A
Anonymous
Guest
Habari,
Naomba suala hili lifanyiwe uchunguzi.
Tarehe 16 nilifika Stendi ya Somanda, Bariadi, Simiyu, ambapo nilitakiwa kulipa shilingi 300 kama ada ya kuingia stendi. Baada ya kulipa, nilimwomba mlinzi anipe risiti, lakini aliponipa niligundua kuwa risiti hiyo ilikuwa ya tarehe iliyopita (siyo ya tarehe niliyolipa) na pia haikuwa inaonesha taarifa sahihi ya gari/pikipiki yangu.
Hali hii imenifanya kujiuliza: Je, hizi fedha za ada tunazolipa zinafikishwa serikalini kama inavyotakiwa, au zinaishia njiani?
Naomba mamlaka husika zifuatilie matumizi na utoaji wa risiti katika stendi hii ili kuhakikisha fedha za wananchi zinakusanywa na kutumika kwa uwazi.