Tuhuma inayoharibu future kwa maumivu makubwa. Je, Serikali ina la kujifunza?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
172,415
2,000
Hii ni simulizi ya kutia huzuni mno ya mhanga wa kusingiziwa tuhuma aliyekaa gerezani mahabusu kwa miaka tisa.. Pengine katiba mpya itarekebisha haya mapungufu ya kisheria.

Kipindi cha pili na cha mwisho cha utawala wa hayati Benjamin Mkapa kulikuwa na matukio mengi sana ya uvamizi wa kwenye mabenki, taasisi za fedha na maduka mbalimbali kwa kutumia silaha.

Mojawapo ya matukio ya kukumbukwa sana ni lile la uvamizi wa ubungo gari aina ya landcruiser hard top lililokuwa limebeba pesa za bank ya NMB zikisafirishwa kwenda Morogoro nadhani.

Kwenye ule mtiti walikufa wengi wasio na hatia na walikamatwa wengi wasio na hatia pia.. Mmojawapo ndio huyu ndugu ambaye ndio kwanza harusi yake ilikuwa na mwaka mmoja huku akiwa amejaaliwa mtoto mmoja .. Wakati wa tukio mtoto alikuwa na umri wa miezi minne.

Askari kanzu walimwagwa mitaani kupeleleza wahusika wa tukio lile... Mtu mmoja asiyefahamika akamtaja huyu jamaa kuwa anamshuku kutokana na lifestyle yake.

Anasema jamaa ni mtu wa bata sana na hajulikani pesa anapata wapi na shughuli zake ni zipi.. Kama utani jamaa akadakwa yeye pamoja na mkewe na mtoto wao mchanga.. Siku wanamkamata ilikuwa tarehe 1.4 hivyo jamaa akadhani ni maskhara kutokana na tarehe husika.

Walikaa mahabusu kwa wiki nzima kisha mkewe na mtoto wakaachiwa huru akabaki jamaa.. Alijipa matumaini kuwa naye atatoka soon kwakuwa hakuwa na hatia yoyote.. Mwaka ukakata akiwa mahabusu.

Upelelezi ukaendelea na wahusika wote wakakamatwa. Lakini jamaa hakuachiwa. Huko nyumbani mambo yakazidi kuharibika.. Mkewe na mtoto wakafa kwenye ajali ya moto nyumbani kwao. Jamaa hakuweza kwenda kuzika wapendwa wake
Maumivu yakawa juu ya maumivu.

Mwaka wa tatu akiwa anasoma kitabu cha SAMEHE NA SAHAU akashukiwa na Neema ya Mungu na kuokoka..akajihisi ametua mzigo mzito sana.. Aliwasamehe wale wote waliomletea matatizo yote yale.

Mwaka wa nne watuhumiwa halisi wa ile kesi walihukumiwa wote vifungo tofauti tofauti lakini huyu ndugu bado akawa yuko ndani. Kukoleza maumivu kwenye kidonda akampoteza dadaake wa pekee ambaye ndio lilikuwa tegemeo lake la mwisho baada ya mkewe kufariki.

Mambo yalizidi kuwa magumu kule mahabusu gerezani kukiwa na matukio mengi yenye kuumiza sana. Ni baada ya miaka 9 kamili ndio aliachiwa huru baada ya kukosekana ushahidi wa kumtia hatiani.

Niki ni kisa cha kweli cha kuumiza na kufikirisha sana! Je tuna sheria ya kuwalinda watu wanaosingiziwa mambo mabaya? Je tuna sheria ya kuwaadhibu watu wanaosingizia wengine mambo mabaya?

Kuna watu hata sasa wako mahabusu kwa kesi za kusingiziwa.

Kuna watu hata sasa wako wanatumikia vifungo vifupi na virefu kwa kesi za kubambikiwa!

Kuna watu wamehukumiwa adhabu za vifo kwa tuhuma ambazo sio zao.. Wamesingiziwa. Wamebambikiwa!
 

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
4,134
2,000
IMG_8365.jpg


Hii picha ndivo inaonyesha watu walivyo.wanataka muwe sawa.kisa cha jamaa na jamii iliyomzunguka.

IMG_8480.jpg

Alafu wanakuacha kwenye maisha ya andhaa kaanoon.

Unanikumbusha hii sinema hii.pale amita bachan alipopewa kesi kuwa kafanya mauaji na kupigwa kifungo.
Miaka ilipokwenda akaachiwa huru.

Siku yupo mtaani kakutana na marehemu anapiga kampeni,marehemu kuona tu ni yule jamaa,wacha akimbie basi marehemu kila akikutana na watu kuomba msaada ndio wale waliomsingizia na kusimamia kidete kufungwa kwa amita.

Marehemu akaona bora kukimbilia mahakamani,kufika mahakamani ,yule hakimu ndio aliyemfunga amita. Amita akampokonya jambia mlinzi na kumcharanga jamaa mpaka kifo mbele ya mahakama.

Hakimu kashikwa na kigugumizi “maana uliyesema aliyemuhua mpaka kumfunga na kutumikia ndio leo kauliwa”

Hii sinema inafunzo sana
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
7,623
2,000
Muhimu ni kesi ziwe zinasikilizwa kwa wakati, tabia ya kuchelewa kusikiliza kesi ndio inawasababishia wengi maumivu wasiyostahili.

Sijajua kwa nini huyo jamaa kama washukiwa wengine wa lile tukio walikamatwa na kufungwa, kwanini nae hakujumuishwa kwenye hiyo kesi ili ushahidi uliotolewa mahakamani uoneshe hakuhusika na tukio ili aachiwe?

Hapa napo naona kuna udhaifu mkubwa kwenye mahusiano kati ya magereza yetu na mahakama, inawezekana huyo jamaa alikuwa gereza tofauti na watuhumiwa wengine na hapakuwepo na mawasiliano kati ya mahakama na magereza, au kati ya gereza moja na jingine, hii ni kwasababu watuhumiwa walikamatwa kiholela kila mmoja na siku yake.
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
172,415
2,000
Muhimu ni kesi ziwe zinasikilizwa kwa wakati, tabia ya kuchelewa kusikiliza kesi ndio inawasababishia wengi maumivu wasiyostahili.

Sijajua kwa nini huyo jamaa kama washukiwa wengine wa lile tukio walikamatwa na kufungwa, kwanini nae hakujumuishwa kwenye hiyo kesi ili ushahidi uliotolewa mahakamani uoneshe hakuhusika na tukio ili aachiwe?...
Jamaa kabla ya mkewe kufariki, ndio alikuwa mfuatiliaji mkubwa kwa kusaidiana na wifi yake... Halafu wote wakafariki..hiki kisa kinatatiza sana
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
172,415
2,000
Muhimu ni kesi ziwe zinasikilizwa kwa wakati, tabia ya kuchelewa kusikiliza kesi ndio inawasababishia wengi maumivu wasiyostahili.

Sijajua kwa nini huyo jamaa kama washukiwa wengine wa lile tukio walikamatwa na kufungwa, kwanini nae hakujumuishwa kwenye hiyo kesi ili ushahidi uliotolewa mahakamani uoneshe hakuhusika na tukio ili aachiwe?...
Maneno ya mwisho ya George Stiney kijana wa miaka 14 aliyesingiziwa kumuua binti wa kizungu
[Why Would They Kill Me for Something I Didn’t Do?’]
It was the question a 14-year-old innocent black teen asked before being executed in 1944’s Jim Crow South. And it’s a question the Square One Project — which recently held its first roundtable in North Carolina — continues to grapple with.

Screenshot_20210817-095940.jpg
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
172,415
2,000
View attachment 1895224

Hii picha ndivo inaonyesha watu walivyo.wanataka muwe sawa.kisa cha jamaa na jamii iliyomzunguka...
Why Would They Kill Me for Something I Didn’t Do?’

It was the question a 14-year-old innocent black teen asked before being executed in 1944’s Jim Crow South. And it’s a question the Square One Project — which recently held its first roundtable in North Carolina — continues to grapple with
 
Jul 28, 2020
21
45
Hii ni simulizi ya kutia huzuni mno ya mhanga wa kusingiziwa tuhuma aliyekaa gerezani mahabusu kwa miaka tisa.. Pengine katiba mpya itarekebisha haya mapungufu ya kisheria....
Hii ni dalili ama ishara kuwa wapo wengii wanaoteseka magerezani kwa kesi za kubambikiwa ikiwa ni pamoja na walioshtakiwa kabisa ila hawakuhusika katika matukio hao pia ambao wapo mahabusu kwa muda wa miaka kadhaa wakisubiri upelelezi ukamilike
 

Mamndenyi

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
32,916
2,000
Ni ile hujafa hujaumbika.

Maisha ni fumbo.

Ona Mbowe anavyotaabishwa sasa, Mungu ndiye anayejua. Swali je ni lini Mungu atapita huko magereza, wapo wengi wanateseka kifungoni ili mtu fulani afurahi tu. Je Mungu utanyamaza mpaka lini.

Tunao vijana wamepotea na mifupa ni heri hata wangefariki ili wazazi au familia wazike.

Mamndenyi unaongea mno, duuu
 

Mtukutu wa Nyaigela

JF-Expert Member
Sep 4, 2018
3,658
2,000
Hii ni simulizi ya kutia huzuni mno ya mhanga wa kusingiziwa tuhuma aliyekaa gerezani mahabusu kwa miaka tisa.. Pengine katiba mpya itarekebisha haya mapungufu ya kisheria...
Mkuu mi nakumbuka wasiohusika walichujwa within two years wakawa wametoka, na hii ni baada ya mmoja wa wahusika ku confess na kueleza tukio zima lilivyopangwa pia akataja na wahusika. hivyo wasdiohusika wakatolewa.

Sasa kwamba huyu yeye alikaa miaka tisa ,hiyo ni mpya
 

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
172,415
2,000
mkuu mi nakumbuka wasiohusika walichujwa within two years wakawa wametoka, na hii ni baada ya mmoja wa wahusika ku confess na kueleza tukio zima lilivyopangwa pia akataja na wahusika. hivyo wasdiohusika wakatolewa
sasa kwamba huyu yeye alikaa miaka tisa ,hiyo ni mpya
Ndio hivyo na watuhumiwa walihukumiwa baada ya miaka minne... Yeye alikaa lupango mpaka miaka 9
 

Malchiah

JF-Expert Member
Feb 10, 2021
921
1,000
Chuki,wivu na kijicho ni vitu vinawatesa watu wengi na kupelekea haya yote.

Pia sheria zetu nyingi hazipo fair kwa mtuhumiwa,yaani mtuhumiwa anachukuliwa kama mhalifu. Kabla ya katiba mpya ipo haja ya vyombo vyote vinavyohusika na mienendo ya kesi kufundishwa/kuelimishwa namna ya kushughulikia kesi na uendeshaji mzima wenye uwazi.
Haiwezekani kesi ya wizi wa kuku ichukue miaka miwili kwenye upelelezi,kuna namna serikali inahusika kubariki vile vyombo ya ulinzi vinavyowaadhibu watuhumiwa.

Asanteee kwa ku-share nasi, muhimu tuishi na watu kwa akili na tuepuke kuhukumu watu bila ushahidi, familia nyingi zimeingia katika umaskini uliokithiri na kusababisha vifo sababu ya sheria zetu kandamizi.
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
9,650
2,000
mkuu mi nakumbuka wasiohusika walichujwa within two years wakawa wametoka, na hii ni baada ya mmoja wa wahusika ku confess na kueleza tukio zima lilivyopangwa pia akataja na wahusika. hivyo wasdiohusika wakatolewa.

sasa kwamba huyu yeye alikaa miaka tisa ,hiyo ni mpya
Mumlipe fidia sasa kudadeki!! Kha!!!! Na huyo mke na mtoto wake, ikibidi nao muwafufue!!

Haiwezekani kila siku Lengai Ole Sabaya abebwe kwenye landrover pickup kama Mtalii vile kwenda mahakamani, halafu Watuhumiwa wengine wakose gari la kuwapeleka Mahakamani huko huko katika dunia hii ambayo magari siyo big issue kabisa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom