Unajua athari na jinsi ya kujiepusha na matumizi ya Bangi?

May 2, 2023
5
3
Chawa si nzito lakini husumbua, wahenga walikuwa na maana Matatizo madogo madogo yasipodhibitiwa tangu awali huweza kusumbua na kusababisha matatizo makubwa zaidi lakini pia kwa namna nyingine Hutumika kuwatahadharisha wale the wenye tabia ya kudharau matatizo madogo madogo kwani huweza kuongezeka na kushindwa kutatulika.

Vijana wengi wameweza kujikita katika makundi mbalimbali ambayo ni hatarishi kwa maisha ambayo bila ya kuchukua hatua mapema kubadilika ama kujitambua wamejikuta kuangukia katika changamoto na kushindwa kujikwamua kabisa.

Moja ya mambo yanayowakabiri vijana ni matumizi ya Bangi, Mmea wa bangi umekuwa ukitumiwa na binadamu kwa zaidi ya miaka elfu moja Ingawa inajulikana zaidi kwa matumizi yake kama burudani ambayo inavutwa au kumezwa, pia imehalalishwa kwa matumizi ya dawa za matibabu katika nchi mbalimbali duniani.

Aidha Waziri mkuu Kassim Majaliwa aliweza kuongelea kuhusu kupiga vita vya matumizi ya bangi na mirungi na matumizi ya madawa ya kulevya na kuweza kusema dawa ya kulevya na bangi zimeweza kutumika kwa wingi aina ya bangi kama vile chaArusha pamoja na sakanka ambazo zimeweza kusababisha madhara makubwa kwa vijana kuweza kuwa na urahibu wamatumizi hayo ya bangi na kufanya vijana kuwa vichaa na taifa kupoteza nguvu kazi.

" Dawa ya kulevya na bangi zimeweza kutumika kwa wingi aina ya bangi kama vile chaArusha pamoja na sakanka ambayo imeibuka hivi karibuni ambayo inawafanya watumiaji wengi kuwa vichaa" Alisema Majaliwa.


Pia Tatifi tatu za zilizochapishwa na majarida ya Psychopharmacology, jarida la Neuropsychopharmacology, na International Journal of Neuropsychopharmacology inaonesha jinsi matumizi yake yanavyoweza kuathiri hatua za utambuzi na kisaikolojia.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Dawa na Uhalifu liliripoti kuwa takriban watu milioni 192 duniani kote kati ya umri wa miaka 15 na 64 wanatumia bangi kwa burudani, kulingana na takwimu za 2018.

Matumizi ya bangi yanaweza kuwa na athari mbaya kwenye akili, utambuzi, hisia, na afya ya akili baadhi ya madhara yanayoweza kutokea kutokana na matumizi ya bangi.

Matumizi ya bangi yanaweza kuathiri mfumo wa utambuzi, kusababisha utendaji duni katika majukumu ya kila siku kama kazi au masomo pia Watu wanaotumia mara kwa mara wanaweza kukumbwa na tatizo la ugonjwa wa utambuzi.

Mmoja wa mwanafunzi anasoma katika chuo kikuu cha Iringa katika kozi ya saikologia ngazi ya stashahada Joel Moleli ameeleza kuwa matumizi ya bangi ni hatari kwa afya ya mwili na akili kwa ujumla kwa kuwa inaweza kumfanya mtumiaji kuwa na matatizo ya kiakili kwa baadae.

"Bangi sio nzuri kiafya maana inaweza kufanya vijana kuweza kupata ukichaa kutokana na kama ijulikanavyo vijana ndio tegemeo kwa taifa utumiaji huo wa bangi pia unarudisha taifa nyuma kimaendeleo kwa kuanza kutumia kiasi kikubwa cha fedha kusaidia matibabu kwa waadhirika" Alisema Moleli.

Bangi inaweza kuathiri jinsi tunavyohisi na kufikiri Matumizi yake yanaweza kusababisha anhedonia (kutokuwa na uwezo wa kusikia raha) na matatizo mengine ya afya ya akili.

Matumizi ya bangi yamehusishwa na matukio ya kisaikolojia, ikiwa ni pamoja na schizophrenia aidha Inaweza kuongeza hatari ya dalili za kisaikolojia, hasa kwa wale walio na mwelekeo wa hali hizo.

Kwa upande mwingine Kujiepusha na urahibu wa bangi ni muhimu ili kulinda afya yako kuelewa madhara yatokanayo na matumizi ya bangi ili uweze kutambua hatari zake kama vile Kuepuka mazingira au watu ambao wanaweza kukuvutia kutumia bangi.

Mmoka wa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Iringa katika kozi ya Elimu shahada Mariam Said alisema ni vema Kutafuta Msaada wa Kisaikolojia Ikiwa unapata tabu katika kuacha matumizi, tafuta usaidizi wa kitaalam ili kupata msaada unaohitajika.

Kutokana na kupata shida jinsi ya kuacha kutumia bangi ni vema kuweza kupata msaada wa kisaikologia na kuweza kupata huduma ilikuweza kuachana na urahibu huo" Alisema Said.

Ni muhimu kuelewa kwamba athari za bangi zinaweza kutofautiana kwa kila mtu na kutegemea mambo mengi, watu wanapaswa kujua hatari zinazohusiana na matumizi ya bangi na kuzingatia afya zao na ustawi wao kabla ya kutumia au la.
 
Aisee mimi ninaunga mkono ila wengi kuacha lazima uwe na alternative labda mazoezi au kubadilisha circle na maeneo unayohang au kutembelea
 
Bangi sio mbaya ila wewe mvutajaji ndo mbaya pia ganja haipo kwa kila mtu.i smoke weed everyday nna zaidi 20yrs an feel blessed man.!
 
Watoto wengi sana wa kike wamejiingiza kwenye uvutaji wa bangim imekua kama style siku hizi. Maofisini vijana wengi wanavuta bangi. Mitaani ndio usiseme.

Sijawahi kuona umuhimu wa stimu ya bangi.
 
Back
Top Bottom