Rais Samia: Wananchi muache kuwachagua wanaowapa khanga na hongo hao sio wawajibikaji

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,064
49,751
Wakuu habari zenu.

Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa JMT Samia SH amesema Chama hicho kikubwa na makini kitawachuja na kuwaengua Wabunge wote ambao hawawajibiki Kwa Wapiga kura wao na wanaosababisha chama kupakwa matope.

Kwa mustakabali wa CCM na Taifa ni vyema tumsaidie Mwenyekiti kuwataja Wabunge ambao hawawajibiki Kwa Wananchi na chama Chao.

Listi Inaanza na Hawa,unaweza ongeza na wengine 👇

1. Luhaga Mpina (Kisesa)
2. Hammis Kigwangala (Nzega Vijijini)
3...
Unaweza ongeza na wengine

My Take: Hakuna Ubunge wa Mseleleko 2025.

============

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema chama hicho kitawapima viongozi wao wakiwemo wabunge, wawakilishi na Madiwani kutokana na utendaji kazi wao kama ambavyo ilani ya CCM ilivyoahidi kuwaletea maendeleo wananchi wake

Rais Dkt. Samia ameeleza hayo wakati akizundua kituo cha wajasiriamali kilichopo Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja kilichojengwa na Mwakilishi wa viti Maalum UWT kupitia Mkoa huo na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Riziki Pembe Juma

Akiwa katika eneo hilo Dkt Samia amewataka wana-CCM kuwachagua viongozi wanaowajibika na kuacha kurubuniwa kwa kanga na fedha huku shughuli za maendeleo zikizorota

Amesema chama hicho kitataka kupata tathmini na kujionea juu ya hatua za maendeleo zilizofanywa na viongozi hao

Akiyataja mafanikio yatakayopatikana katika kituo hicho cha Wajasiriamali ni pamoja na kuwawezesha wananchi kiuchumi kupata shughuli rasmi ya kujiingizia kipato huku akiahidi kuongeza idadi ya Cherehani kwaajili ya kuendeleza harakati za kituo hicho

Dkt. Samia amehitimisha ziara yake leo katika mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo kesho atamalizia ziara hiyo katika mkoa wa Kusini Unguja, Mjini na Magharibi.

==========For English Audience Only==========​

President Samia Emphasizes Accountability Towards Election Season

The National Chairperson of the Chama Cha Mapinduzi (CCM) and the President of the United Republic of Tanzania, Dr. Samia Suluhu Hassan, has announced that the party will assess the performance of its leaders, including Members of Parliament, representatives, and councilors, based on their work, as outlined in the CCM manifesto promising development for its citizens.

President Samia made these remarks during the inauguration of an entrepreneurial center in Mahonda, North Unguja, constructed by the Special Seat Representative of UWT for the region and the Minister of Community Development, Gender, Elderly, and Children, Riziki Pembe Juma.

She further urged citizens to choose responsible leaders and avoid being swayed or corrupted by material things, emphasizing the need for sustained development efforts. The President mentioned that the party aims to assess and evaluate the progress made by its leaders in fulfilling the promises outlined in the CCM manifesto. Notable achievements expected at the Entrepreneurial Center include economic empowerment for citizens and the formalization of income-generating activities. President Samia pledged to increase the number of sewing machines to further support the center's initiatives.

View: https://youtu.be/sr8TOTZwZo4?si=lplOV1SmplGf6ShT
 
..Na yeye Samia achujwe?

..kwanza uwezo wa kiutendaji hana.

..pili ni kiongozi laghai asiyekuwa na msimamo.
Unapimaje huo uwezo wake wa kiutendaji? Au unatumia Kipimo Cha chuki binafsi? Thibitisha hapa
 
Wakuu habari zenu.

Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa JMT Samia SH amesema Chama hicho kikubwa na makini kitawachuja na kuwaengua Wabunge wote ambao hawawanibiki Kwa Wapiga kura wao na wanaosababisha chama kupakwa matope.

Kwa mustakabali wa CCM na Taifa ni vyema tumsaidie Mwenyekiti kuwataja Wabunge ambao hawawajibiki Kwa Wananchi na chama Chao.

Listi Inaanza na Hawa,unaweza ongeza na wengine

1. Luhaga Mpina (Kisesa)
2. Hammis Kigwangala (Nzega Vijijini)
3...
Unaweza ongeza na wengine

My Take: Hakuna Ubunge wa Mseleleko 2025.

============

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema chama hicho kitawapima viongozi wao wakiwemo wabunge, wawakilishi na Madiwani kutokana na utendaji kazi wao kama ambavyo ilani ya CCM ilivyoahidi kuwaletea maendeleo wananchi wake

Rais Dkt. Samia ameeleza hayo wakati akizundua kituo cha wajasiriamali kilichopo Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja kilichojengwa na Mwakilishi wa viti Maalum UWT kupitia Mkoa huo na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Riziki Pembe Juma

Akiwa katika eneo hilo Dkt Samia amewataka wana-CCM kuwachagua viongozi wanaowajibika na kuacha kurubuniwa kwa kanga na fedha huku shughuli za maendeleo zikizorota

Amesema chama hicho kitataka kupata tathmini na kujionea juu ya hatua za maendeleo zilizofanywa na viongozi hao

Akiyataja mafanikio yatakayopatikana katika kituo hicho cha Wajasiriamali ni pamoja na kuwawezesha wananchi kiuchumi kupata shughuli rasmi ya kujiingizia kipato huku akiahidi kuongeza idadi ya Cherehani kwaajili ya kuendeleza harakati za kituo hicho

Dkt. Samia amehitimisha ziara yake leo katika mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo kesho atamalizia ziara hiyo katika mkoa wa Kusini Unguja, Mjini na Magharib
Ata yeye anatakiwa achujwe!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom