya sita mambo yamebadilika mambo mengi huanzia bungeni kwanini majaliwa anashindwa kuyadhibiti kuanzia huko ni mtu wa maigizo anayetaka kuonekana ana mikono misafi anataka kuonekana serikali inatengeneza matatizo na kuyatatua. Hii si awamu ya ndiyo mzee ni awamu ya kuonyesha uwezo.

ANAYEISHI KINAFKI
Uislamu unaelekeza mnafiki ana sura tatu kwanza akihaidi atimizi, muongo tatu ameficha uzuri kwenye ubaya kufanya kihiyana. Sura aliyoitengeneza na kutoa matamko kwenye mambo madogo ni sura ya unafki mbona hatumuoni akizungumzia masuala ya sensa, mbona hazungumzi masuala ya mwenge, haonekani kwenye kuzungumzia bei ya mafuta serikali imesimama wapi. Waswahili wanasema kama umeamua kuuza utumbo usiogope nzi. Majaliwa anataka kujitengeneza kuwa yeye ni msafi siasa za janja janja kama za RUTO.

MTENDAJI MKUU WA SHUGHULI ZA SERIKALI NI NANI KAMA SI WAZIRI MKUU?.
Wakati huu ambapo tupo kwenye kupanda kwa bei za mafuta na nishati nyinginezo waziri mkuu yupo kimya na lawama zote ni kwa Waziri wa nishati,

Matatizo ya kukosekana kwa maji lawama ni kwa Rais na waziri wa Maji, Yakifungiwa magazeti, vifurushi vikipanda lawama ni kwa Rais na waziri wa habari. Waziri Mkuu anasimamia jambo gani? badala yake yupo kushanga kupanda kwa bei ya mchele ambao unalimwa hapa nchini kwamba hajui athari ni suala la kupanda kwa bei ya mafuta ndiyo kuna athiri uzalishaji hivyo bei kupanda?

Ukitazama mfumo huo aliojiwekea anataka kuonekana msafi kuna ajenda nyuma ya pazia na genge lake. Kama Huna Uwezo Jiuzulu kama Una Ndoto za Urais Jiuzulu, Usiharibu nchi kwa kutaka Rais Aonekane Mbaya na Wewe Mzuri kwa Kuweka Mikono yako Safi.

Tunafahamu kuna baadhi ya wabunge Livingstone Lusinde (kibajaji), Luhaga Mpina Kuanza kupishana kwa kauli ndani ya chama ni mgogoro inayotengenezwa na genge la Waziri mkuu. mtifuano wa hoja zinazo kinzana katika siasa ya CCM. Katika awamu ya tano hatukuwahi kusikia kauli za kushangaza kutoka kwa wabunge kutupia lawama Mawaziri siku zote maswali ya kitaifa bungeni hujibiwa na Waziri mkuu ambaye ni mtendaji mkuu wa Serikali.

WAVURUGAJI WA AWAMU YA SITA
Wamepanga kuleta mtikisiko wa siasa za kistaarabu zilizoanza kutamalaki na kwa kuanza kuchokonoa na kuharibu taswira ya mwenyekiti. Mawaziri wanatukanwa na wabunge kwa kashfa za hovyo Waziri Mkuu hatoi uelekezi wa ajenda kama nchi tunasimama wapi?

Mh, Rais tunakuomba muangalie Waziri wako mkuu kwa jicho la tatu kama anakutosha.
Akivaa miwani analinga,akitokea hadharani anamzidi Mama umaarufu,akivaa suti anajiona yeye Rais,Sasa afanyeje!?
 
Back
Top Bottom