Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

'Hiyolela hiyolela hiyolea aah, Hiyolela hiyolela hiyolea na bolingo. Magagula na Lusonga sitaenda tena, maafande wa Mlale watanisurubu.'
Mhh jamani JKT kulikuwa na raha zake, Mlale hiyo Songea wimbo mmojawapo wa mchaka mckaka. Nakumbuka wimbo mwingine.
'Nalia yombwe nalia yombwe nalia yombwe nalia yombwe. Mama mbali Mlale mbali tukumbukane kwa barua na Baba mbali Mlale Mbali tukumbukane kwa barua.'
Utasikia afande Kuruta maliza hiyooo yaani muache kuimba nyimbo za masikitiko.
Ila umoja, ushirikiano, uvumilivu, usafi, ukakamavu, uzalendo nk. ni mambo muhimu niliyojifunza.
 
Mlale JKT- ruvuma jamani mko wapi? Kwa wenyeji kule chakula kebekebe tena ugali mkubwa wa makuruta shurti kusongwa na wanaume. Halafu ugali bure mnanunua tu mboga- maarufu kule kiti moto. Embakasi shamba la mahindi. Unapewa palilia mistari 3 ambayo unaona mwanzo tu mwisho wake huuoni.
Maafande: Nguvu ya Nyani ( a.k.a yake), Rweikiza, madame Grace ( Matron), Afande Sabuni, Mwaipopo, Mande??, Chuma n.k!
 
Nilikuwa operation miaka 30 ya uhuru Makutupora. Kuna magumu mengi na pia kuna mafunzo mengi. Nikikutana na nilokuwa nao shule na chuo huwa nafurahi but nikikutana na nilokuwa nsye jeshini huwa nafurahia zaidi maaba ni jambo la onky 1yr lkn lenye kumbux2 nyingi.
 
Uchaka.........that was the real part of JKT man.....sio siku hizi kuuza matrekta

camp+001.jpg

Hii wapi? waacheni watu wawe mafisadi. Watu wamechoka kama wafungwa.
 
Siku hizi hakuna mateso kivile, hakuna kubeba dunia wala kupigwa nuwa, watoto wanakufa kufa so wameamua kulegeza kuendana na wakati.
 
Mafinga jkt e coy kwa afande mangwembe we acha tu ,kwenye mziki tukiwa na lali wawa ,mbio ndefu tukiwa na nyoka,hiyo ilikuwa operation usafi kabla ya vita,na afande makona usisahau mp ngere, ee bwana acha tu ,mahindi ya kuchoma na uchinjaji wa kiti moto.mkuu wa kambi msilu, sharp shooter afande mwandemane.nyimbo kalebuse
 
Aise mimi nilikuwa kule Makutupora operesheni ni siri yangu. Yaani kuna jamaa wakati afande anauliza majina yetu akasema yeye anaitwa MBORO SULULU. Basi ilikuwa ni mshke mshike maafande wakadhani anawatania na kuwatukana . Jamaa aliteswa kisawasawa. Sasa huyo sijui yuko wapi huenda akawa ni profesa somewhere. I salute you MBORO SULULU wherever you are and if you are still alive.
 
Wengi mmeandika.............mengi tumekumbuka................kumbukumbu ni nyingi,...............................vituko ni vingi kwa kila kombania na kambi pia,............................. asanteni sana..........................ila kuna hawa kuruta waliopitia oljoro JKT..........kuna siku waliamua na kukutana,........................walifanya bonge la party.......ilikuwa maeneo ya mikocheni,......................hakika niliwaone wivu walivyokuwa wanajikumbsha mambo waliokuwa wakifanya wakati huo...............................hakika ni kitu kizuri sana.....................................hongereni kuruta wa OLJORO

Hao kuruta wa Oljoro walikuwa operation ipi? Mimi nilikuwa Okoa please update me
 
Umenikumbusha mbali sanaaaa.wale wa Operation Okoa Oljoro JKT kombania A kwa afande Dauda, John Matondo,Msambaa mmoja jina simkumbuki na afande mmoja mtu wa kusini alkuwa anapenda sana kuimba disko wa kombania C,kuokota kuni shimo la mungu majitambo ya maafande kuwa kuruta 10 wa jeshi kazi yao ni sawa na trekta moja la valmet na tela lake,kwata ya nguvu drill,mchakamchaka kula kwa foleni kimbembe ni pale unapozira chakula cha jeshi au mboga ni sangara au nyama kwata inakuwa kali kuliko0,wengine walipigwa bogi kwenda mgambo tanga waliotoroka na kurudi wanasimulia unyama wa afande Mtono,service wengine tulikatwa bogi kenda Itende nakumbuka ile siku tulipoimba disko kusherehekea kifo cha mtoto wa Meja ...... baada ya kughadhabishwa na matendo yake ya kutufanya wote pamoja na maafande kama kuruta,mtoto mwenyewe alishika waya wa umeme wakati wa greda likifanya cut&fill karibu na nyumba ya afande Rest House,kutulazimisha kuchimba mabwawa ya samaki katika makaburi ya wazungu walikuwa wamezikwa pale, kwa ujumla mwaka mmoja nilijifunza mambo mengi na nashukuru sana kuwa yananisaidia hadi leo hasa MM na ukakamavu.

Nilikuwa oljoro nikapigwa bogi la mgambo!
 
Nilikiwa Oljoro nikapigwa bogi la
Mgambo
 
Back
Top Bottom