Je waweza?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,216
113,512
Mwenzio (mwenza/ mwenzi wako) anakujia na wazo la kubadilishana simu za mkononi angalau kwa wiki moja - kuanzia Jumatatu asubuhi hadi Jumapili jioni.

Na anataka mbadilishane papo hapo bila kusubiri chochote. Yeye atakuwa na simu yako kwa hiyo wiki nzima na ataweza kupokea simu zako, text messages zako, na mengineyo na wewe utaweza kufanya vivyo hivyo na simu yake.

Je utafanya nini? Utamkubalia? Au utampiga tarehe kwanza ili upate wasaa wa kuwataarifu baadhi ya watu kuwa mwenzio anayo simu yako kwa hiyo wasikutafute kwenye namba hiyo i.e. kuweka mambo sawa?
 
Aisee NN very good idea I will be glad kufanya hiyo exchange on the spot tena without hesitating.
 
KWA HISANI YA NDOA YETU(JAPO SIJAFIKA HUKO)......NTAVINJA UKIMYA.... NA KUMWOMBA AWE NA VIDONGE VYA KUSHUHSA PRESHA:becky::becky::becky::becky::becky::becky::becky:!!
 
nitaona udhia wa kukabidhisha simu yangu kwa mtu mwengine na kushindwa kuwasiliana na niwatakao bila ya kuomba namba kutoka kwake.

lakini akitaka hiyo simu ili apate amani ya nafsi yake..........nitampa ila nitampa warning asije kulalamika kwa kitakachotokea baada ya hapo :)
 
Anapokuja na hilo wazo yeye anakua ashajiandaa.....sasa na mimi anipe muda wa kujiandaa...
Kwanza sihitaji simu yake in the first place:doh::frown::frown::frown:
 
Anapokuja na hilo wazo yeye anakua ashajiandaa.....sasa na mimi anipe muda wa kujiandaa...
Kwanza sihitaji simu yake in the first place:doh::frown::frown::frown:

haina haja kabisa, namkatilia moja kwa moja.
 
Kwangu itakuwa ngumu sio kuficha kitu la hasha ni mambo ya kazi. Simu yangu imeconnectiwa na shughuli za ofisi kwa hio kuna update nitaweza kukosa au kupigiwa na bosi kuna emergence kazini nishindwe kwa vile atakuwa nayo mama. Cha muhimu ni kupendana na kuaminiana. Infact siku hizi vicheche vina simu maalumu vinaacha ofisini kwenye droo hazifiki nyumbani kabisa.
 
Hapo unajitafutia homa zisizo na ulazima kwa mtaji huu mmmh :confused2:
 
Simu yangu ni yangu, siwezi kumpa. na aking'ang'ania nitampa yangu then ntamwambia yake akae nayo tu maana atakuwa alishajiandaa ndo maana akatoa hilo wazo. kwa hiyo ni kama ananiambia anataka kunikagua mimi sababu sitapata lolote toka kwake, so akae tu na simu zote
 
Back
Top Bottom