Makala Jr
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 3,395
- 1,107
Wakuu...nawasalimu sana! Naomba tukumbushane tulikotoka na mtandao wetu pendwa wa Jamii forums.Katika kumbukumbu zangu,uzi wa kwanza kuusoma baada ya kujiunga JF ulikuwa unahusu ukabila nchini katika sekta mbalimbali haswa Ikulu,BOT na TRA.Makabila yaliyojadiliwa sana ni Wanyakyusa,Wachagga na Wahaya.Katika hitimisho la mjadala,nilijifunza kitu kimoja kwamba kuna aina ya propaganda chafu za kikabila ambazo wanaJF walizipinga na wanazipinga kwa maslahi ya taifa letu Tanzania...nakumbuka nilivutiwa sana ujengaji wa hoja zenye ushawishi wa kuleta umoja wa kitaifa kutoka kwa wadau mbalimbali. SASA:Naomba unikumbushe mdau...ni uzi gani ulikuvutia na kuchangia mawazo kwa mara ya kwanza?