Je Unazo Siri Ambazo Hutozisema Hadi Ukifa?

VUVUZELA

JF-Expert Member
Jun 19, 2010
3,103
782
Ni matumaini yangu kuwa nyote muwazima na mnajiandaa na maandilizi mema ya weekend. Kwa muda mrefu sana toka nikiwa mtoto hadi nimekuwa mtu mzima sasa nimeshawahi kusikia mara nyingi sana kutoka kwa watu wa umri tofauti, rangi tofauti, mila tofauti, nchi tofauti wazee kwa vijana na wanawake na wanaume wakiongelea kuwa wanazo siri ambazo hawatozisema na watakufa na kuzikwa nazo. Wapo waliodai watazianika baadae ktk maisha yao kabla mauti haijawakuta.
Wapo ambao wameweza kuziweka wazi lakini anonimously na hivyo wamezianika bila watu kufahamu hizo siri zimetoka kwa nani. Binafsi sina.
Swali:
1. Je unayo siri ama unazo siri ambazo utakufa nazo na kuzikwa nazo kaburini bila ku-confess kwa mtu yoyote yule wakati wa uhai wako?
2. Je unaweza kuzisema hapa jamvini hata kama just in brief?

Weekend njema!!
 
SHERRIF ARPAIO

JF-Expert Member
Aug 25, 2010
9,542
5,852

Naamini 100% kuwa kila binadamu anazo siri ama habari nyeti ambazo atakaa nazo na atazikwa nazo. Kuna sababu mbalimbali ambazo zinachangia kutozisema kama vile kuogopa kuvunja ndoa, mahusiano, kutenganisha familia ama hata kwenda jela ama kulipiziwa kisasi. Unaposema hapo juu kwenye red eti wewe binafsi huna sidhani kama uko honest. Kila member humu JF anazo na deep down kila mtu analijua hilo na dhamira zinatusuta rohoni
 
Chauro

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
2,970
1,470
sio kila jambo la kusema na hata yale nayosema sio kwa watu wote kuna mtu unaweza jisikia kushare nae jambo fulani lakini usiweze kumueleza mtu mwingine yeyote maisha.
 
Husninyo

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
23,788
9,115
Kuna siri zangu mwingine naweza mweleza ila mwingine siwezi. Mambo mengine unaweza fanya siri yakabumbuluka kwa hiyo inakuwa sio siri tena.
 
VUVUZELA

JF-Expert Member
Jun 19, 2010
3,103
782
Kuna siri zangu mwingine naweza mweleza ila mwingine siwezi. Mambo mengine unaweza fanya siri yakabumbuluka kwa hiyo inakuwa sio siri tena.

Kuna watu wengine wanaaminiwa kuambiwa siri na hawazitoi hata uwaue
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom