Je, wajua kuwa mazungumzo yetu na Barrick ni mazungumzo tu? Mwenye uamuzi wa mwisho ni Acacia!, Kwanini hakushirikishwa?!. Je, Tutalipwa?.

Mkataba uliyokuwapo ulikuwa unaruhusu kusafirisha makinikia, haikuwa kosa kwao bali la waliopitisha huo mkataba.
Uchunguzi wa akina Prof Mruma ulitakiwa ufanyike pakiwepo wawakilishi wa Barick pamoja na mtu wa tatu ambae ataangalia na kuthibitisha kuwa, ulifanyika kwa kufuata taratibu za kitaalamu. Uchunguzi watz watupu ulikosa nguvu na hata hoja. Huwezi kuishitaki Barick popote kwa matokeo yenu wenyewe ya uchunguzi.
Propesa Kalamagamba mwanasheria nguli alikuwa analijua hilo kama Lissu na wanasheria wengine walivyolifahamu.
Kwa nini "Mzalendo" Propesa na wengine waliyo karibu na Jiwe, waliamua kutoa matumaini hewa kwa watz, ni jambo ambalo linasikitsha.
Kwa mitindo ya aina hii Tz haitokuja kusogea mbele kimaendeleo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa bahati mbaya kwenye suala hili la madini, tumeingia kichwa kichwa katika kila sekta. kuanzia sheria mpya tulizotunga, uzuiaji wa makinikia, uundwaji wa zile kamati mbili, na hatua zilizochukuliwa, na hata katika hayo "mazungumzo" na Barrick. kote huko tumekwenda kichwa kichwa na tumeangukia pua.
Siku ambayo Tundu Lissu alipigwa risasi, asubuhi alikuwa bungeni na alitoa hoja nzito kuonesha jinsi zile sheria zilizopitishwa kuhusu sekta ya rasilimali zetu ikiwemo madini, zilivyokuwa za hovyo.

Tundu Lissu ameshughulika na hawa jamaa wa madini kwa miaka mingi. ni mzoefu sana tu. na katika mengi ambayo amekuwa akitahadharisha miaka yote hii, amekuwa sahihi. cha kushangaza ni kwamba badala ya serikali kumshirikisha, hata kama ni mtu wa upinzani, kama alivyomshirikisha Spika Anne Makinda enzi zile katika uwanja wa sheria, anaonekana ni adui. sasa serikali iko kwenye CUL DE SAC, na hatujui tunatokaje hapo bila kuaibika zaidi.
 
Ngoja wafanye kazi zao, wao ndio wanajua yasirini na wazi . Sisi walalahoi tusubiri matokeo. Yakiwa chanya tunamshukuru Mungu yakiwa hasi tutachukua "lessons learned" hata tusipojifunza kitaifa tunaweza kujifunza ktk level za familia au mtu mmojammoja.
 
Simply watakwambia yalikuwa maagizo toka JUU, na hao wa juu wanalindwa na Katiba.
Ndio maana TZ haiwezi kuwa na kiongozi smart, cuz unajua una kinga na issue zote zikifika kwa mkuu mstaafu ndio inakuwa "sky is the LIMIT"
 
The dic is IN long time, tutulie watule......Japo mi simo ahahaahahaaa
 
Nilimshangaa sana Kabudi aliposema kuwa wao (Barrick) walikuwa 24 lakini sisi tulikuwa 5, na tukafanikiwa.

Ukisikia mwanafunzi mbumbumbu anasema mtihani ulikuwa rahisi sana lakini wenye akili wanasema mtihani ilikuwa mgumu, ujue kuwa yule mwanafunzi mbumbumbu, kuna uwezekano mkubwa, hakuelewa hata kilichoulizwa.

Naikumbuka sehemu ya hotuba ya Rais wa Barrick mwaka 2001:

Barrick has realized overall profit throughout since it was started. While other companies were collapsing, Barrick kept on fluorishing. It is not because of the gold reserves, money or equipment it is possesing but because of the people we have.

In short ni kuwa, hakuna kishika uchumba wala kodi yoyote tutakayolipwa. Madai yetu yalijengwa kwa kutumia taarifa za uwongo. Huwezi kuutegemea uwongo ili kushinda.

It was for political popularity from brain lows. There we have got it.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Man watu werevu tulimuelewa TL huwa hakurupuki wala kuropoka, he does his home work thoroughly, he is a policy wonk and a work holic! Na zaidi ya hapo yule ni "Nabii"; (binadamu wa kawaida how do you survive an assasins bullet tena 30+?!)
Japo wakati utaongea, lakini pia Nji hii itamkumbuka TL both akiwa hai na akishatangulia mbele ya haki! Get well soon TL
 
Kuna mtu kashalipwa 'watch out' Hakuna mazungumzo business as usual!!
 
KIBST pamoja na maongezi mazuri yakupendeza umesahau kitu kizuri haukutaka kukisema..Hatujawahi kuibiwa hata na MTU mmoja kupitia uwekezaji..TUMEJIIBIA wenyewe kupitia MIKATABA ya uwekezaji. Haya yakifanyika serikali hii ilikuwepo. Uthubutu wa Mwenyekiti wetu ni pale alipobadili sheria kujaribu kuzuia..Nawasilisha
 
Mara nyingi ukweli huwa haujifichi, na ukweli hukuweka Huru.
Report hazikufanyika huru kisayansi bali kisiasa. Namna ya uwasilishaji tuu kwa muelewa wa mambo ulileta ukakasi, matangazo yalivyokuwa nayo pia ilileta ukakasi, na report ya pili Mwenyekiti wake alikuwa anatetemeka na hajiamini means kuna yaliyotamkwa si sahihi.
Mzalendo yeyote hatapenda kuonea Kama asivyopenda kuonewa. Je, Kama maprof Wetu waliyoyaona ni kweli kwanini wasitafute Mchunguzi huru wote Serikali, Barick na Accacia wampe namna ya kuchukua sampuli na namna ya kupima majibu yatolewe ili ijulikane na kukubalika kwa wote, hapo watakosa cha kusingizia then serikali inataifisha kila Kituo chao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…