Je, unatambua athari za majibu yako?

Tanzania Nchi Yetu Sote

JF-Expert Member
Mar 12, 2017
505
854
Kwa faida ya wengine...

Ijumaa iliyopita, nilikuwa darasani nikiwafundisha wanafunzi wangu ndipo mwanafunzi mmoja wa kike akainua mkono kuuliza swali. Nilimruhusu na akauliza swali rahisi sana ambalo nilidhani anapaswa kujua jibu lake maana tayari nilikuwa nimezungumzia mada hiyo wiki iliyopita.

"Kaa chini, tafadhari! Na sura yako mbaya! Muone!" ndilo jibu pekee nililompa. Darasa zima liliangua kicheko na alionekana kufedheheka sana.

Niliendelea na somo langu lakini nilihisi kuwa na hatia kwa sababu ya kile nilichokuwa nimesema. Nilimaliza kipindi changu na kuondoka.

Siku ya Jumapili, nilienda Kanisani. Mhubiri alikuwa akiongea juu ya nguvu ya ulimi.

Alizungumza juu ya jinsi unavyoweza kuwavunja moyo, kuwakatisha tamaa na kuwaangusha kabisa wengine kwa kile unachosema. Nilikumbuka kile kilichotokea Ijumaa na nikajiona ni mwenye hatia zaidi. Niliapa kuwa nitaenda kumuomba msamaha Jumatatu nikifika darasani.

Jumatatu alasiri, nilienda darasani lakini sikumuona yule mwanafunzi. Nilimuulizia kwa wenzake lakini hawakuonekana kujua ni nani hasa niliyekuwa nikimzungumzia.

Ndipo nikasema "ninamtafuta mtu niliyemtukana Ijumaa".

"Aah, huyo ni Furaha, mwalimu! Hayuko darasani leo"
walijibu.
Rafiki yake ni nani? Niliuliza.

"Aisha", walijibu. Lakini Aisha pia hayupo darasani.

Ghafla, msichana aliye na Hijab aliingia. "Mwalimu, huyo ni Aisha" wanafunzi wangu walinijulisha.

Yuko wapi rafiki yako? Nikamuuliza.
"Yupi?" Alijibu bila kunitazama usoni.
Furaha! Nilisema.

Yuko chumba cha kuhifadhia maiti. Alijibu.
Jibu hilo lilinishtua! Chumba cha kuhifadhia maiti ????? Kufanya nini hapo ?? Niliuliza.
"Alikufa Ijumaa" Aisha alijibu.
Imekuaje ?????? Niliuliza.

Baadaye niligundua kuwa baada ya kipindi changu Ijumaa, Furaha aligongwa na gari lililokuwa likienda kwa kasi. Alikuwa akivuka barabara bila tahadhari, labda kwa sababu ya kile nilichosema.

"Mazishi yake ni Jumamosi na umealikwa pia, mwalimu" Aisha aliendelea.

Wakati nilikuwa nimesimama nilijaribu kuudhibiti mshtuko niliokuwa nao, Aisha alisema huku akilia, "Mwalimu, umemuua rafiki yangu".

Alikuwa sahihi! Ninapaswa kuwa muuaji! Wasichana wengine darasani walikuwa tayari wanalia! Sikujua niseme nini, ikiwa ni kuomba msamaha kwa rafiki wa Furaha au kwa roho ya Furaha.

Niliwasilisha barua yangu ya kujiuzulu siku iliyofuata ikiwa na maneno haya: Wapendwa Wahadhiri na Walimu, tafadhali acheni kutukana wanafunzi wenu. Wako shuleni ili kujifunza kutoka kwenu. Ingekuwa tayari wanajua, wasingekuwa shuleni!

Tafadhali fikiria kile unachosema kwa watu wengine. Je! Maneno yako yanaleta uhai au kifo kwa wasikilizaji?

ZINGATIO: HADITHI HII NI LAZIMA ISOMWE NA HAIWAHUSU WALIMU TU BALI SISI WOTE TUNAPOKUWA TUNAWASILIANA NA BINADAMU WENZETU: WATEJA, WANAFUNZI, WAZAZI, WENZIO, MARAFIKI NA KADHARIKA

Yatupasa tuwe waangalifu sana juu ya jinsi tunavyosemezana.

Asante.👍👍
 
sina uhakika na ukweli wa story yako lakini ujumbe wake ni muhimu sana.

kwanza nirejee katika uhalisia wa sasa na kazi zote za wito,ualimu,uuguzi na utabibu,uaskari nk.

hizi kwa sasa zimegeuzwa kuwa kazi na si huduma kama zamani.

mashuleni kuna watu tunaamini ni walezi wa watoto lakini kumbe ni wahuni tu,mtoto anachelewa kila siku nayeye anamchapa kila siku badala ya kufuatilia ajue hata mtoto ana shida ipi.

hospitalini kuna wauguzi tunawategemea lakini ndio hawa unakwenda unavuja madamu kwa ajali wanauliza mtu anayemfahamu kwanza ndipo waendelee na matibabu

vituo vya polisi huko nako watu wamepewa dhamana, unakwenda unalia kwa kuonewa, kunyanyaswa au hata kudhalilishwa ulikotoka, unafika pale unafokewa kama mtoto au uliyeyataka yaliyokukuta.

wahenga wanasema kama umeshindwa kumfanya mtu afurahi tafadhali usimuumize.
 
sina uhakika na ukweli wa story yako lakini ujumbe wake ni muhimu sana.

kwanza nirejee katika uhalisia wa sasa na kazi zote za wito,ualimu,uuguzi na utabibu,uaskari nk.
hizi kwa sasa zimegeuzwa kuwa kazi na si huduma kama zamani.

mashuleni kuna watu tunaamini ni walezi wa watoto lakini kumbe ni wahuni tu,mtoto anachelewa kila siku nayeye anamchapa kila siku badala ya kufuatilia ajue hata mtoto ana shida ipi.

hospitalini kuna wauguzi tunawategemea lakini ndio hawa unakwenda unavuja madamu kwa ajali wanauliza mtu anayemfahamu kwanza ndipo waendelee na matibabu

vituo vya polisi huko nako watu wamepewa dhamana,unakwenda unalia kwa kuonewa,kunyanyaswa au hata kudhalilishwa ulikotoka,unafika pale unafokewa kama mtoto au uliyeyataka yaliyokukuta.



wahenga wanasema kama umeshindwa kumfanya mtu afurahi tafadhali usimuumize.
KAMA UMESHIDWA KUMFANYA MTU AFURAHI TAFADHARI USIMUUMIZE
 
Michael Jackson ameharibiwa na baba yake mzee jackson kwa kumwambia mwanae ana pua mbaya hili neno ndilo limepelekea hadi michael kuwa vile kujibadili.
 
Maneno ni Roho kamili, wanawake wengi sana hasa afrika uuwa destiny vipawa nyota za watoto wao kwa kuwatamkia maneno. Kupitia neno unaweza ua, unaweza ponya.
 
Akhsante sana mleta mada yaani utunge usiitunge hii Story kuna cha kujifunza kikubwaaa sana!....kuna ndg aliniletea story za kusimamishwa kwangu kazi tena za ghafla aseee nilijisikia vibaya sana!...…

mawazooo yalijaa moyoni ….midomo ilikakauka ghafla…... huenda mie ningegongwa na gari km huyooo mdada!! ajili ya ulimi mbovu wa ndg yangu wa damuuu!! toka nitoke! ! ambaye sasa amepooza…...

Yule angeniua!!!...kiukweli sikuwa na furaha lkn nilikaa nikatafakari weeee! kweli adui yako ni ndg kabisaaaaaaa
 
Back
Top Bottom