Je, Wazazi mnayajua wanayofanya mabinti zenu wawapo vyuoni?

Mi nasoma tu michango yenu. Nipo jirani kabisa na chuo cha Uhasibu Kurasini. Ninayoyaona hapo! Eeeeeh
 
Hahaha huu ni upotoshaji, kijana aliyeko chuo kikuu ni mtu mzima sio mtoto. Akimaliza chuo harudi nyumbani kuishi ile ni kuaga kwenda zake kuanza maisha. Hivyo kuishi na mke au mume ni utayari wa kujiandaa aendako baada ya chuo.
Hapa wazazi hawahusiki kwa lolote na kwa namna yoyote.
 
Hahaha huu ni upotoshaji, kijana aliyeko chuo kikuu ni mtu mzima sio mtoto. Akimaliza chuo harudi nyumbani kuishi ile ni kuaga kwenda zake kuanza maisha. Hivyo kuishi na mke au mume ni utayari wa kujiandaa aendako baada ya chuo.
Hapa wazazi hawahusiki kwa lolote na kwa namna yoyote.

Rights involve obligations. Nimemaliza.
 
Sitasahau brother alinywa papuchi na mchumba wake sharti atolewe bikra akiwa ndani ya ndoa

Ndugu, marafiki na familia tulijua ndoa yao itafuata baada ya msichana kumaliza chuo kikuu..

Mara paaah.... Mchumba mtarajiwa anakuja na kibendi kutoka chuo.huko chuo panahitaji akili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unadhani anakubali kumpeleka MTU, ni kweli mtu akimaliza chuo ni mtu mzima kimaamuzi lakini binti wa miaka 23 hataki kuwaambia ndugu zake na familia shughuli inayomuweka mjini Kama mzazi inauma subiri uwe mzazi mtoto wako afikie stage hii ndio utajua maharage ni mboga au futari!!!!!
Najua yanayofanyika. Kuna wengine huwa hawataki kurudi vijijini nk. Ila ukitumia nguvu bila maarifa ndiyo mtamkosa kabisaa.


Maranyingi niko maeneo ya karibu na moja ya hostel za hapa dar. Unakuta likizo ndefu mabinti kati ya 4-8 wanakaa chumba kimoja kwa miezi zaidi ya mitano hawarudi kwao hili ni tatizo. Wengine wanahangaika kupata nafasi za field hukuhuku ili wasirudi ma kwao.

Mkitumia nguvu hamumpati huyo ashajua kutafuta pesa...tena akihisi nyumbani mlikuwa mnamtesatesa ndo kabisaa....tumien i maarifa zaidi ya command


Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
Habari zenu wana JF,

Leo nimeona nilete bandiko lenye kichwa hiko cha habari hapo juu...

Kwa kuanza napenda kueleza kuwa binafsi nimebahatika kusoma katika taasisi tofauti za elimu ya juu na katika mikoa tofauti... nikimaanisha College kwa ajili ya diploma na University kwa ajili ya bachelor degree katika mikoa miwili tofauti...

Katika mazingira hayo nimeshuhudia mabinti kwa asilimia kubwa wakifanya mambo ya kusikitisha katika miaka yao yote vyuoni...binti ambae akiwa nyumbani hataki kusaidia kazi ndogo ndogo za nyumbani, basi akiwa chuoni anakaa chumba kimoja kama mume na mke na kijana wa kiume au hata mtu mzima kwa miaka yote anapokua chuo

Zaidi ya hapo anafanya kazi zote za hapo getoni...anapika anafua nguo zake na za mumewe, anafanya usafi wa geto lakini pia anatoa unyumba kila siku kwa sababu wanalala kitanda kimoja!

Bahati mbaya binti akiwa nyumbani hafanyi na hataki hata kuosha kikombe chake alichonywea chai yeye mwenyewe....na hii ni asilimia kubwa sana ya mabinti wanaishi hivi wakiwa vyuoni.

Wazazi tafakarini na muongee na watoto zenu wakike wanaosoma chuo mjue uhalisia wa maisha yao wanapokua vyuoni.

NB: Kila nikiwaza hivi napata jawabu kwanini ndoa zimekua ngumu sana siku hizi. Mabinti wamekuwa wakianza maisha ya ndoa kabla ya muda wake hvyo wanapata experience ambayo ni ya uongo kuhusu ndoa...na hili ni tatizo. Zaidi ni kiasi cha mimba ambazo mabinti wanazitoa katika kipindi cha miaka ya chuo...

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanaume inabidi washiriki sana kwenye maisha ya mabinti zao,wanapokuwa vyuoni,hakikisha unamuwezesha kifedha ili ukata usimlzimishe kutengeneza ndoa hewa.
Tamaa ya fedha,na vitu vya thamani,malezi duni huchangia mabinti wengi kufanywa wake za watu wanapokuwa vyuoni,na muda wa chuo ukiisha,na "ndoa" hiyo imeisha.
Akitoka hapo,unakutana naye,unaoa kumbe umeoa janga,ameishatumika balaa,ametoa Komba kama zote.Laana tupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa tatizo kubwa ni malezi tena kwa pande zote mbili, wanaume na wanawake.
Tatizo huwa tunaona kuwa malezi anapaswa apewe mtoto wa kike tu ndio maana tuna jamii za ajabu sana kwa wakati huu.

Watoto hatuwalei ktk misingi inayopaswa tunafikiri ubabe na kuwachunga chunga kama ndama ndio malezi. Matokeo yake mtoto anapopata uhuru hajui jinsi ya kuutumia. Mtoto wa kiume anaoa na mtoto wa kike anaolewa akijua ndivyo alivyopaswa kuutumia uhuru huo. Tuwape skills za maisha,wajitambue,wakue,wajiongoze na wajiheshimu. Ili hata ikitokea hawapo ktk macho yetu wayaendeleze hayo mazuri.

Na inasikitisha zaidi pale mtoto wa kiume anapojisifia kwa kufanya uovu na kuona kuwa mtoto wa kike ndio anapoteza, maybe ni kweli mtoto wa kike anapoteza zaidi maana kuna mimba nk(kwa mawazo yetu) lkn ikumbukwe mimba hizo zinatolewa kwa shinikizo la wanaume na ndio watoaji hadi wa pesa. Dhambi hii inawatafuna wote hadi kifo.

Wote tunatarajia kuwa na familia hapo baadae, lakini sidhani kama kuna mtu anapenda kuwa na familia ya hovyohovyo. Tukumbuke tu kuwa haya tuyaonayo sasa ni matokeo tu ya yale madhambi tuliyoyafanya huko awali yanaendelea kututafuna(KARMA)


KUWA MTOTO AMBAE UNGEPENDA WATOTO WAKO WAWE KESHO, KISHA UKIWAPATA WALEE KTK MISINGI IPASAYO.
 
Bora yao hao wanaoolewa,kuna wale ambao wanapenda kuishi maisha ya kifahari,na kuamua kuwa na mabwana zaidi ya 6 tena wenye pesa,unafikia baada ya muda demu anajulikana mji mzima hasa miji midogo,WANAWAKE HAWAOGOPI UKIMWI
 
Jamani acheni kiwaoa wazazi majukumu yaliyopitiliza! Lijitu liko chuo lina akili timamu likizingua unalitimua home, bado unataka mzazi aende akakague chuo anafanya nini na anaishi wapi na nani??

Mzazi jukumu kake hapo ni kutoa wawaiza tu akiyafata au kuyatupa ni yeye mwenyewe maana ameshakuwa na uwezo wa kujua future yake na akicheza atasaga meno.
 
Hapa nilipo saiv nyumba nilio panga jamaa kamuweka Mtoto Wa chuo ndani afu kanaonekana bado kadogo sana . kapo kanasoma Chuo cha mahakama . Hadi nakaonea huruma maana huyu jamaa anabadilisha wasichana . wazazi kuweni makini watoto watarudi na maradhi badala ya ujuzi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najua yanayofanyika. Kuna wengine huwa hawataki kurudi vijijini nk. Ila ukitumia nguvu bila maarifa ndiyo mtamkosa kabisaa.


Maranyingi niko maeneo ya karibu na moja ya hostel za hapa dar. Unakuta likizo ndefu mabinti kati ya 4-8 wanakaa chumba kimoja kwa miezi zaidi ya mitano hawarudi kwao hili ni tatizo. Wengine wanahangaika kupata nafasi za field hukuhuku ili wasirudi ma kwao.

Mkitumia nguvu hamumpati huyo ashajua kutafuta pesa...tena akihisi nyumbani mlikuwa mnamtesatesa ndo kabisaa....tumien i maarifa zaidi ya command


Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
Upo sawa
 
Jiulize kwa nini inatokea hivo, nani wa kulaumiwa? Ulichoeleza ni matokeo. Gharama za masomo ni kubwa. Wazazi hatuna uwezo. Serikali imenawa mikono hata mikopo ni tabu. Usajiri wa vyuo haujari miundombinu, hakuna hostel, watoto wanaishi vibandani vingine havina umeme. Tusilaumu matokeo, tulaumu chanzo.
 
Tunafahamu vzr. Kwani nasisi tumepita huko. Elewa kwamba Colleges & Universities ni kwaajili ya watu wazima
Kwa hiyo acha wajiachie tu. Mimi sipotezi muda wa kumchagulia kijana na binti yangu maisha yake
Nashukuru nimefanikiwa kuwavusha salama utoto wao.
 
Back
Top Bottom