Mkuu
shaurimbaya wakati ule FLY DUBAI inaanza safari zake kati ya Dubai-Dsm-Znz-Dubai walikuwa na nauli ya offer,nilitumia nafasi hiyo kusafiri na familia kwenda kuosha macho duniani
Ndege haikuwa na abiria wengi,tena nakumbuka ilikuwa flight #FN675...njiani humo wale flight attendant walikuwa wanazunguka huku na huko wakituhudumia
Mwanangu mmoja akaanza kuniuliza,baba hivi hawa huwa wanasomea wapi?nikamwabia hawa wanasoma wapi hawa ni kama bar maids tu,tofauti yao ni kuwa hawa ofisi yao ipo angani na inahudumia wateja classic.
Loooh!!kumbe yule dada anayetuhudumia ni dada wa kimanga,Mama Mpemba na baba Mmanga wa Mombasa,anaongea Kiswahili fasaha,na amekulia Unguja baadae akaenda Oman.Muda wote anatusikiliza tu yupo kimyaaa!!Tukapiga stori weeee na familia pale,ye anajidai haelewi kabisa Kiswahili.
Baadae tumekaa yule dada akaja,akasema "Vipi Kaka nikuletee kinywaji gani?Maana sisi ndio mabar maid wenyewe"....Loooh yani nilitamani kuingia uvunguni mwa seat,lkn dada alikuwa fair sana,tulipiga sana story akanieleza jinsi alivyopata kazi Fly Dubai,jinsi watu wa Pemba,Unguja na Tanga wenye jamii ya kiarabu walivyojaa kwenye kazi za mashirika ya Mashariki ya mbali.
Dada anang'aa huwezi dhani "mswahili"....tulipiga story hadi pale Dubai akatusaidia kufanya connection