Tukienda nyuma sana mnamo mwaka 1494 ugonjwa wa kaswende ulipatikana kwa wanajeshi wa ufaransa, ugonjwa huu ulikuwa ni mbaya sana kiasi ambacho ukiupata unatokwa na upele mwili mzima na kuanza kutoa usaha baada ya hapo ngozi huanza kutoka yote kuanzia usoni na baada ya miezi mitatu kwaheriiii!!
Kuna mtu alitengeneza vitambaa na kuviwekea chemical fulani na kujaribishia watu 1100 na kuona haiambukizi ( walivaa kama condom ila kwa kuwa ni kitambaa wanafunga na ribbon)
Condom zilianza miaka ya 1642 wakitumia utumbo wa Mbuzi na wanyama wengine(usicheke) kwa wanaume na kwa wanawake walitumia vibofu vya wanyama kuzuia mimba. Pia walitumia kwa kujikinga na maradhi.
Kwa hiyo swali lako hilo wengi hupuuza na kujipa faraja kuwa aah anasingiziwa