Je, wajua mshahara wa "Flight Attendant" wa Emirates?

Sijamlinganisha flight atendant wa Emirates na wa ATC bali mkurugenzi mkuu wa Tanesco na Tanapa kulipwa mshahara mdogo... ndo shida mkuu.......
Kwa hali ya kiuchumi ambayo watu wanatembea 50km kuchota maji kwenye ndoo, mshahara Wa 15,000,000/= ni mdogo? au unaongelea mshahara gani huo mdogo...
 
mbona pesa ndogo sana! haifiki hata pato la wastani la mkazi wa UAE. sema ukiileta kibongo inakuwa habari nyingine.
 
Pilots average monthly salaries: Emirates...!!

Captain... $ 25K ~ $32K

First Officer... $ 15K ~ 25K...

Duuuh...!!! Pilots wanakula hela sana jamani... kaaah..!!
Unadhani kurusha ndege mchezo? Ni kazi ya hatari ile. Ukipata ajali ndugu zako hata maiti hawataiona
 
Kwa hali ya kiuchumi ambayo watu wanatembea 50km kuchota maji kwenye ndoo, mshahara Wa 15,000,000/= ni mdogo? au unaongelea mshahara gani huo mdogo...
Sijui kama umeajiliwa na una elimu ya kutosha... na unajua majukumu ya wakurugenzi wakuu.... mshahara wa 15m kwa mkurugenzi mkuu ni mdogo hasa kwa taasisi kubwa kama Tanesco/tcra/tanapa.... fanya utafiti. ..
 
Hii ni kwa mtazamo wako.Hakuna mahali niliposema nilimuona mjinga.Wakati wewe hapa JF unaonekana "kukasirika" kwa hiyo kauli yangu,yule dada ni moja kati ya marafiki wangu wakubwa wa familia yangu.Umetafsiri tofauti sababu umeona hii kauli ikiwa kwenye "fasihi Andishi",laiti ungeisikia katika "Fasihi Simulizi" ungeona "tone" yangu na "facial expression",hivyo usingahamaki zaidi ya kunipa ushirikiano wa kauli yangu
Kama hukumuona "kama mpuuzi flani hivi" ni nini kilichokufanya ufadhaike baada ya yeye kuja kukusemesha kiswahili? Ni kutokana na mafunzo tu aliyopewa ndio maana aliendelea kukusikiliza na si ajabu pia alikupa darasa la kutosha lakini hujasema hapa!
All in all nilitaka tu tuwekane sawa kuwa kila mtu analo kabila lake na lugha yake hivyo si vizuri kumsema mtu(vibaya) kwa sababu tu haelewi unachokisema na tuelewe pia hata kama alitenda kosa hawezi kujutia wala kujirekebisha kwa sababu haelewi kunachosemwa dhidi yake.
 
kuna siku nilisafiri na qatar.. dar to doha ndege ilikuwa haijajaa kabisa siku hiyo. abiria wachache sana.. nikapiga story sana na flight attendant mdada wa kikenya anaejua kiswahili vizuri sana amewekwa special kuhudumia abiria wa kitanzania wasiojua lugha za kugeni (nafasi ya mtanzania hii ila mkenya kadaka fursa)

tukawa tunataniana kwenye story kuhusu salary zikoje anazopata... akanizingua nizingua ila akaniambia around usd 4000 hapo bado ma bonus ya kukaa angani. na ni 23 tu hako kadada

Nahisi hata namba za simu mlipeana
 
Mkuu vipi ulifanikiwa kupata contact zake?
 
Kama hukumuona "kama mpuuzi flani hivi" ni nini kilichokufanya ufadhaike baada ya yeye kuja kukusemesha kiswahili? Ni kutokana na mafunzo tu aliyopewa ndio maana aliendelea kukusikiliza na si ajabu pia alikupa darasa la kutosha lakini hujasema hapa!
All in all nilitaka tu tuwekane sawa kuwa kila mtu analo kabila lake na lugha yake hivyo si vizuri kumsema mtu(vibaya) kwa sababu tu haelewi unachokisema na tuelewe pia hata kama alitenda kosa hawezi kujutia wala kujirekebisha kwa sababu haelewi kunachosemwa dhidi yake.
Ni kweli minnilijifunza tu kuwa sio vizuri kumsema mtu,lkn sikuwa namsema kwa nia mbaya zaidi ya kuwa katika maongezi na watoto
Yeye mwenyewe alikiri nilichokisema ndio maana hakuna lolote baya kati yetu.Tuufunga mjadala,nimekuelewa na wewe nielewe pia
 
An Airhostess is just a mere barmaid....sio kazi ambayo mimi ninatamani kijana wangu aje kuifanya,na moja ya njia ya kumfanya isiwe kazi anayotamani ni kumpa ukweli wa kazi yenyewe,ili asidhani kuwa angani na kuhudumia watu katika ndege ni kazi "exceptional" sanaaa.

Huwezi kutafsiri mode ya malezi yangu kwa meseji ya mistari 10+ hapa JF,nilikaa na yule dada zaidi ya masaa 4 juu,alinifundisha mengi juu ya kazi ya Cabin Crew na madhila yake,kuna mdau humu amegusia jinsi hawa wadada wanavyoenda kwenye destinations tofauti wakiwa na marubani tu na kuishia kuwa "kitoweo".Jambo hilo sijaanza kulisema mimi,Frequent Flyers wote humuweka "Airhostess" katika kundi hilo.

Hata yeye alinambia ana malengo ya kufanya kazi hiyo kwa miaka 5 then aingie kwenye biashara zake,anahisi ni kazi isiyompa heshima na haimpi nafasi ya kuijenga familia na kuwaweka sawa watoto wake.Naona umechukulia juujuu hii story,nilimweleza mwanangu kwa kirefu sana,nimesema tu hayo maneno ya bar-maid sababu ndio yaliibuwa mjadala kati yangu na dada

Alinitumia mimi kupata kiwanja Kange-Tanga kati ya vile viwanja vilivyotangazwa na Jiji la Tanga,amejenga Kange na Insha'Allah ana mpango wa kuja kuishi Tanga akifanya biashara zake.Aliniambia hicho nilichoongea ndicho kinachowakumba kama changamoto katika kazi yao.Anatumia nafasi ya kuwa attendant wa Fly Dubai kusafirisha mizigo yake bure toka Dubai na kuleta Tz kwa ajili ya biashara zake.[/QUOTE
Ninachotaka kukufahamisha ni kwamba hukumjibu mtoto sawa hata kama ni ukweli..UNAWEZA UKAFIKISHA UKWELI NA FACT ZOTE BILA KUONYESHA NENO LENYE KUSHUSHA AU KUDHARAU KAZI YA MTU. Hata kama wale wanahudumia watu huwezi mshusha level ya barmaid huko wanakokunywa mbege, hao unaowaita ma barmaid wana maisha mazuri na majumba mazuri kushinda hao unaowapa heshima, wenye akilia wamejua kujijenga kwahiyo kazi ya ubarmaid wa kwenye ndege...NA KUHUSU WAO KUWA CHAKULA CHA MAPILOT NIKUPENDA TU, Hata masecretary na manures na madr. WANAKULANA TU, HIYO POINT TOA KABSAA, SIO KAMA MAPILOT WANAWABAKA NA UKUMBUKE PILOT NI MFANYAKAZI KAMA MFANYAKAZI MWENGINE HANA UWEZO WAKUMFUKUZA MTU KAZI KWAHIYO WANA UWEZO WA KUWAKATAA HAO MAPILOT Ukiona mtu kakubali ni tabia yake au ni mapenzi kama mapenzi mengine watu wanavyokutana makazini.

HATUJAKATAZWA KUWAELEZA WATOTO UKWELI ILA IPO NJIA SAHIHI, NAMNA HIYO UNAMFUNZA MTOTO MAJIVUNO, DHARAU NA KEBEHI Kitu ambacho sio sifa nzuri, mfafanulie kwa fact angekuelewa tu. NA KUHUSU KUJENGA HATA SISHANGAI WANAJENGA MAJUMBA YA MAANA HASA , SISHANGAI KAMA NA HUYO KAJENGA, NA WENGI HUFANYA KWA MALENGO NA WANAWEZA WAKAJA WAKAWA NDIO WAFANYABIASHARA WAKUBWA WAKAJA MUAJIRI MWANAO AMBAE WAKATI HUO SIJUI ATAKUWA NDIO USHAMSOMESHA AMEKUWA NANI HA HA HA HA Mungu amuongoze mwanao, pole kama nimekukwaza.
 
Hujanikwaza ndugu..humu tunajadiliana na kubadlishana mawazo
Tunajifunza toka kwa kila mtu kwa maandishi yake na maneno yake
Nimejifunza pia toka kwako...Asante kwa mjadala na changamoto!!Hakuna binadamu aliye kamili 100%
Life is experience,and experience is all about long run process of learning!We are still learning
 
Back
Top Bottom