Bin Maryam
JF-Expert Member
- Oct 22, 2007
- 685
- 14
nadhani hawajui la kufanya au ni kutetea chochote kitu....wanaogopa wakileta za kuleta wanamwaga unga au wanakuwa wakolimba! Kwa hivyo hata wapinzani wakipewa nchi, mambo ya kulinda maslahi na kuogopa kushindwa yapabaki palepale. Kwa hiyo hakutakuwa na jipya sana. Cha muhimu ni kufight kubadilisha kwanza haya mambo, bila kuyabadilisha hawataweza kuchukua nchi. Kama wameweza kufichua ufisadi nadhani hata fight ya kubadili hizo institutions wanaiweza.
Yes Ngabu,
this is what I am also talking about. Utasikia mtu akikubali kuwa ccm haifai kabisa kuongoza nchi na kisha baadaye tena anaishia kwenye kusema kuwa si vyema kuitoa ccm madarakani sasa hivi.
Mama,
wapinzani walishaanza kuchukua nchi hata vijijini - anzia Tarime - samahani watani zangu wakurya lakini huko kwenu bado ni kijijini.
Bila kuiondoa ccm kwenye uongozi wa nchi, hizo katiba wala roots zingine za vijijini nani atajenga kama ccm wanatumia whatever they can to stay in power?
Huku kwetu bado sana, na wananchi wanajua upinzani maana yake ni vita!
kumbuka hata majimbo yote ya tarime yakachukuliwa na upinzani, na yale ya kilimanjaro pia, na kigoma na wapi tena bado sio nguvu ya kutosha kuleta maendeleo. Lakini sio itakuwa mwanzo mzuri wa kuleta challenge bungeni na sio kuchukua madaraka ya nchi nzima.
Mama:
Unachozungumza wewe ni EYES ON PRIZE. Lakini kuna upande mwingine hatujaungalia. Hivi wapinzani wakiweza kuwa na nusu ya viti vya bunge na kubaki kama wapinzani, ni vitu gani vitatendeka bungeni? Ninaamini check and balance itakuwepo.
Mama ukisema kuwa wapinzani wasichukue madaraka nchi nzima unamaanisha kuwa ccm waendelee kuongoza si ndio?
kama wataweza kuchukua nusu ya viti bunge, kudos. Lakini wapinzani ,watawezaje kuchukua nusu ya viti bungeni?ukweli unabaki kuwa hawataweza kwa vile hawajajiandaa, leo hii ni May 2008! kuna mwaka tu kabla kampeni za uchaguzi hazijaanza.
Kwa vile hamjajiandaa kuchukua kura yangu, sasa mie nifanye nini? hata kama wanaJF wote tukaamua kuwapa kura wapinzani its just a small fraction to win......5000 in ca 40m?
kama wataweza kuchukua nusu ya viti bungeni, kudos. Lakini wapinzani ,watawezaje kuchukua nusu ya viti bungeni?ukweli unabaki kuwa hawataweza kwa vile hawajajiandaa, leo hii ni May 2008! kuna mwaka tu kabla kampeni za uchaguzi hazijaanza.
Muda mwingine huwa najiuliza kama hawa wapinzani ni kina nani. Hivi ni nani leo hii anajitolea kupoteza kila kitu kuwa mpinzani wa ccm Tanzania?
Taarifa zinaonyesha kuwa wale viongozi wa upinzani ni sehemu kidogo tu ya population ya Tanzania. Je waachiwe wao tu kuleta mabadiliko Tanzania.
Nani yuko responsible na kwenda kuhamasisha upinzani kiteto kama matokeo yatakuwa ni kukutana na full brass ya ccm kuanzia Msekwa hadi Komba hadi FFU na wengine ambao wana orders za kupiga yule anayeonekana kuhatarisha maslahi?
Kuna kazi hapa kama ccm ikiendelea kuachiwa dola hata hiyo ndoto ya wabunge 50 percent haitafikiwa.
Kwa matatizo yalivyopo Tanzania wapinzani wajiandae vipi?
Je thread hii imefikia conclusion? kama ndio bado hilo swali lako linahitaji thread mpya ili tusichanganye mambo!
Mimi nadhani tusije kukosa kuelewana. Ngoja nisema msimamo wangu kwenye hili ili kusiwe na utata wowote ule.
a. CCM imeshindwa kuongoza nchi
b. CCM ndiyo chanzo cha matatizo yote ya kisiasa na kiuchumi.
c. CCM ndiyo mama ambaye amemzaa mtoto ufisadi.
d. CCM hawastahili hata dakika moja ya ziada ya kuendelea kutawala jinsi walivyo
e. CCM lazima iondolewe madarakani mapema iwezekanavyo.
That given:
a. Kwa wanaotaka kuiondoa CCM lazima wajue lengo lao la mwisho ni nini. Kuiondoa CCM siyo lengo la mwisho.
b. Lengo lao la mwisho lihalalishe nia yao ya kuiondoa CCM; hivyo kuiondoa CCM ni sehemu ya kufikia lengo hilo.
c. Lengo hilo lazima liwe wazi, linalowezekana, linalovutia na linaloweza kushawishi akili ya mtu yeyote yule. Kwa maneno mengine, lazima liwe lengo lenye kufanya watu waone matumaini, wajawe na shauku, na watambue sababu ya wao kulifikia lengo hilo.
d. Lengo hilo lazima lishawishi fikra za watu wengi zaidi na kati yao lazima wawepo wana CCM. Bila kushawishi idadi ya wana CCM (crossovers) kuiondoa CCM ni njozi isiyotimilika. Ndio maana wenzetu hapa hawategemei kura za watu wa chama chao tu bali wanategemea pia crossovers na independents. Ni lengo gani linaweza kuwashawishi wana CCM na watu wasio na vyama?
e. Wale wanaotaka kuiondoa CCM lazima waonekane kuwa ni bora kuliko siyo sawa au dhaifu kuliko. Hadi watu waone kuwa wale wanaotaka kuingia badala ya CCM ni BORA kwa kila hali hawataweza kuibadilisha CCM. Hivyo, haitoshi kuonesha ubovu wa CCM, bali pia UBORA wa wanaotaka kuingia madarakani.
f. Kwa upande wangu naamini njia ya msingi ya kuonesha ubora wa wanaotaka kuiondoa CCM ni kujenga fikra zenye mvuto na kushinda katika uwanja wa fikra unaothibitishwa na vitendo vya kuvutia.
g. CCM inaweza kuondolewa madarakani saa na siku yeyote pale tu lengo sahihi litakapowekwa wazi na litatimiza kifungu (c) na litakalohakikisha kuwa kifungu (e) nacho kinatimizwa. Nje ya hapo, CCM na ubovu wake itaendelea kuongoza.
h. Kila anayetaka kuona CCM inatoka madarakani lazima aanze kushiriki katika nafasi yake. Ndugu msomaji, wewe unashiriki vipi katika kuhakikisha CCM inaondoka madarakani mapema iwezekanavyo? Jibu la swali lako litakupa wazo ni mapema kiasi gani CCM itaondoka madarakani.
M. M.
Uliuliza swali kuwa upinzani haujajiandaa. Matatizo ya Tanzania ndio maandalizi ya mabadiliko ya serikali. Na kama mtu haoni matatizo ya kutaka mabadiliko then there are something wrong.
Wanasema: Mtu anakuita mpumbavu kwa ridhaa yako na watanzania ni ridhaa yetu kutawaliwa na vichwa maji.
Kwa vile hamjajiandaa kuchukua kura yangu, sasa mie nifanye nini? hata kama wanaJF wote tukaamua kuwapa kura wapinzani its just a small fraction to win......5000 in ca 40m?
Kwa hiyo ina maana CCM wamekushawishi uwape kura yako?
Mimi nadhani tusije kukosa kuelewana. Ngoja nisema msimamo wangu kwenye hili ili kusiwe na utata wowote ule.
a. CCM imeshindwa kuongoza nchi
b. CCM ndiyo chanzo cha matatizo yote ya kisiasa na kiuchumi.
c. CCM ndiyo mama ambaye amemzaa mtoto ufisadi.
d. CCM hawastahili hata dakika moja ya ziada ya kuendelea kutawala jinsi walivyo
e. CCM lazima iondolewe madarakani mapema iwezekanavyo.
That given:
a. Kwa wanaotaka kuiondoa CCM lazima wajue lengo lao la mwisho ni nini. Kuiondoa CCM siyo lengo la mwisho.
b. Lengo lao la mwisho lihalalishe nia yao ya kuiondoa CCM; hivyo kuiondoa CCM ni sehemu ya kufikia lengo hilo.
c. Lengo hilo lazima liwe wazi, linalowezekana, linalovutia na linaloweza kushawishi akili ya mtu yeyote yule. Kwa maneno mengine, lazima liwe lengo lenye kufanya watu waone matumaini, wajawe na shauku, na watambue sababu ya wao kulifikia lengo hilo.
d. Lengo hilo lazima lishawishi fikra za watu wengi zaidi na kati yao lazima wawepo wana CCM. Bila kushawishi idadi ya wana CCM (crossovers) kuiondoa CCM ni njozi isiyotimilika. Ndio maana wenzetu hapa hawategemei kura za watu wa chama chao tu bali wanategemea pia crossovers na independents. Ni lengo gani linaweza kuwashawishi wana CCM na watu wasio na vyama?
e. Wale wanaotaka kuiondoa CCM lazima waonekane kuwa ni bora kuliko siyo sawa au dhaifu kuliko. Hadi watu waone kuwa wale wanaotaka kuingia badala ya CCM ni BORA kwa kila hali hawataweza kuibadilisha CCM. Hivyo, haitoshi kuonesha ubovu wa CCM, bali pia UBORA wa wanaotaka kuingia madarakani.
f. Kwa upande wangu naamini njia ya msingi ya kuonesha ubora wa wanaotaka kuiondoa CCM ni kujenga fikra zenye mvuto na kushinda katika uwanja wa fikra unaothibitishwa na vitendo vya kuvutia.
g. CCM inaweza kuondolewa madarakani saa na siku yeyote pale tu lengo sahihi litakapowekwa wazi na litatimiza kifungu (c) na litakalohakikisha kuwa kifungu (e) nacho kinatimizwa. Nje ya hapo, CCM na ubovu wake itaendelea kuongoza.
h. Kila anayetaka kuona CCM inatoka madarakani lazima aanze kushiriki katika nafasi yake. Ndugu msomaji, wewe unashiriki vipi katika kuhakikisha CCM inaondoka madarakani mapema iwezekanavyo? Jibu la swali lako litakupa wazo ni mapema kiasi gani CCM itaondoka madarakani.
M. M.
hawajanishawishi kama ambavyo wapinzani hawajanishawishi, lkn bibi yangu na babu na majirani zao kule kijijini wameniambia wanawapa kura zao sisiemu.