Je, wajua? Weakness Point ndio Target ya Ushindi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,884
"WEAKNESS POINT NDIO TARGET YA MSHINDI" JE WAJUA?​

Kwa Mkono wa, Robert Heriel


Maisha ni vita, kuna kushindwa na kushinda; Mshindi na mshindwa. Kila ulifanyalo lifanye kwa tahadhari, kila hatua uipigayo ipige kwa umakini na tahadhari kubwa mno. Hakuna jambo zuri linalopatikana pasipo mapigano makali, naam vita ndio suluhu ya ushindi wako. Huwezi shinda bila kushindana katika vita yako. Hatuwezi kujidanganya kama watu wasio na akili, hao wasemao maisha ni bahati, wasemao maisha hupangwa. Huko ni kukosa akili na wendawazimu. Kushinda kwenye vita sio bahati. Kushinda vita ni jambo la uamuzi wa mtu au kundi la watu. Bahati inatengenezwa na mtu mwenyewe. Hii ni kusema ushindi wa mtu hutengenezwa na yeye mwenyewe. Hakuna bahati katika kushinda vita.

Niite Taikon wa Fasihi, mwana kutoka Nyota ya Tibeli, Nyota yenye mbawa mbili za Yakuti samawi ipaayo kutoka ulimwengu hata ulimwengu.

Tangu na tangu, kale na kale. Ushindi hauji wenyewe; kama ungekuja wenyewe basi pasingekuwa na thamani ya Ushindi, hivyo watu wasingeshangilia pale washindapo. Ushindi unatafutwa kwa udi na uvumba, Unatafutwa kwa machozi, jasho na damu. Kwa nguvu na kwa akili, hila na werevu. Ushindi ni ushindi tu.

Vita ya mwanadamu huanza tangu akiwa tumboni mwa mamaye, hata akizaliwa, akikua na tamati yake ni siku atakapokufa. Ili uishi lazima mwingine afe, ili ufanikiwe lazima mwingine asifanikiwe. Ili uolewe au uoe basi sharti mwingine asiolewe au asimuoe huyo unayemuoa, Ili upate basi sharti mwingine akose. Vita ni vita, hakuna huruma kwenye vita, ili ushinde unapaswa uuzidi ujasiri wa adui yako.

Thamani ya maisha ni Kifo, na thamani ya mauti ni Uhai. Pale mauti na Uhai vinapopigana vita pasi lazima wapiganaji wachague upande wa kujiunga. Pale Ufukara na Ukwasi vinapopigana vita basi lazima wapiganaji wachague upande. Huwezi chagu upande wa ufukara ukapigana na Utajiri kwa mategemeo ya kupata utajiri. Na huwezi kuchagua upande wa mauti ukapigana na uhai/uzima alafu utegemee utapata uzima. Huko ni kujidanganya na kujiongopea.

Pale Upendo na Chuki vinapopigana vita lazima mpiganaji achague upande. Huwezi chagua upande wa chuki alafu mwisho wa vita utegemee kupendwa au upendo.

Pengine bado nikawa nasema kwa jinsi isiyowazi hata wengine wasinielewe. Ikiwa ni hivyo mnisamehe.

Nataka ufahamu kuwa, unapozaliza tuu ni rasmi umeingia kwenye vita. Labda niweke sawa hapa. Kuna vita na Pambano.

Pambano ni kama mashindano tuu ambayo wote mnaweza ibuka washindi. Pambano ni mashindano ambayo watu hushindania jambo fulani la umuhimu kama vile elimu, au huduma zingine muhimu. Kwa mfano, Wakati tunasoma shule tulikuwa tunapambana kila mtu alikuwa anataka aende mbele mpaka afike chuo. Kulikuwa na uwezekano wote tukafaulu na kwenda chuo kikuu. Lile lilikuwa pambano. Kumbuka kushinda pambano sio kushinda vita.

Vita ni mapigano makali ambapo mtu mmoja au upande mmoja ndio unapaswa kushinda. Mapigano mengi ya vita hupiganwa mpaka mmoja afe(To the Death), Kuangamiza, kutokomeza, kupoteza kabisa. Hii ni tofauti na mapambano ambapo ni kama michezo tuu ya kimaisha kama vile michezo ya mipira n.k.

Sio kila vita yapaswa kupiganwa mpaka kifo, ni baadhi tu.

Imekuwa ni kawaida kwa watu kusema maisha ni magumu, ni kweli maisha ni magumu kwani ni vita. Weka kwenye akili kuwa kila vita ni ngumu, na kamwe hakujawahi kuwa na vita rahisi. Watu wengi wanaosema maisha ni magumu ni kutokana na kuwa wengi wao hawajui wapo kwenye ulingo wa vita. Wao hujiona wanaishi tuu kwa bahati lakini wanaowapiga wanawapiga kwa makusudi kwani vita ni makusudi na wala sio Nasibu.

Maisha yanakuwa magumu, na hasa nikitumia neno vita ili nieleweke vizuri kwa sababu kuna mambo bado watu hatujayaelewa na kama tumeyaelewa basi hatuyatilii Maanani.

Maisha ni yako pekee yako sio ya mtu mwingine. Hakuna atakayepigana kwa ajili yako. Wewe ndiye unauamuzi wa kushinda au kushindwa sio mtu mwingine. Kumtegemea mtu kwenye maisha/vita ni kumpa ushindi huyo unayemtegemea na kujinyima ushindi kwa uzembe. Pigania maisha yako, pigania familia yako. Usikubali kupigiwa vita na mtu, usimtegemee mtu kwenye vita, utashindwa asubuhi na mapema.

Usikubali kupigania mtu vita yake kwa sababu hakuna atakayepigania vita yako. Kwa kadiri unavyopigania wengine vita zao ili washinde ndivyo unavyoruhusu kushambuliwa na kuangamizwa.

Jipiganie wewe mwenyewe, kisha familia yako na hapa namaanisha, Baba, mama na watoto wako. Hao ndio watu wako, hiyo ndio timu yako. Usipopigana kwa ajili ya familia yako basi hesabu maumivu, hesabu umeshindwa vita hata kama unajiona umshindi kwa wakati huu lakini ushindi wako ni wakitambo tuu. Jinsi unavyoipigania familia yako ndivyo unavyojipa uhakika wa kushinda hasa katika dakika za lala salama, dakika za majeruhi naam mwisho wa vita. Familia ni mke, mume na watoto wao. Kuwahusisha watu wengine ni kujidanganya. Ukiiweka familia yako mbele kuliko jambo lolote basi upo katika nusu ya ushindi wako.

Kwenye Maisha naam ndio Vita kwa mujibu wa andiko hili, lazima ujue jambo moja muhimu kabla hujaingia katika vita yoyote ile. Kabla hujapigana na yeyote yule lazima ujue jambo moja la lazima. Nalo ni WEAKNESS POINT. Ukishajua sehemu iliyodhaifu kwa adui yako basi ifanye kuwa hiyo ndio Target yako. Usipige popote pale bali shabaha yako iwe hapo kwenye weakness point. Usipigane kwenye vita yoyote ile kama hujui Weakness point ya adui yako. Ni bora ujisalimishe kwa muda ukiwa unasoma mchezo kabla hujaingia kwenye Vita na adui yako.

Jambo moja la uhakika ni kuwa kila adui na kila mtu ana weakness point yake. Na mara zote washindi ni wale waliojitahidi kuficha weakness point zao kwa adui zao huku wao wakiwa wameshazijua weakness za adui wao. Huwezi mpiga adui na kumuangamiza kwa kubahatisha huo ni uongo. Adui anapigwa baada ya kumfahamu na kujua udhaifu wake.

Udhaifu wa mtu au wa adui upo zaidi kwa kile anachokipenda zaidi au kile ambacho hakipendi zaidi. Watu wote wenye akili duniani na mashujaa wa vita hawakuwa mashujaa kwa sababu ya kujua kupigana hasha! Bali kwa kuweza kuficha mambo wayapendayo zaidi au wayachukiayo zaidi kwani huko ndiko walipo wadhaifu.

Mashujaa wote waliopigwa na kuangushwa walishindwa kuficha mambo wayapendayo sana au wayachukiayo mno hali iliyopelekea adui zao kuyatumia mambo hayo kuwadhuru na kuwaangamiza. Kwa mfano mashujaa wote waliopenda kufanya ngono na wanawake wazuri walijikuta katika anguko kuu, hao hao wanawake walitumiwa na adui kuwaangamiza. Kama vile Samson alivyoangamizwa na Wafilisti kisa Mrembo Delilah.

Maisha ili uyashinde yakupasa ujue ndani ya jamii yako ni kitu gani kinapendwa kuliko kitu kingine, ukishakijua basi lenga humo humo, usipoteze nguvu kufanya mambo mengine, hutafanikiwa zaidi ya kupoteza muda wako bure. Ichunguze jamii yako, chunguza taifa lako, angalia weakness point ipo wapi, ukishaijua basi iweke ndio target yako. Maisha hayaaribiwi, Vita haijaribiwi ati unaenda bila kujua adui yako ni dhaifu kwenye nini na utumie silaha gani kumuangamiza.

Ndoa ni vita, ili uoe mwanamke mzuri na anayekupenda basi sharti upigane kwenye vita vya mapenzi. Ili uolewe na mwanaume mzuri unayempenda basi lazima upigane. Wanawake wengi hupenda wanaume wenye utajiri, wazuri na warefu lakini kuingia kwenye vita ndio hawataki.

Wanaume wengi tunapenda wanawake wazuri lakini hatutaki vita, wewe unaoa mke mrembo alafu hutaki atongozwe, Umelogwa kweli wewe! Hiyo ni Vita. Mke mzuri ukimpata jua umetangaza vita, mume mzuri ukimpata jua umetangazaa vita. Vita ni vita Muraa! Ukizembea unapasuka, unaangamia hivi hivi unaona.

Kazi nzuri ni Vita, kuna watu wapumbavu sana, huwezi pata kazi nzuri yenye heshima na mshahara mnono kilaini, lazima usote lazima upigane. Tena kuipata ni vita namba moja, vita namba mbili ni kubaki kwenye kazi hiyo miaka yote. Hapo ndipo kazi ilipo. Utapigana na kila vita hata ambazo hujatarajia.

Hakuna kazi nzuri isiyo na Fitina, majungu, uchawi na ulozi, zengwe, na hata kutengenezewa ajali kama sio kuuawa. Na hiyo ndio vita yenyewe.

Narudia, iwe ni Vita ya ndoa au vita ya kazi, jambo moja la muhimu kabisa, hakikisha unajua weakness point ya watu wote wanaokuzunguka eneo la kazi, zingatia pia adui hatokagi mbali na ndio maana nimekuambia hakikisha wanaokuzunguka unawafahamu vizuri kabisa na madhaifu yao. Kisha wewe shabaha(Target) yako kubwa iwe huko. Usiishi kama mjinga kwamba kwa vile wewe huna time na mtu basi na watu hawatakuwa na time na wewe, huo utakuwa ni ujinga.

Yaani uwe na kazi nzuri alafu watu wasiwe na time na wewe, hahaha! Unachekesha kweli. Yaani uwe Uoe mke mzuri, Tako tako, Paja paja, Nyonga nyonga, mtoto mkali alafu ati watu wasiwe na time na wewe, hhahahah! Au uwe umeolewa na mume mzuri, mwenye pesaa na sifa zote alafu utegemee wanawake wenzako wasiwe na time na wewe Sirius kweli! Huko ni kujidanganya.

Huwezi ingia vitani alafu ukadhani kuwa kwa vile wewe huwashambulii maadui ukadhani wao hawatakushambulia, utapigwa risasi ukafie mbele, kwa upumbavu wako.

Mwajeshi mzuri ni yule anayejifunza mapigano ya kila namna; Lakini mwanajeshi bora na mshindi ni yule anayejifunza kwa wepesi udhaifu wa adui yake na huyo ndiye hushinda vita.

Ukipagana na adui usiyemjua vizuri udhaifu wake utatumia muda mwingi kupigana tena anaweza kukushinda kwa urahisi kwa sababu utakuwa unapiga bila Target. Lakini ukishajua weakness point yake basi vita utaimaliza mapema mno. Na hapa ndio umuhimu wa UJASUSI unapojitokeza.

Maisha ni Vita, na Kushinda vita sio wingi wa silaha bali ubora wako katika fani ya UJASUSI.

Huwezi kujua weakness point bila kuwa mzuri katika kukusanya taarifa, naam mbobevu wa Ujasusi.

Nini kipo wapi, kina nani wanakimiliki, kina thamani gani, utakipata vipi kwa muda gani?

Mwisho; Information is a power
Penda nchi yako, kuwa mzalendo.

Ulikuwa nami;

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Dar es salaam
 
Find weakness ya mfumo na mazingira
Ngoja nikupe mfano, ...
Nimeajiliwa na shirika nje ya nchi nalipwa mshahara mzuri sana na nilikuwa nawekeza hapa nchini, baadaye serikali imeniona na kunitaka kuja kuijenga nchi, nilipofika nikapewa ukurugenzi mkuu wa taasisi ya fedha.

Katika muendelezo wa kazi hapa nchini mshahara niliokuwa nalipwa ukawa mdogo kulinganisha na ule wa taasisi ya nje ya nchi, so uwekezaji wangu ukasua sua sana.

Baadaye nikapunguziwa zaidi mshahara kisa niwe mzalendo, mwishowe nikasimamishwa kazi kuwa ni mwizi!.

☝️Hapo tunaweza sema ni madhaifu ya mfumo au mazingira?
 
Ngoja nikupe mfano, ...
Nimeajiliwa na shirika nje ya nchi nalipwa mshahara mzuri sana na nilikuwa nawekeza hapa nchini, baadaye serikali imeniona na kunitaka kuja kuijenga nchi, nilipofika nikapewa ukurugenzi mkuu wa taasisi ya fedha.

Katika muendelezo wa kazi hapa nchini mshahara niliokuwa nalipwa ukawa mdogo kulinganisha na ule wa taasisi ya nje ya nchi, so uwekezaji wangu ukasua sua sana.

Baadaye nikapunguziwa zaidi mshahara kisa niwe mzalendo, mwishowe nikasimamishwa kazi kuwa ni mwizi!.

☝️Hapo tunaweza sema ni madhaifu ya mfumo au mazingira?

Huijui nchi yako Mkuu?

Ikiwa viongozi wanaficha pesa zao nchi za nje vipi wewe mwenzangu na miye?
 
Katika maisha vita vina manufaa mengi jitahidi uwe na vita ata vita bandia. Unaishije bila vita, jiweke tayari kwa vita muda wowote jiandae kushambuliwa na kushambulia.

Hii falsafa imenisaidia sana kufanya maadui waniogope kwa kuwa muda wote nakuwa tayari kushambulia na kushambulia.

Mbinu ingine ni kumfanya adui azani upo pamoja upande wake au unakaribia kuaga pambano kumbe unajipanga kwa mashambulizi makali.

Mwisho kwenye vita mimi huanza na silaha kubwa kuokoa muda na kelele. Nikishaamua kupambana sijali madhara baada ya pambano muhimu ni ushindi wa haraka na kuendelea na vita vingine
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom