Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,466
- 113,551
Wanabodi,
Wakati mchakato wa kelekea kwenye Katiba Mpya unakwenda vizuri na sasa ni wazi tunaelekea kwenye serikali tatu, baada ya miaka hii 50 ya Muungano uliozaa Taifa la Tanzania, tufike mahali tujiulize hivi Taifa letu la Tanzania lipo kisheria (De Jure) au kimabavu tuu (De Factor)?!.
Andamana nami katika ziara hii fupi kukufanyia utambuzi wa uhalali wa Taifa la Tanzania kisheria ili kuwa taifa de jure, na pia kulijua taifa the facto.
https://www.google.com/url?sa=t&sou...cQFnoECBgQAQ&usg=AOvVaw1rq5EAFapufDcpElW4fsdJ
Asanteni na Happy New Year!
Pasco.
Wakati mchakato wa kelekea kwenye Katiba Mpya unakwenda vizuri na sasa ni wazi tunaelekea kwenye serikali tatu, baada ya miaka hii 50 ya Muungano uliozaa Taifa la Tanzania, tufike mahali tujiulize hivi Taifa letu la Tanzania lipo kisheria (De Jure) au kimabavu tuu (De Factor)?!.
Andamana nami katika ziara hii fupi kukufanyia utambuzi wa uhalali wa Taifa la Tanzania kisheria ili kuwa taifa de jure, na pia kulijua taifa the facto.
- Ili taifa lolote liweze kuwepo, ule tuu uwepo wake wa being, likiwa na eneo na mipaka inayotambulika, ni tayari taifa hilo lipo, litambulike au lisitambulike, linakuwa lipo tuu, ila lisipotambulika, linakuwa japo lipo, ila ni lipo lipo tuu!. Hivyo Tanzania kama taifa, japo lipo kuhalali, kisheria Taifa la Tanzania lipo lipo tuu!.
- Ili taifa lolote liwepo kihalali kwa kisheria (de jure) au isivyo kihalali kisheria lakini lipo (de factor) taifa hilo lazima lijitambulishe Umoja na Mataifa na umoja huo ulipitishe rasmi kama Taifa.
- Tanzania nayo pia ilipitishwa rasmi kule UN kama Taifa huru, la Jamuhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mnamo tarehe 14 May, 1964 kufuatia kuwasilishwa kwa taarifa rasmi ya maandishi, Note Verbale toka kwa Balozi wa Tanganyika kwenye Umoja wa Mataifa, wakati huo, Chief Arasto Mang'enya na kuitambulisha United Republic of Tanganyika and Zanzibar. Wakati huo, jina la Tanzania halijaanza kutumika. Mwezi June Balozi Mang'enya aliteuliwa rasmi kuwa balozi wa kudumu wa Jamhuri ya Tanganyika na Zanzibar kwenye Umoja wa Mataifa, na mwezi September ndipo akawasilisha rasmi hati zake za utambulisho na jina rasmi la United Republic of Tanzania kuwasilishwa UN.
- Hii ni taarifa rasmi ya UN kuhusu kuungana kwa mataifa -MERGER OF MEMBER STATES, during the period under review, the issue of the merger of Member States arose in the United Nations in connexion with the formation of the United Republic of Tanganyika and Zanzibar, later called the United Republic of Tanzania. Tanganyika and Zanzibar, which had been admitted in the United Nations since 14 December 1961 and 16 December 1963 respectively, informed the Secretary-General by a note verbale dated 6 May 1964 of the following:
- Hiki ndicho kilichokuwemo ndani ya Note Verbale ile
" . . . the Republic of Tanganyika and the People's Republic of Zanzibar were united as one Sovereign State on 26 April 1964, under the name of the United Republic of Tanganyika and Zanzibar and under the presidency of Mwalimu Julius K. Nyerere. A copy of the said Articles of Union is enclosed herewith.
"The Secretary-General is asked to note that the United Republic of Tanganyika and Zanzibar declares that it is now a single Member of the United Nations bound by the provisions of the Charter, and that all international treaties and agreements in force between the Republic of Tanganyika or the People's Republic of Zanzibar and other States or international organizations will, to the extent that their implementation is con- sistent with the constitutional position established by the Articles of Union, remain in force within the regional limits prescribed on their conclusion and in accordance with the principles of international law." - On 14 M a y , the Secretary-General, at the request of the Government of the United Republic of Tanganyika and Zanzibar, communicated the note to all States Members of the United Nations, to the principal organs of the United Nations and to the subsiding organs of the United Nations to which Tanganyika or Zanzibar had been appointed or admitted, and to the specialized agencies and to the International Atomic Energy Agency, by a note verbale which included the following statement:
- Hili ndilo Tamko la Katibu Mkuu wa UN wakati huo, kulitangaza rasmi taifa la Tanganyika and Zanzibar (Tanzania) "The Secretary-General is taking action, within the limits of his administrative responsibilities, to give effect to the declaration in the attached note that the United Republic of Tanganyika and Zanzibar, is now a single Member of the United Nations bound by the provisions of the Charter. This action is undertaken without prejudice to and pending such action as other organs of the United Nations may take on the basis of the notification of the establishment of the United Republic of Tanganyika and Zanzibar."
- Hivyo msingi mkuu wa Taifa la Tanzania ni zile hati ambazo zimeelezwa kuwasilishwa na lile tangazo la Balozi, swali ni jee Hati hizo, ziliwasilishwa?, kwanini hazikuwasilishwa?, bila hati hizo Tanzania bado ni taifa?. Uhalali wa Tanzania kama Taifa bila hati ukoje?.
- Wakati wa Kipindi cha Rais Benjamin Mkapa nilibahatika kwenda UN, na nikaenda ubalozi wetu kunusa nusa tuu kama hizo hati zinaonekanika, nikashindwa kufuatia urasimu fulani. Wakati wa Kipindi cha JK nikaenda tena pale pale ubalozini, this time receptionist ni shemeji yetu (mke wa member mwenzetu wa jf), nikaomba appoinment kumuona balozi bila mafanikio!. Hata hivyo nilipokwenda maktaba ya UN, Note Verbale ile ipo, ila hakuna hiyo attachment ya Articles of Union!. Hivyo swali la kujiuliza jee kuna nini kuhusu hizi articles hadi zisiwepo?!.
- Ukweli ni kuwa au hiki kitu kinaitwa Mkataba wa Muungano, "Articles of Union" sio mkataba halali, (Contract) bali ni makubaliano tuu "agreement" ya Muungano, tofauti kati ya Mkataba (Contract) na Makubaliano (Agreement au MoU) ni kuwa mkataba uko kisheria zaidi una vipengele vya kisheria na unatawaliwa na sheria, (legal binding) wakati makubaliano yanategemea mapatano tuu na maelewano, hakuna legal binding ya mapatano japo yakisajiliwa kisheria yana legal binding ya kimapatano na sio kimkataba!. Jee kwa nini hizi "Articles of Union" naziita ni mapatano tuu na sio mkataba?!.
- Ili makubaliano yoyote yaitwe mkataba ni lazima yawe na sifa kuu 4 za mikataba, zinazoitwa vipengele, na kikikosekana kimoja wapo cha sifa hizo, then huo sio mkataba bali ni makubaliano tuu ambayo nayo ni halali ila sio binding kisheria.
- Makubaliano hayo ya Muungano yaani zile Hati za Muungano (articles of the Union), hazina zile sifa kuu 4 za mkataba wa kisheria (legal binding), hivyo Wanzanzibari wakiamua kuyavunja makubaliano hayo wakati wowote, they can just walk out, kwa sababu siyo legal binding!.
- Jee sifa hizo kuu 4 za mkataba wa kisheria ni zipi?!. (Hii sio thread ya contents za Hati za Muungano bali presence ya hati hizo). Ili kujua kwa nini hati za muungano sio mkataba bali ni makubaliano, then itakubidi unitembelee hapa!- Jee Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kilichopo ni Makubaliano tuu?!.
- Kufuatia uwezekano wa Taifa la Tanzania kuwasilishwa kwa NV tuu kule UN, bila ya Mkataba wenyewe wa Mungano, hivyo ile nchi ya Tanzania iliyopo UN ni Tanzania De Facto na sio Tanzania De Jure. Tanzania bado ni nchi, iwe de jure au de facto bado ni nchi!. Yaani inchi yetu Tanzania, imekalia kiti chake cha UN kama nchi De Jure, kumbe infact Tanzania sio nchi De Jure, bali ni nchi De Factor, hivyo uanachama wenu UN kwa miaka yote hii, ni a big lie!. Tanzania we are an existing lie!, Tanzania, we are a living a lie and we continue living lie till to date!.
- Hivyo kufuatia huu mchakato wa katiba mpya unaoendelea, pia natoa wito kuwa sasa ni wakati muafaka, pia turekebishe makosa tulioyafanya huko nyuma, lets make things right kwa Tanzania kuwa na Mkataba halali kabisa wa Muungano ambao njia pekee ya kuupata ni kupitia referandum, hivyo wakati tukipiga kura ya katiba mpya, tupigie na kura ya referendum ya muungano wetu ili sasa kuuhalalisha huu muungano bandia uliopo!.
https://www.google.com/url?sa=t&sou...cQFnoECBgQAQ&usg=AOvVaw1rq5EAFapufDcpElW4fsdJ
Asanteni na Happy New Year!
Pasco.