Je vaginismus inatibika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je vaginismus inatibika?

Discussion in 'JF Doctor' started by Amyner, Aug 12, 2011.

 1. Amyner

  Amyner JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 2,404
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Wandugu naomba msaada wenu mnijulishe iwapo vaginismus inatibika? Kama ndio, kwa tiba ipi na inapatikana wapi hapa tanzania.
   
 2. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Vaginismus ni condition rare kidogo...labda kwa sababu huku kwetu hakuna statistics, na ni ugonjwa ambao mwanamke anaweza hasiwe comfortable kuuongelea kwa daktari au mtu mwingine..mara nyingi wanawake huwa wanadhani ni kosa lao, au ndio walivyo na hivyi kutotafuata msaada.

  Vaginismus inatokea pale msuli ambao uko ndani ukeni unaitwa kwa kifupi 'PC muscle' (PuboCoccygeus muscle) unakuwa unakaza as a reflex reaction to any sort of penetration (uume, kidole, tampoon etc). Reflex ni reaction ambayo inatokea bila mwanadamu kuamua (involuntary), kwa hiyo huo msuli unapokaza sio kwamba mwanamke mwenyewe anaamua kuukaza.

  Vaginismus inaweza ikawa 'primary' iwapo mwanamke hajawahi kuingiliwa na kitu chochote ukeni kwa sababu ya hiyo reaction, au 'secondary' iwapo mwanamke alishawahi kuingiliwa mara kadhaa halafu baadae ndio anakuja pata hilo tatizo. Matibabu yake ni tofauti.

  Primary mara nyingi inaweza tokana na magonjwa mfano ya zinaa, UTI sugu au mara kwa mara, jaribio la kubakwa (attempted sexual abuse), kuona mwanamke mwingine akibakwa (witnessing sexual abuse), domestic violences, kuogopa kuingiliwa kimwili mfano kwa mabikra (fear of penetration), hofu (naxiety), stress etc.


  Secondary mara nyingi husababishwa na psychological factors mfano kubakwa, kuumizwa wakati wa kujamiiana mara ya kwanza (kutolewa bikra) etc.


  Matibabu ya vaginismus yanategemeana na aina (primary/secondary) na/au sababu iliyopelekea tatizo lenyewe. Kama kuna ugonjwa basi unatibiwa, halafu baadae unapata psychological counselling. Wenye primary vaginismus huwa wanaweza kuhitaji procedure inaitwa 'desensitization' kwa kutumia vipanua uke (vaginal dilators). Ambapo mwanamke anawekwa kwenye sessions kadhaa ambazo akija clinic daktari/nurse/physiotherapist aliyepata mafunzo kwenye hiyo procedure anakuwa anamuiningiza dilators ukianzia size ndogo inaenda ukiongeza size kwenye session tofauti mpaka mwanamke anazoea.

  Vaginismus inatibika na uwezekano mkubwa tu wa mwanamke kuendelea kuenjoy penetration..
   
 3. Amyner

  Amyner JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 2,404
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Asante sana kwa ufafanuzi mzuri kaka riwa..
   
Loading...