Mkuu tatizo la baadhi ya wasomi wetu muungano lazima uandikwe kwa kizungu kilichojaa maneno ya kilatini na kukubalika na walimu wa kizungu waliowafundisha darasani kuongea kizungu.
Babu yangu na bibi na baba yangu na mama yangu waliungana kuoana bila kuandikiana popote wala kusainiana popote lakini miungano yao ilidumu vizuri.
Muungano wowote ule uwe wa kuandikwa au kutoandikwa uwezeshe maisha ya watu kwenda hayo mambo mengine ya kilatini sijui DE JURE na DE FACTOR yanafaa kuyaongelea mtu akishalewa pombe za kizungu.
Muungano huu wa Mdomo ni
muungano wa Ajabu sana uliosalia Duniani,kwani muungano huu licha ya
kudumu kwa miaka 50 ,ni muungano wenye Ukiritimba wa ajabu,mianya ya
Mafisadi kujilia pesa za Umma kiulaini kwa kisingizio cha kumaliza kero
za muungano, kero za muungano na mladi wa watu wachache ambao hawataki
Amani ZNZ ili fungu la kumaliza Kero liendelee kupewa bajeti na wao
huvuna hizo pesa kirahisi,hao watu hawataki kusikia Serikari 3 Maana
zitakimbiza Ulaji wao.
Pasco uhalali wa mkataba upo mikononi mwa waliokatibiana na si vinginevyo, ndo maana UN hawana na hawakuwa na jinsi ispokuwa kuheshi makubaliano yetu "hata kama haikidhi matakwa ya sheria ya mikataba"
kwa maan hiyo ondoa porojo zako hapa.
Wewe mwenyewe umethibitisha na kuhitimisha kuwa either tz iliundwa kwa de factor au de jure zote ni halali. Sasa tujadili nn tena hapa
Tutayajua mengi mwaka huu. Kweli hakuna uongo wa kudumu ila uko ukweli wa kudumu hata uufiche vipi.
Aliyetufikisha hapa ni Mwinyi na Kikwete kutokana na udhoofu wao.
.
- Ili makubaliano yoyote yaitwe mkataba ni lazima yawe na sifa kuu 4 za mikataba, zinazoitwa vipengele, na kikikosekana kimoja wapo cha sifa hizo, then huo sio mkataba bali ni makubaliano tuu ambayo nayo ni halali. Makubaliano hayo ya Muungano hayana zile sifa kuu 4 za mkataba. Jee sifa hizo kuu 4 za mkataba ni zipi?!. (Hii sio thread ya contents za Hati za Muungano bali presence ya hati hizo). Ili kujua kwa nini hati za muungano sio mkataba bali ni makubaliano, then itakubidi unitembelee hapa!- Jee Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano Tuu!.
Sasa nimeanza kuelewa kwanini CUF (ZNZ) na UAMUSHO wanang'ang'ania Muungano wa MKATABA. Wakati sisi Watanganyika upeo wa kuona mambo yetu hauzidi urefu wa pua zetu. Wenzetu Wazanzibari they are miles away. Masikini Tanganyika!
Kwa tulipofikia mabadiliko ni muhimu maana Muungano umeshakuwa na dosari watu hawaoni manufaa wanaokazania ni wezi wanaonufaika kwa jina la muungano
Wasemaji wa Tanganyika ndio hao hao wanaonufaika kupitia mapungufu na kasoro za muungano hawapendi serikari moja au tatu wanajua zitafichua mengi na wao kuumbuka sasa wamekituma kizee Shivji kianzishe mkanganyiko ili waendelee kula pesa mpaka watu kuja kushituka baadae watakuwa tayari wameshiba na kuja na mbinu zingine za kuwahadaa watanganyika.Sasa nimeanza kuelewa kwanini CUF (ZNZ) na UAMUSHO wanang'ang'ania Muungano wa MKATABA. Wakati sisi Watanganyika upeo wa kuona mambo yetu hauzidi urefu wa pua zetu. Wenzetu Wazanzibari they are miles away. Masikini Tanganyika!