Je Unatumia Bolt Business katika Biashara yako?

Je Unatumia Bolt Business katika Biashara yako?

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,913
Reaction score
6,603
Moja kati ya huduma ya kipekee ambayo nimekuwa nikitumia ni huduma ya BOLT Business

Kwa wajasiriaali wengi ambao biashara zao huwahitaji kusafiri kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine uhitaji wa huduma bora ni moja kati ya jambo la muhimu sana,Mara nyingi baadhi yao hulazimika ama kusafiri na magari yao au kujikuta wakitumia gharama kubwa sana katika usafiri.

Changamoto kubwa zaidi wanayopata ni pale ambapo wanataka sasa kuweka gharama za usafiri kama sehemu ya gharama za uendeshaji katika taarifa zao za kodi.Wengi hujikuta na changamoto ya kutokuwa na records zote za gharama pamoja na risiti za efd kwa ajili ya kutunza records zao.

Kwa Wafanyabiashara wajanja,huduma ya BOLT Business ni huduma nzuri ambayo kila biashara inapswa kujiunga nayo kwani inasifa nyingi za kipekee kama hifuatavyo:

simamizi na Uthibiti wa Gharama

  • Bajeti ya Pamoja (Centralized Billing): Kampuni inapokea ankara moja tu ya mwezi (monthly invoice) badala ya kulipia kila safari tofauti au kurudisha fedha za usafiri kwa kila mfanyakazi (reimbursements).
  • Kuweka Mipaka ya Matumizi: Unaweza kuweka viwango vya mwisho vya matumizi (spending limits), muda maalumu wa kusafiri (mfano: saa za kazi tu), au maeneo maalum ambapo mfanyakazi anaruhusiwa kutumia huduma hiyo.
Urahisi wa Utawala (Administrative Efficiency)

  • Dashibodi Moja (Admin Dashboard): Inampa meneja au kitengo cha fedha uwezo wa kuongeza au kuondoa wafanyakazi kwenye mfumo kwa urahisi.
  • Ripoti za Papo kwa Papo: Unaweza kupakua ripoti za kina za safari zote zilizofanyika, nani alisafiri, na gharama zilizotumika bila kuhitaji risiti za karatasi.
  • Unapata Risiti za EFD kwa malipo ya gharama zote za usafiri kwa mwezi mzima
Urahisi na Usalama kwa Wafanyakazi

  • Bila Pesa Taslimu (Cashless Rides): Wafanyakazi hawahitaji kutumia fedha zao za mfukoni; wanachagua tu Wasifu wa Kampuni (Work Profile) kwenye programu yao ya Bolt wakati wa kuagiza gari.
  • Ufuatiliaji wa Usalama: Safari zote hufuatiliwa kwa GPS na kuna vipengele vya usalama vya dharura (SOS), jambo linaloongeza usalama wa watumishi wako wanapokuwa safarini.
 
Back
Top Bottom