GE2025 Je, watanzania wale wanojiandaa kupiga kura ni wale ambao hawana cha kupoteza? Na ni kwanini wafanye hivyo?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richard

Platinum Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
16,630
Reaction score
25,586
Kesho ni tarehe 1 Oktoba 2025 siku ya kwanza ya mwezi wa uchaguzi, mwezi muhimu na wenye kubeba mstakabali wa siasa za Tanzania.

Mie nina suali kwa watanzania ambao wamekuwa wakijitokeza kudandia magari ya kukodi na kwenda kushabikia mikutano ya kampeni ya CCM na baada ya hapo kurudi majumbani mwao kuendelea na maisha yao ya kila siku.

Je, ni kwanini watanzania hawa wenzetu watajitokeza kwenda kupiga kura katika mazingira ya sasa ya CCM kuwa ni chama pekee ambacho kimejindaa kushinda uchaguzi huo?

Je, watanzania hawa wakubali kuwa wao ni wajinga na wameshindwa kutafakari hali halisi ya siasa za nchi yetu na kwamba chama tawala cha CCM kimeshindwa kuwaletea maendeleo, kuinua hali yao ya maisha, kuinua kipato chao na kupata huduma bora za hospitali bila kusumbuliwa na ada ya kumuona daktari?

Je, watanzania hawa wakubali kwa moyo mmoja kwamba vitendo cha utekaji raia wenzao, kuteswa, kuuawa na kupotezwa ni vitendo halali na vya kuungwa mkono?

Je, watanzania hawa wakubali kwamba hata wasanii waweza kuwa ni sehemu ya wabunge katika bunge la Tanzania chombo pekee cha kutunga sheria za nchi hii wengine wakiwa hawana sifa sahihi za kielimu kushika nafasi za ubunge?

Je, watanzania hawa wakubali kuwa miradi yote mikubwa ya kimkakati ukiwemo mradi wa bwawa na Mwalimu Nyerere imejifia tangu ahadi ya kujengwa kwake itolewe mwaka 2015?

je, watanzania hawa wakubali kuwa ukienda ofisi ya TRA uwe tiyari kutoa rushwa ili upate leseni ya biashara au leseni ya udereva?

Je, watanzania hawa khasa wale wamachinga wakubali wamachinga wote wameondolewa katika maeneo ambayo walikuwa wakifanya shughuli zao za kihalali tangia mwaka 2021?

Watanzania bado wana muda mzuri kabla ya uchaguzi tarehe 29 Oktoba kutafakari sana juu ya dhamira ya CCM kutaka kuendelea kutawala nchi hii. Tukiwa ni waafrika kama wenzetu wa Ethiopia ambao juzi wamemaliza ujenzi wa bwawa la umeme la GERD (Grand Ethiopian Renaissance Dam) jambo linochochea ukuaji himilivu yaani sustainable growth.

Ethiopia walikuwa wakitumia njia za kiasili za kupata nishati ya umeme khasa katika maeneo ya vijijini wakitumia mbao, kuni na kinyesi cha wanyama hiyo huitwa biomass. Ethiopia wamekuwa na mabwawa zaidi ya mawili yaani bwawa la kwanza la Aba Samuel lilojengwa mwaka 1932 na baadae wakajenga mabwawa ya Koka na Awash katika miaka ya sabini na tisini.

Ethiopia sasa wana bwawa la GERD lenye kutoa mishati zaidi ya megawati 6000 ambazo ni za kutosha kwa nchi nzima kiasi cha kuanza kuiuza nishati hiyo katika nchi zingine za Afrika.

Mapinduzi haya ya nishati katika nchi ya Ethiopia yaonyesha ni kwa jinsi gani nchi hiyo ina dhamira ya kweli ya kuleta maendeleo kwa wananchi wake pamoja na uongozi imara wenye nia na dhamira ya kweli.

Nishati ya uhakika husababisha maendeleo ya haraka khasa viwanda, biashara mbalimbali na khasa katika maeneo ya vijijini umeme utachochea ujenzi wa makazi bora na miundombinu ingine ya uhakika kama barabara, madaraja, mahospitali na shule za maana. Maendeleo haya huleta pia watoto wa shule za vijijini huko kuweza kupata elimu bora khasa ya kompyuta ambazo zitawawezesha watoto hao kuwa na uwezo wa kiakili katika ubunifu na ukuzaji vipaji mbalimbali.

Sasa Tanzania bado twahangaika na ujenzi wa bwawa la Nyerere na hata mkandarasi anaejenga bwawa hilo (Arab Contractors) haijulikani kama bado aendelea na kazi ya ujenzi wa bwawa hilo.

Je, watanzania wameona na wapo tayari kuruhusu hali ya kusuasua kwa ujenzi wa bwawa la Nyerere na usitoshe tunayo mabwawa kama la Mtera na Nyumba ya Mungu. Na kwanini tusijenga mabwawa ya kutoha ya umeme ambao ungetosheleza nch nzima ili kuondokana na dhana ya kutaka kununua umeme wa Ethiopia?

Watanzania na waafrika kwa ujumla tabia zetu zafanana mno kiasi kwamba hata wagombea ubunge mara nyingi wamekuwa wakitoa ahadi ambazo ni wazi ni za mizaha. Kwa mfano hata Kenya kwenye kampeni za uchaguzi mwaka 2022 mgombea aitwae George Wajackoyah akitoa ahadi za kampeni alisema akichaguliwa atahakikisha ainua uchumi wa Kenya kupitia kilimo cha Bangi, kufuga nyoka na kuuza nyama ya mbwa na fisi! Bwana Wajackoyah aliamini kuwa kilimo cha bangi kingetatua matatizo ya kiuchumi yanoikabili Kenya.

Sasa kwa watanzania wapo wagombea ubunge ambao wametoa ahadi za kimzahamzaha kabisa. Yupo ambae amesema akichaguliwa atamleta mcheza sinema maarufu wa zamani wa kimarekani Arnold Schwarzenegger mwenye umri wa miaka 78 kuja Arusha Tanzania! Pia yupo mgombea ambae amesema akichaguliwa atasaidia wanaume wapewe fedha za kutolea mahali kwa ajili ya kuoa!

Hivi, watanzania kweli twasimama majukwaani kusikiliza ahadi za kimzaha kama hizi kweli?

Ikiwa watanzania wengi hawakubaliani na kinoendelea kwamba CCM yaonekana kulazimisha watu wajitokeze kupiga kura ifikapo tarehe 29 Oktoba katika uchaguzi ambao una mizengwe, basi jambo la msingi ni kutoshiriki uchaguzi huo.

Watanzania wasipojitokeza kupiga kura watakuwa watoa funzo kwa CCM na serikali yake kwamba wapaswa kujitafakari na hii itaitwa kutoshiriki zoezi la kupia kura au "disengagement".

Kupiga kura ni haki ya msingi kabisa katika kukuza demokrasia lakini haimaanishi CCM na serikali yake au INEC waweza kuwalazimisha wapiga kura kufanya hivyo ilhali utaratibu wa kidemokrasia umekiukwa hata ndani ya chama tawala chenyewe kwa kukiuka katiba yake na ile katiba ya nchi.

Hivyo CCM na serikali yake wakubali kwamba demokrasia katika nchi yetu imevurugwa (is in crisis), jamii wa wananchi wengi imegawanyika, kipato cha watu maskini kimezidi kupotea huku baadhi ya watanzania wakiwa na uwezo mkubwa wa kifedha huku wakionyesha uwezo huo kupitia mitandao ya kijamii na pia katika wakati wote wa maisha yao bungeni, wabunge wameshindwa kuonyesha nia ya kutatua shida za wananchi wanowawakilisha.

Bila mabadiliko ya katiba, ushirikishwaji wa wanasiasa wote katika utaratibu wa kidemokrasia na CCM wenyewe kurudi tena Chamwino kurudia taratibu halali za kumpata mgombea wa uraisi, uchaguzi wa tarehe 29 Oktoba si uchaguzi halali.

Sasa namaliza kwa suali.

Hawa watanzania wanojitokeza kuhudhuria mikutano ya kampeni kwa bashasha na nderemo nyingi je, hawa ni wale ambao hawana cha kupoteza au kwa kiingereza husemwa "They have nothing to lose?

Na je, hawa watanzania kwanini wafanya hivyo au ni kujidharau tu yaani "ignorant"?
 
Kuna wengine wanajiandaa kupiga kura na kupiga waandamanaji
 
Tunaongozwa na watu ambao walitakiwa kua jela na wanotakiwa kutuongoza wako jela
 
Unalinganisha bwawa la umeme la Ethiopia dhidi ya hili la JKNHEP tulilojenga sisi? Au unaongelea uchaguzi wa 29/10.

Hebu jipange ueleweke
 
Ni wajinga pekee ndiyo watakao jitokeza kushiriki kwenye hayo maigizo.
 
Wewe mtu wa kukubali kusombwa kwenye lorry sijui bus kwenda kwenye mikutano ya CCM unaona ana akili sawa sawa?

Kwanza ukimwambia habari ya hali ya bwawa la umeme la Mwl.Nyerere ukilinganisha na lile la Ethiopia wala hakuelewi. Anaona ni kama unaongelea mambo ya mbinguni ambako hana ukakika kama hiyo mbingu ipo au haipo. 🙆
 
Na hii ndio aina ya watanzania ambao serikali ya CCM inawataka hili iendelee kutawala milele.

Serikali ya ccm inapenda watanzania wawe ma mbumbu wasiojua vitu vingi kiasi kwamba hata wakiambiwa kwa hapa Africa ni Tanzania pekee tu ndio kuna train ya SGR watakubali na watampigia vigeregere Samia kwa kuifanya Tanzania iwe na miundo mbinu ya kipekee africa nzima.
 
Back
Top Bottom