Je, Unafahamu kuhusu Allan Lucky?

bomouwa

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
1,149
798
Habari wanajamvi,

Leo nimemkumbuka kijana aliepata ajira EATV kupitia auditions za kiushindani na hatimaye akapata ajira na kuanza kipindi cha SKOOONGA!

Ni kijana mbunifu kwa kweli, kutokana na kutokua nyumbani kwa muda baada ya kurudi wiki iliopita nikaona kipindi kuna kijana mwingine.

Naomba kujua Allan ameachana na EATV au anamajukumu mengine ndani ya EATV.

Ahsante!
 
Baada ya kuoa aliacha kazi na alitangaza hadi kwenye ukurasa wake wa facebook, amepata mchongo mwingine.
 
Allan aliacha Skonga kitambo karibu miaka miwili imepita, jamaa alikuwa mkali, japo mi umri umesonga ila nilikuwaga naenjoi kukiangalia kipindi chake
 
Nyie mnasema mkenya kirahisi na mnaona sawa tu, ila wakenya wangesema Allan ni wao sio povu hilo kutoka, kuomba msaada wa kanusho mpaka wizara ya mambo ya nje. Tujikubali tunafanya vizuri.
 
Kwao ni Ruvuma mkuu
japo kwao ni ruvuma lakini allan ni fahari ya tanzania. laiti vijana wengi wa tz wangekuwa na ubunifu na iq kubwa kama yake soko la ajira la africa mashariki lingeomba poo kwa watz.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom